Vipaji maalum si lolote, si chochote

Vipaji maalum si lolote, si chochote

VETA ilikuja baadaye sana...kabla ya veta ndo zilikuwepo hizi shule...zilikuwa zinatoa wanafunzi wazuri sana ila selikali ilikuwa inashindwa kuwaendeleza....kama ingekuwa inaendelea nao mpaka mwisho hakika wangekuwa wanafunzi wenye ubunifu wa hali ya juu...ila tatizo ni hilo selikali nyingi za kiafrika hazijali sana mambo ya creation and inovation

Sidhani kama VETA wana 'CREATE!!unachanganya kati ya KIPAJI na TRAINED PERSON
 
Tanzania ina Shule sita zinazojulikana kama Vipaji Maalum. Zipo nne za wavulana na mbili za wasichana. Shule hizo ni Mzumbe,Tabora Boys,Ilboru,na Kibaha(kwa wavulana). Kwa wasichana ni Kilakala na Msalato.

Katika matokeo ya Kidato cha Nne ya 2012 yaliyotangazwa leo,Shule hizo za vipaji maalum zimeboronga. Hakuna hata moja iliyo kwenye kumi bora. Zimeshindwa kujidhihirishia utofauti wao. Vipaji maalum sasa hakuna lolote,hakuna chochote.

Nafasi zao ni kama ifuatavyo: Mzumbe(17),Kibaha(18),Ilboru(31),Tabora Boys(44),Msalato(59) na Kilakala(63).

NOTE: Shule mpya ya Marian Boys ambayo ndio kwanza imeanza kutoa wahitimu wa kidato cha nne imeshika nafasi ya pili kitaifa. Hii ni Shule pacha ya Marian Girls (zote ziko Bagamoyo).Marian Girls imekamata nafasi ya nne nyuma ya Feza Boys(3) na vinara St. Francis Girls ya Mbeya.

Kwaheri vipaji maalum!

wewe umesomea shule gani?
 
Nadhani kinachochangia kwa vijana hawa tunaowaita vipaji maalum kutofanya vema hususani katka mitihani ya kuhitimu kidato cha nne, ni aina ya wanafunzi wenyewe wanaochaguliwa. Kumekuwa na uzembe ama kwa wanafunzi wenyewe kuzembea ama walimu wa shule husika kutoweza kutimiza wajibu wao.

Nimebahatika kusoma katika shule ya kibaha kwa elimu yangu ya kidato cha tano na cha sita, nikitokea shule binafsi ya secondary. Kimfumo wa ufundishaji na jinsi walimu wanavyojihusisha na wanafunzi katika shule hizi ni tofauti sana. Mathali, nilipo kuwa shule hiyo binafsi mifumo iliyowekwa ilikuwa hampi mwanya wa uhuru uliopitiliza kwa mwanafunzi hususani kwenye kujipangia maswala ya kusoma ama shughuli zingine za shule. Sheria zilikuwa wazi na ilikuwa vigumu kwa mwanfunzi kukaidi kwani adhabu iliyo ndogo kabisa ni kusimamwishwa masomo kwa muda wa siku tatu, na kwa kosa kubwa ilikuwa kufukuzwa shule ila fimbo ama viboko havikutumika kabisa.

Kitu nilichokiona kwa shule kama ya kibaha, ni kwamba ule uhuru walionao wanafunzi wa kujiamulia kuingia darasani muda anaojisikia haijalishi kwamba kuna mwalimu darasni ama la, mwanafunzi kutojishughulisha vya kutosha na shughuli za shule na pia wanafunzi walikuwa huru kutoka katika mipaka ya shule kuanzia mida ya jioni kwende kwenye vijiji vya jirani kama Mwanalugali imechangia sana huku walimu wakiwa wanatoa adhabu dhaifu mno kwa wanafunzi kulingana na kosa husika.

Ukilinganisha aina hii ya uhuru unaopatikana katika shule hizi, na aina ya wanafunzi wanaopelekwa pale ni lazima na tena kwa urahisi mno mwanafunzi kutoka katika misingi imara ya kujisomea na kuweka taritibu njema za masomo binafsi na zile za shule. Wanafunzi wengi wanaoharibika ni hali hii ni wale wadogo wa kidato cha kwanza na hukua na tabia hii mpaka wakifika kidato cha nne hali yao kitaaluma inakuwa dhaifu mno na wengi kutofanya vema.

Sipingani na ukweli kwamba ukipaji wao huwa unaonekana sana mbali na kuwa na alama za juu za ufaulu walipotoka, bali pia wanafunzi hawa wanasoma sama, sana na kupitiliza kwa kutegemea "notes" zao binafsi ama walizo pata "tution" na hudharau walimu wao kwa kiasi na wengine kutoingia darasani.

Nimejikita kwa wanafunzi hawa wa "O'level" kwa sababu ni wahanga wakubwa sana, na huwa wanafeli na kushindwa hata kufikia wastani mzuri na wengi hushusha jina la shule kwenye mafanikio ya kitaaluma.

Kwa upande mwingine, wanafunzi wa "A'level" wao hatuna shaka nao sana maana huwa wanaelewa nini kimewapeleka shule hata ufanisi wao katika kusoma huonekana kwa matokeo mazuri ya mitihani ya taifa. Mimi binafsi nilibahatika kusoma na wanfunzi walio bora zaidi katika wakati wetu wa mwaka ule na kwa ushirikiano tuliweza kufanya shule kushika nafsi ya NNE kitaifa, na Ya PILI kimkoa nyuma ya Marian Girls.

Ingekuwa vema kama shule hizi za "vipaji maalumu" zingetengeneza mazimngira bora zaidi kwa wanafunzi hao wa kidato cha kwanza mpaka cha nne. Pengine labda hali inaweza kubadilika na kuwa bora zaid.
 
kipaji maalum by books...syo mpango.utasikiaaa oh mwanafunzi hyu ndye kaongoza nchI nzima...mwisho wa siku ana sahaulika hana mpango tena ana rudi tu srreet...mmm siamini kbsa khusu kipaji maalum...kwanza hata kutengeneza vizibo vua soda hawajui vipaji malum my ass
 
Wakuu hizi Shule zinajulikana kama Special Schools; Ni special sababu wanaokwenda kule kwa Form One (ni wale waliofanya vizuri kuliko wenzao darasa la saba) na Form V (ni kwa wale waliofanya vizuri kuliko wenzao Form IV)..

Hicho ndio kipimo mitihani ya darasa la saba au form IV; Sasa maswali ya kama wameshinda Nobel Prize na mimi nikuulize ni watanzania wangapi wameshinda Nobel Prize ?, na kuhusu uvumbuzi wa mambo hicho sio kipimo hapa kipimo ni mitahani ambayo in short hawa jamaa walifanya vizuri kuliko wenzao. Ukitaka vipaji hata kina Diamond au wachoraji na wachonga vinyago hawa wanavipaji ingawa hizo tasnia hazifundishwi kwenye hizo shule.

Sasa kuboronga kwao after four or two years haimaanisha kwamba two or four years ago they performed brilliant. Kumbuka maisha sio sprint ni marathon (Its not a Battle its a War) na kushindwa kwao maisha haimaanishi kwamba walikuwa vipanga darasa la saba au form four. Every game has its rule Hizo shule haimaanishi kuna watu wenye akili kuliko wengine Tanzania nzima, bali inamaanisha kuna watu walio-perform brilliant than their counterparts. Lakini lack of teachers au kubweteka on their part inaweza kusababisha wakashindwa maisha mbeleni
mkuu umeeleza kwa kirefu, alaf nakubaliana na wew kabisa. Siku hizi shule binafsi hasa hizi saint marian na wenzie, wanafaulu sana kuzid special school, kutokana na mfumo wa ufundishaji wao, mazingira mazuri, na mchujo wnaofanya kabla ya kufikia form4. na sio kwamba wana uwezo mkubwa kuliko hizo special school.

mie naamin hivo kwa sababu, hao wenye div one kutoka saints wakiletwa kwenye mazingira sawa na hawa wenye div 2 kutoka kayumba mpaka utawahurumia yaan, hawana lolote.

nakumbuka pale CASS UDSM miaka 3 iliyopita, tulisoma na watu wenye one za 4 kutoka hizo shule, full ku-fail hawana uwez kabisa wa kujenga hoja. hata waioenda eng full majanga wengine mpaka kudisco. ingawa sio wote lakin wengi wao wanapata shida sana wakija kwenye shule za kawaida.
 
Tanzania ina Shule sita zinazojulikana kama Vipaji Maalum. Zipo nne za wavulana na mbili za wasichana. Shule hizo ni Mzumbe,Tabora Boys,Ilboru,na Kibaha(kwa wavulana). Kwa wasichana ni Kilakala na Msalato.

Katika matokeo ya Kidato cha Nne ya 2012 yaliyotangazwa leo,Shule hizo za vipaji maalum zimeboronga. Hakuna hata moja iliyo kwenye kumi bora. Zimeshindwa kujidhihirishia utofauti wao. Vipaji maalum sasa hakuna lolote,hakuna chochote.

Nafasi zao ni kama ifuatavyo: Mzumbe(17),Kibaha(18),Ilboru(31),Tabora Boys(44),Msalato(59) na Kilakala(63).

NOTE: Shule mpya ya Marian Boys ambayo ndio kwanza imeanza kutoa wahitimu wa kidato cha nne imeshika nafasi ya pili kitaifa. Hii ni Shule pacha ya Marian Girls (zote ziko Bagamoyo).Marian Girls imekamata nafasi ya nne nyuma ya Feza Boys(3) na vinara St. Francis Girls ya Mbeya.

Kwaheri vipaji maalum!

binafsi yangu naamini lengo lilikuwa zuri tu kwa wakati ule Enzi za mwalimu,ambapo shule zilikuwa chache na wakati huo taaluma ya ualimu ilikuwa hot cake,kwa maana waalimu walikuwa wachache na ilikuwa taaluma inayoheshimika,hivyo mwanafunzi hadi kufikia ufaulu wa kuchaguliwa secondary ilikuwa apigane kweli kweli,waliofaulu kwa kiwango cha juu zaidi walitunukiwa nafasi ya secondary kwenye shule zilizokuwa na waalimu wenye taaluma za juu katika ufundishaji,maabara nzuri za sayansi kwa wakati huo,pamoja na viffa vizuri vya ufundishaji,hivyo matunda yake ya baadaye pia yalikuwa mazuri,zilichukuliwa kama shule za hazina ya taifa kwa maana zilitoa waalimu wazuri,madaktari,viongozi wa juu wa serikali na kadhalika.lakini kutokana na kutofanyiwa maboresho kwa miongo kadhaa na kutokana na ongezeko la shule binafsi zenye kutoa huduma nzuri kwa waalimu na wanafunzi wake,ndio maana lengo la shule hizo za vipaji maalum limepitwa kwa mbali sana kutokana na waalimu wenye sifa nzuri kukimbilia kwenye mashule binafsi,wanafunzi wenye uwezo mkubwa kimasomo kutokwenda kwenye shule walizochaguliwa kwenda kwenye shule binafsi.hivyo tusiwalaumu wanafunzi wa vipaji maalumu bali ilaumiwe serikali kwa kuzitelekeza shule zake,binafsi yangu nimesoma kibaha secondary,nakumbuka mwaka wetu tulishika nafasi ya 8 kitaifa kwa maana ya kwanza kwa shule za serikali,lakini mazoezi mengi ya practical tulikuwa tukifanya mitaani,maabara zilikuwa hazina baadhi ya kemikali na vifaa.kwa upande wangu naona wamejitahidi
 
sawa mkuu ila jua kuwa shule za umma zilishapotea kitambo, kipaji maalum na kawa the same lever ndo big result now
 
Tanzania ina Shule sita zinazojulikana kama Vipaji Maalum. Zipo nne za wavulana na mbili za wasichana. Shule hizo ni Mzumbe,Tabora Boys,Ilboru,na Kibaha(kwa wavulana). Kwa wasichana ni Kilakala na Msalato.

Katika matokeo ya Kidato cha Nne ya 2012 yaliyotangazwa leo,Shule hizo za vipaji maalum zimeboronga. Hakuna hata moja iliyo kwenye kumi bora. Zimeshindwa kujidhihirishia utofauti wao. Vipaji maalum sasa hakuna lolote,hakuna chochote.

Nafasi zao ni kama ifuatavyo: Mzumbe(17),Kibaha(18),Ilboru(31),Tabora Boys(44),Msalato(59) na Kilakala(63).

NOTE: Shule mpya ya Marian Boys ambayo ndio kwanza imeanza kutoa wahitimu wa kidato cha nne imeshika nafasi ya pili kitaifa. Hii ni Shule pacha ya Marian Girls (zote ziko Bagamoyo).Marian Girls imekamata nafasi ya nne nyuma ya Feza Boys(3) na vinara St. Francis Girls ya Mbeya.

Kwaheri vipaji maalum!

Ni ngumu sana shule ambayo mzazi analipa ada milioni 2 iwe sawa na wanaolipa ada 70,000
 
Mambo yanaendelea.Vipaji Maalum hoi kweli kweli Matokeo ya Kidato cha Sita
 
Shule za vipaji maalumu zitabaki kuwa hivyo lazima tuukubali ukweli huu hata kama wengine tunamachungu ya kutopata nafasi katika shule hizo.kuweka kumbukumbu vizuri kwa wavulana shule hizi ni Kibaha,Iliboru.Mzumbe na Tabora wavulana.

Kulinganisha shule hizi na feza boys,kisimiri,igawele na shule hizi ni kulinganuisha jua na nyota.
1.Toka mkoloni shule hizi zimedhihirisha ubora wake mpaka leo.
2.Idadi ya wanafunzi wanaotahiniwa katika shule hizi ni kubwa sana ukilinginisha na shule nilizozitaja hapo juu zenye watahiniwa wachache mfano Feza ilikuwa na watahiniwa 60 pekee.daraja la 1-36,daraja la pili 18,daraja la tatu 6,hakuna four wala ziro.igowole ambayo ni ya kwanza ina watahiniwa 30tu,Kisimiri watahiniwa 52 tu.daraja la 1 -34,la pili 10,la tatu 8.

3.Shule nyingi hizi ndogondogo hutegemea sana udanganyifu kwenye mitihani ndiyo maana inaweza chomoza mwaka huu ikapotea kabisa isionekane tena wakati hizi za vipaji watu hutunisha misuli hasa kombi zenyewe nyingi ni za sayansi mfano pcb Hebu tuzipe

kwa mamtiki hiyo shule za vipaji maalumu zimezihirisha uwezo wao angalia matokeo yake na idadi ya watahiniwa.

1.Kibaha watahaniwa 161,daraja la kwanza 82,la pili 59,la tatu 18,la nne 2 hakuna 0.
2.Mzumbe watahiniwa 125,daraja la kwanza 56,la pili 38,la tatu 29,la nne 2 hakuna 0.
3.Iliboru watahiniwa 150,daraja la kwanza 53,la pili 50,la tatu 44,la nne 3 hakuna 0.
4.Tabora wavulana watahiniwa 158,daraja la kwanza 49,la pili 62,la tatu 45,la nne 2 hakuna 0.

Huwezi kuzinganisha na shule za watahiniwa wachache,hebu linganisha na shule zingine za wanafunzi wengi kama Tambaza,Pugu,Milambo ndo utajua kweli hizi shule ni majembe.

hazina daraja 0,daraja la nne ni 7 tu

hongereni madogo kwa kudhihirisha uwezo wenu njia nyeupe vyuo vikuu.

UKIONA NYANI MZEE JUA KAKWEPA MISHALE MINGI.
 
Umefunga kabisa mijadala ya aina hii Mkuu!!
 
ACCORDIND TO WIKIPEDIA
Talent means the skill that someone has quite naturally to do something that is hard. Someone who has talent is able to do something without trying hard. It is an ability that someone is born with. It is a high degree of ability or of aptitudes. People may have talent for music, dancing, acting, sport or other skills. Someone who has talent is talented:
Mozart had a talent for music. He had a great talent. He was very talented.
We say that someone is “born with a talent”.
If someone has talent they still have to work very hard if they want to be very good at something. Some people become quite good at something even if they do not have much talent, but if they are willing to work very hard at the skill. Some people “waste their talent” (they have talent but do not work hard at it, they do not “use their talent”).
Other words for talent are aptitude or gift.

MYTAKE:
Shule nyingi za vipaji siku hizi watoto wapelekwao wana uwezo mdogo kitalent kupitiliza.
Either waliiba mitihani ya la saba(waliiba kupitiliza,kwa mfano badala ya kuiba waende kata,wanaiba mpaka kuchaguliwa special) au walitafutiwa/waliunganishiwa kwa watu wizarani na kuchaguliwa special.
 
Back
Top Bottom