Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,757
- Thread starter
- #3,601
VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034
EPISODE 19
Nilitafakari ni namna gani nifungue maongezi yangu na Obama ili walau anipe nafasi ya haya mawazo ya ajabu niliyokuwa nayo kichwa ayasikilize.
"Unakumbuka siku ya kwanza nilipokuja humu?" Nikafungua maongezi kwa swali.
"Umekuja juzi tu hapa Ray, nakumbuka kila kitu mpaka jina lako nakumbuka" akanijibu kwa utulivu.
"Ulisema kwamba 'asset yeyote inapaswa kulindwa'! Unakumbuka?" Nikamuuliza tena.
"Unataka nini Ray?" Akaongea na kubadilika na kuwa 'serious'.
"Well tusema sasa ndio umefika wakati wa kuilinda 'asset'". Nikaongea kwa mafumbo nikiamini kuwa kama Obama alikuwa ni mtu ninayemfikiria kuwa ndiye basi atanielewa.
Hisia zangu zilikuwa zinaniambia kuwa Obama alikuwa ni kibaraka au tuseme ni afisa ambaye anatumiwa na Idara ya Usalama wa Taifa kuwapa taarifa wanazozihitaji kutoka humu gerezani. Hisia hii niliipata baada ya siku yangu ya kwanza humu gerezani, Obama alipotamka sentesi inayofanana kabisa iliyotamkwa na baba bite dakika chache kabla sijaletwa gerezani. "asset inapaswa kulindwa."
Na kwakuwa baba bite alionyesha dalili ya kwamba Usalama wa Taifa wana nia ya kunilinda humu gerezani basi nilikuwa na imani kama niko sahihi Obama ni pandikizi la usalama wa taifa, basi atakubali kunisaidia.
"Nakusikiliza!" Obama akanijibu tena akiwa na uso mkavu.
"Nahitaji funguo ya selo namba 46" nikaongea kwa uso mkavu.
"What?" Akaniuliza kwa mshangao.
"Nahitaji funguo ya selo namba 46! Selo ya Blaki" nikamueleza tena usoni nikiwa mkavu kweli kweli.
"Ya nini?" Akaniuliza huku bado akiwa na mshangao.
"Well, nadhani jambo la muhimu unalopaswa kufanya ni 'kukinda asset', hayo mengine niachie mimi!" Nikaongea kwa kujiamini sana kwa kuwa sasa nilikuwa naamini Obama ni pandikizi la Usalama wa Taifa hapa magereza.
"Ok! Hicho kitu unachokihitaji ni kitu sensitive sana kwahiyo angalau ungenieleza unakihitaji kwa ajili gani?"
"Na kwa Bahati mbaya hicho sicho pekee ninachohitaji.!!"
"Kuna lingine tena??" Akaniuliza kwa mshangao zaidi.
"Yes! Nahitaji umruhusu Msauzi aingize mzigo mkubwa wa bangi weekend hii.!!"
"Whaaaaaaaaa???" Obama alishtuka mpaka anainuka kutoka kwenye kiti.
"Siku kadhaa zijazo demand ya bangi humu jela itakuwa kubwa sana kwasababu kesho kuna kiasi kikubwa cha bangi kitateketea!! Kwahiyo ni fursa kwa Msauzi kufanya biashara wiki hii na kina blaki… Na kabla hujaniuliza chochote! Niseme kwamba, kwa siku hizi kadhaa ambazo nimekuwa ndani ya hili gereza nimejaribu kusoma vitu kadhaa humu! Bangi inapatikana kwa wingi sana, humu ndani ni mtu tu kuwa na hela ya kununulia au vipande vya sabuni.. Kwa upatikanaji huu kwa wingi wa bangi ni lazima kutakuwa na askari ambaye anafanya mchongo na blaki! Mzigo wa bangi ni wa huyo askari, lakini blaki kazi yake ni kuwauzia wafungwa.! Sasa ukiniuliza nifanye a wild guess ni askari gani anayeingiza humu bangi, basi nitakujibu ni Msauzi.. Yeye ndiye askari pekee mwenye personality na connection na wafungwa kumuwezesha kufanya hiyo biashara!"
Nikamdadavulia kwa kujiamini kabisa.
"Na tuseme kwa mfano nikapata namna ya kumsaidia Msauzi kuingiza bangi humu!! Sisi tunanufaikaje?" Akaniuliza.
Kwanza nikapenda akivyotumia neno "sisi". Nikahisi somo limeanza kumuingia.
"Nahitahi kesho umpange lindo la hapa jikoni muda wa mchana, na umpe maagizo afanye kile nitakachomuelekeza" nikamjibu kwa ufupi tu.
Obama akaitingishwa kichwa akiwa aamini kile ninachomueleza. Ni dhahiri kuwa alikuwa hajapenda mpango niliokuwa nao kichwani, lakini alikuwa anaonyesha dalili za mtu ambaye yuko tayari kukubali kufanya kile ninachopendekeza hata kama hapendi.
"And sijamaliza!" Nikaongea mwa kujishtukia huku natabasabu.
"Kumamaeee!! Bado kuna kingine??" Obama akatukana kwa hasira. Nikagundua kuwa alikuwa amekasirika kweli maana hakufanania na mtu mwenye kutukana tukana hovyo.
"Sinyorita" nikaongea kwa mkato.
"Hahahaha.! Unataka nikutongozee sinyorita??" Akacheka na kunikejeli kwa makusudi kupunga hasira zake.
"Trust me, sihitaji msaada wa kutongozewa.. Humu gerezani kuna kitu wanaita maharage ya kuoka! Nadhani unafahamu naongelea nini! Nataka umuwekee bili ya maharage ya kuoka kwa mwezi mzima angalau.!" Nikaongea huku natabasamu nikikaribia kucheka.
"Maharage ya kuoka kwa siku ni buku, so kwa mwezi ni thelathini hiyo tunaongelea" akaongea huku amekodoa macho.
"come on man!! Askari mwenye nyota mbili begani elfu thelethini kitu gani??"
"Alafu Sinyorita anatusaidia nini?"
"Utaona kesho!" Nikamjibu kwa mkato.
"Ray, unajua ungenieleza walau huo mpango wako nina weza kukusaidia mawazo!"
"Ubaya ni kwamba sihitaji unisaidie mawazo.. Nahitaji unisaidie kutekeleza mawazo yangu!" Nikamjibu huku naanza kuinuka pale kwenye kiti.
"Kesho mchana ikigonga kengere ya chakula, nitakuwa yard namba mbili nasubiri funguo ya selo namba 46."
Nikaongea kwa kujiamini huku nainuka na kuanza kuondoka kutoka ofisini kwa Obama.
"Fuuuuucccckk" nikamsikikia anajilalamikia.
Nikatoka kwenye ofisi huku natabasamu kimoyo moyo. Nikajua hapa nishapiga goli la tik tak.
Nikaelekea moja kwa moja mpaka yard namba mbili.
Nilipofika nikaanza kuangaza macho huku na huko kumtafuta Godi ambaye nilimuagize ahakikishe anakuwa na Sinyorita ili niongee naye.
Baada ya kutazama tazama sana, hatimaye nikawaona wamekaa nyuma ya mwembe pale yard. Nikatembea haraka kwenda mahali walipo.
"Wooow! Mnapendeza kinoma!" Nikawatania.
Sinyorita akaanza kutabasamu kwa aibu aibu kama mtoto wa kike, huku Godi akizungusha macho kwa kukereka.
"Ok! Sinyorita ndio huyu hapa, ongeeni ukimakiza utanikuta kule." Godi akaniharakisha niongee na kuondoka akionekana dhahiri anakereka na sisi kuonekana tumesimama na Sinyorita.
Nikaanza kumuelezea Sinyorita kila ninachotaka akifanye. Nikamueleza kwa taratibu sana na kwa tahadhari ili aendelee kunisikiliza mpaka mwisho asije akanikatisha kwa kuniporomoshea mitusi na kuondoka.
Maelezo yangu, nilianzia na ofa ya maharage ya kuoka mwezi mzima.
Ifahamike kuwa, humu gerezani kero kubwa ya chakula kuliko zote ni mboga. Kama ambavyo nilieleza awali kuhusu hali halisi ya maharage humu jela, unajaziwa kikombe kizima mchuzi lakini huyaoni maharage na ukiyabahatisha yametuama chini hazizidi punje kumi.
Dona linazoeleka na halikeri sana japokuwa linasagwa na vibunzi. Lakini dona bila mboga ya kulilia ni mtihani.
Kwahiyo wapishi jikoni (ambao ni wafungwa pia) kwa kushirikiana na askari anayesimamia jiko wameunda mradi wa magendo wa kupika maharage kidogo pembeni kwa kuyaunga kwa uzuri kama yanavyopikwa nyumbani. Maharage haya ndio yamepewa jina la utani 'maharage ya kuoka' humu gerezani na wanayauzwa shilingi elfu moja au vipande vitano vya sabuni.
Kwahiyo hiyo ndiyo ilikuwa chambo changu nilichokuwa natumia kumshawishi Sinyorita anisaidie katika mpango wangu. Kwamba atapata maharage ya kuoka mwezi mzima kila siku.
"Kwahiyo anifile kwasababu ya maharage ya kuoka?" Sinyorita akaongea kama anabana pua.
"Nooooo! Sio kukufila… ***! Nimekwambia unavua nguo tu ili askari wawakute wewe ukiwa uchi" nikaongea huku nasikia ukakasi mdomoni jinsi tunavyolitumia neno 'kufila' kirahisi rahisi.
"Mi staki bwana, naweza kuvua nguo akanifila kweli" Sinyorita akaanza kuleta mapozi.
Ilibidi sasa nianze kumbembeleza kama vile 'natongoza demu'. Nikatumia kama dakika ishirini nyingine kumshawishi mpaka hatimaye akakubali.
"Haya poa, ila nataka na ubwabwa kila jumamosi na jumapili.. Kama hutaki basi." Akaongea tena kwa kudeka kama anabana pua.
"Ok ok! Its done.. You got it" nikajisahau na kuropoka kingereza.
"Ndo nini?" Akakunja sura.
"Namaanisha poa! Nimekubali, utapata ubwabwa kila weekend"
"Nyoko zako! Ukiongea na mimi usiniletee vingereza vyako fala wewe!" Akanifokea kishangingi.
"Kuna lingine?" Akaniuliza huku ananiangalia kwa kunilegezea macho.
Nikajikuta nimeshikwa na aibu na kigugumizi. "No! Hakuna lingine"
"Una uhakika?" Akaniuliza tena huku amelegeza macho zaidi.
"Nishakwambia hakuna lingine! Muhimu tu usisahau kesho kengere ya chakula…….." Kabla sijamaliza akanikatisha.
"Eeeeeee babu weeee hebu nitue! nshakuelewa msyuuuuuuuuu" akongea na kumalizia na sonyo kisha akageuka na kuanza kuondoka kimiss.
"Fuuuucccckk! I really need to get out of here" nikajisemea kwa sauti ya chini chini nikimwangalia Sinyorita akiondoka baada ya kushuhudia vituko vyake.
Uzuri ni kwamba, sasa walau nilikuwa na uhakika mpango wangu unaweza kutekelezeka. Kila nilichohitaji, kilikuwa "kimeelekea kibla".
*********************
LEO
"Nimefanya mistake kubwa sana kumuamini Obama! ***..!! alinizidi akili" nikaongea kwa hasira huku natoka pale uchochoroni kuelekea yard namba mbili. Kaburu alikuwa ananifuata nyuma.
"Una maana gani sikuelewi"
"Kuna vitu alinisaidia, ikanifanya nimuamini! Nikaamini ni mshirika wa watu fulani kumbe sio na nimeanza kuwa na hisia kwamba Obama ni kibaraka wa The Board" nikaongea kwa sauti ya chini, tulikuwa tumeshatokea yard namba mbili.
"Unataka kunambia kuwa documents zangu zitakuwa mikononi mwa The Board muda huu?? Are you kidding me??" Kaburu akahamaki.
Godi alitusogelea mahali tulikokuwa baada ya kuingia yard namba mbili. Kwahiyo sasa tulikuwa tumesimama watu watatu pamoja.
"Inabidj tutekeleza plan yetu kwa haraka kuliko nilivyokuwa nimepanga" nikaongea huku nawaangalia wote wawili.
"Nakusikiliza" kaburu akaongea kwa hasira.
"Kukutorosha kutoka humu ni ngumu, inabidi nikutoroshe ukiwa nje"
"What? Sikuelewi" Kaburu akauliza.
"Hii Zahanati ya magereza nimegundua kuwa hailazi watu na haitibii ishu serious.. Kama mgonjwa anaumwa serious na anahitaji kulazwa au uangalizi wa karibu zaidi wa daktari anapelekwa hospitali kubwa chini ya ulinzi wa askari magereza" nikanyamaza kidogo kuwaangalia kama wananielewa, kisha nikaendelea. "Nahitaji keshi upelekwe hospitali kubwa ili nikutoroshe" nikaongea kwa sauti ya chini.
"What the *** are you talking about?? Mimi ni mfungwa, siwezi kuwaambia tu wanipeleke hospitaki kubwa" Kaburu akafoka.
"Hawatakupeleka tu na wala hautawaomba wakupeleke.. Watakupeleka wenyewe"
"Una maana gani?"
"Tunadaiwa shilingi elfu kumi na Nyapara na hatujamlipa mpaka sasa na tulitakiwa kumlipa jana.. Sasa muda wowote najua atakuja na wapambe wake kumdai Godi hela.. So akija nataka uwe shujaa umtetee Godi... Na nina hakika baada ya hapo lazima upelekwe kulazwa" nikaongea nikitabasamu lakini nikimaanisha ninachoongea.
"Dogo umedata nini? Unataka waniue au??" Kaburu akaanza kufoka kwa hasira.
"Mkuu kama una wazo zuri zaidi naomba kulisikia! Na kama huna Fanya ninachokwambia.. Nahitaji kesho uwe hospitali kubwa" nikaongea huku nikimvimbia na mimi.
"Mahakamaaaaaaaaaaaaaaa" mfungwa wa matangazo alipita yard anapayuka akitangaza kuwa muda umewadia kwaa mahabusu wenye kesi zao leo kwenda mahakamani.
"Wakuu naona tunaitwa huko! So mimi nawaacheni" nikaongea huku nawatazama.
"Usinisahau katika ufalme wako mkuu" Godi akakumbushia suala lake la dhamana.
"Usijali Godi, kitaeleweka tu" nikamjibu kisha nikamgeukia Kaburu na kuongea naye kwa sauti ya chini lakini ya ukali huku namsonta kidole kifuani "Nahitaji kesho uwe hospitali.! Don't forget that"
Nikaongea na kuanza kugeuka kuondoka.
"Kilala heri chief" Godi akaniaga huku anapiga saluti.
Kwa mara ya kwanza tangu aanzishe hizi swaga za kupigiana saluti, nikajikuta na mimi nimemjibu kwa kumpigia saluti fupi kwa kama nusu sekunde tu.
"I got this"
Nikageuka na kuondoka.
*************************
Kikichokuwa kinaendelea leo mahakamani niliona kama maigizo tu na ngonjera.
Ilipofika zamu yangu ya kesi kusikilizwa, nikapelekwa mpaka chamber court. Kisha wakaanza "maigizo" yao.
Mwendesha mashitaka akasimama na kuanza kuongea. Akataja nambabyangu ya kesi, shitaka linalonikabili, blah blah blah… Mwisho akaeleza kuwa Jamuhuri haina nia tena ya kuendelea na shauri hili.
Baada ya hapo Mheshimiwa hakimu naye akaanza blah blah blah.. Akataja lundo la vifungu vya Sheria… Sijui nini nini.! Alafu mwishoni akamalizia "…..hivyo basi mahakama hii inalifuta shtaka hilo na inakuachia huru kuanzia sasa"
Sikusema chochote, nikaweka mkono kifuani na kuinama kidogo kama ilivyo desturi kuonyesha heshima kwa mahakama kisha nikageuka na kutoka nje ya Ofisi ya Hakimu.
Koridoni, kulikuwa na cheupe na Issack pekee. Baba bite na wenzake hawakuwepo kama ilivyokuwa siku ya kwanza.
.
Nikamtazama Cheupe wangu kwa shauku kubwa. Damn, sijawahi kutamani kumkumbatia kiasi hiki. Nilitamani nimkumbatie kwa nguvu nisimuachie kwa hata wiki nzima.
Lakini huu haukuwa muda wala eneo sahihi kufanya hivyo.
Nikamshika mkono Cheupe na kuanza wakaongoza nje kwa haraka.
"Its a trap" nikaongea tukiwa tunatoka nje ya jengo lenye ofisi za mahakimu.
"What do you mean its a trap??" Cheupe akauliza kwa shauku.
Sikumjibu chochote. Nikawaongoza mpaka sehemu ndani mule mule kwenye viunga vya mahakama kulikuwa kama uchochoro unaotenganisha open court na jengo lenye ofisi za mahakimu.
Tulipofika hapo nikaangalia huku na huku, na nilipohakikisha tuko peke yetu nikaanza tena maongezi.
"Its a trap" nikarudia tena.
"What trap Ray" Issack akaukiza pia.
"Dr. Shirima juzi alinieleza kuwa nitaachiwa na nikiachiwa anataka niende moja kwa moja kwenye makazi ya askofu.. So obviously siwezi kufanya hivyo! So naamini kuna mtu amewekwa hapa atufuatile tukitoka hapa tunaenda wapi! Hawawezi kuniteka hapa mbele ya mahakama na polisi lakini nikikanyaga nje tu ya jengo la mahakama nina hakika lazima waninyakue kama kifaranga"
Nikawaelezea huku wote wametoa macho.
"So tunafanyaje?" Cheupe akauliza.
"Umekuja na simu yangu?" Nikamuuliza Cheupe.
Akaingiza mkono kwenge mkoba wake na kutoa simu na kunikabidhi.
Nikawasha na kuanza kutafuta namba niliyokuwa naitaka. Nikapekua pekua mpaka nilipoipata namba iliyoandikwa 'Taxi Bonge'.
Baada ya kuipata nikapiga.
"Niaje mzee wa saundi hahahah? Uko wapi….. Ok ok njoo mahakamani hapa mahakamani ila njoo na taxi nyingine mbili…. Yeah ingieni ndani…… aaaaahh wewe mzee wa saundi bhana utajua somjo utakayowapiga getini wakuruhusu kuingia……. Poa poa kaka" nikakata simu.
"Umeagizia taxi tatu??" Cheupe akashangaa.
"Yeah! Nataka tumvuruge akili huyo waliyemuweka atufuatulie"
Dakika tano baadae Taxi tatu zikaingia zikiwa zimeongozana. Nikampigia simu Bonge tena kumuelekeza waje na Taxi mpaka kwenye upenyo unaotenganisha jengo la ofisi za mahakimu na open court.
Taxi zote tatu zikaja. Nikamuomba karatasi na peni cheupe nikaandika kitu fulani kisha nikamoa dereva taxi mmoja.
"Ok, hiyo karatasi nataka upeleke Njia Panda ya Kilakala kwenye makazi ya Askofu wa Jimbo, ikabidhi kwa mlinzi getini muambie amfikishie Askofu… Issack utapanda hii taxi nyingine na uelekee nyumbani mazimbu… Mimi na Hasnat tutapanda taxi ya Bonge..!! Ila nataka taxi zote zitoke pamoja na tukiyoka getini tu kila mtu apite njia yake.. "
Wote wakaniangalia tu kwa mshangao wasielewe kinachoendelea.
"Don't worry Issac you going to be fine! Its me who they want!" Nikamfariji huku nikitumia kingereza ili wale madereva taxi wasielewe kinachoendelea.
Wote tukapanda kwenye magari kama nilivyowaelekeza kisha tukaondoka.
Nje ya geti taxi aliyopanda Issac ikapinda kushoto kufuata njia inayoelekea Central Police, taxi ile amabayo haina mtu pamoja na hii niliyopanda mimi na cheupe tukapinda kulia mpaka kwenye round about ya mnara wa mashujaa kisha ile taxi tupu ikapinda kulia kuelekea kilakala huku taxi niliyopanda mimi nikimuelekeza bonge anyooshe kama tunaelekea jengo la Manispaa.
Akanyoosha moja kwa moja mpaka tukatokea round about ya masika.
"Tunaelekea wapi mkuu" Bonge akauliza.
"Mikese" nikamjibu kwa ufupi tu.
Mimi na cheupe tulikuwa siti za nyuma.
"Whats your plan honey" Cheupe akaniuliza.
"My plan is very simple! Misdirect. Confuse. Deflect" nikamjibu huku namuangalia nikitabasamu.
Cheupe naye akatabasamu, kisha akainuka na kunikalia juu akalala kifuani. Nikampakata kama katoto kadogo huku nimekumbatia kwa nguvu kwa jinsi nilivyommsiss.
Kama dakika ishirini na tano baadae tulikuwa tumefika mikese.
Cheupe akamlipa elfu arobaini, tukashuka.
Baada ya Bonge kuondoka, tukavuka bara bara mpaka karibu na mizani. Tukaisimamisha gari ya aboud kisha tukapanda kurudi mjini.
Uzuri wa gari za Avoid unaweza kushukia stendi msamvu au unaweza kwenda kushukia mjini ambapo gari za Aboud lazima ziende ofisini kwao zikitoka safari.
Kwahiyo hatukushuka msamvu. Tukaenda na gari mpaka mjini na kushukia kwenye ofisi za Aboud zilizopo kati kati ya mji.
Hapo tukachukua bajaji mpaka stendi ya Hiace. Tulipofika stendi tukachukua dala dala inayoelekea nje ya mji maeneo ya Mkundi (Dodoma Road).
Mkundi tukashuka na kupiga mkono hiace zinazoelekea Dakawa. Tukapanda hiace mpaka dakawa.
Tulipofika, tukapumzika kidogo kwenye bar ilitopo pembeni ya bara bara. Nikaangalia kuona kama kuna dalili yoyote ya watu wa kutia shaka. Nilipojiridhisha kuwa tuko salama hakuna anayetufuatilia nikamwmbia Cheupe tuelekee bara barani.
"Are we running away from them??" Cheupe akauliza.
"Hell no! Najaribu kukata tail waliyotuwekea pale mahakamani na naamini tumefanikiwa.. Now its a time to put a tail on them" nikatabasamu na kumbusu kidogo cheupe wangu.
Tukafika barabarani, nikapiga mkono Lori ambalo naamini lilikuwa linaenda nje ya nchi. Naamini lilikuwa linaenda Rwanda. Lori likasimama.
"Mnaenda wapi" Dereva akauliza kwa sauti.
"Dodoma" nikamjibu.
"Aaaaahh mi nachukua abiria wa mbali bhana"
Kabla hajageuka nikatoa noti Tatu za elfu kumi na kumuonyesha.
"Elfu thekathini hii, unatuacha dodoma tu hapo"
Dereva akatabasamu kwa uroho. "Pandeni" akaongea huku anatufungulia mlango.
"So how are you going to put a tail on them?" Cheupe akauliza tukiwa tunapanda kwenye Lori.
"Usijali mama! Utaona" nikamjibu kwa kifupi.
Itaendelea Jumatatu..