VIP wekeza kihalali kuanzia 10,000

VIP wekeza kihalali kuanzia 10,000

Maneno mazito kutoka kwa mwekezaji wetu aliewekeza mradi wa excavator.

Wakati nataka kufanya jambo hili nafsi yangu ilipata wepesi mno haikuwa na chembe ya shaka licho ya kuwa hatufahamiani, mwanzo nilikusudia kufanya kitu kingine ila nafsi ikawa inanisukuma kuwekeza huku, nimemuomba Mwenyezi Mungu sana kabla sijafanya hivyo. Allah atufanyie wepesi na atukidhie malengo yetu inshaallah. Je imefika lakini? nimepodeposit 10000000Tzsh kwenda account number XXXXXX BARCLAYS jina Ghafur Abdallah. Mohamed kupitia NMB XXXXXX.
 
Hawa Vitendo wako vizuri sana,nimewahi kuwatembelea,na ninawakubali sana,sijui kwa nini mpaka leo sijajiunga,toka niwatembelee sijatulia kwa kazi,zilivyonizunguka,lakini tuombe uhai na uzima,itabidi niwatembelee tena na kujiunga,wako vizuri sana.

Our name is our motto.

Huku VTS ni action tu.
 
Kuwa janja janja, vunja kibubu wekeza VIP...

Jinsi VIP inavyolipa kihalali...

500,000 (mtaji) X .5 (50%) = 250,000 (faida)...
500,000 mtaji + 250,000 faida = 750,000...
750,000 / 26 ( wiki za kazi) = 28,846 kwa wiki...
Utachagua zilipwe kila wiki 28,876 au kila mwezi 750,000 / 6 = 125,000
*Malipo ya faida yatakatwa sales commission ya 3% kutunisha mfuko wa SACCOS.
 
Wadau...

Mambo yanapamba moto ndani ya VTS. Unangoja nini kuwa VIP?
 
Karibu sana kwenye mkutano wetu wa kuchagua viongozi. Vitendo SACCOS Inawaalika Wapenda Maendeleo Wote

Update...

Wadau,

Kwanza tunashukuru AlhamduliLlah mkutano umeenda vizuri na umeisha salama.
Tunafuraha kuwafahamisha wadau wote kuwa mkutano umeenda vizuri kabisa na umefana sana.

Tulianza kwa kukaribishwa na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vitendo...

Kisha nikaongea kidogo mimi kuwakaribisha wajumbe wote...

Baada ya hapo ikaanza semina ya ushirika iliotolewa na Afisa Ushirika wa wilaya ya Kibaha, Bwana Msangi. Semina ilikuwa ndefu kidogo lakini ilitoa mwangaza mpana wa nini SACCOS, vipi iongozwe, nini haki za Wana SACCOS na vipi haki zao zinalindwa na kusimamiwa na sheria rasmi za vyama vya ushirika na vipi serikali inasimamia vyama vya ushirika.

Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yaliojiri mtajionea mkanda wa video.

Baada ya semina ukaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa muda. Ulioendeshwa na kusimamiwa na Afisa Ushirika kama sheria zinavyotaka.

Hatimae tukapata kamati ya uongozi wa muda ya uanzilishi wa Vitendo SACCOS Ltd., kwa mujibu wa Sheria na chini ya usimamizi wa Afisa Ushirika wilaya ya Kibaha.

Kamati hio ya muda ikamteua Katibu wa kwanza wa muda wa Vitendo SACCOS Ltd., chini ya usimamizia wa Afisa Ushirika wilaya ya Kiabaha.


Mambo yote hayo yapo kwenye video na picha. Zitakapokuwa tayari, tutapandisha video YouTube na kwenye tovuti yetu (inayoanadaliwa kwa sasa) tutapandisha video na picha.

Tunakaribisha maswali.

Asanteni na karibuni kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. kwa faida ya wengi.

Abdul Ghafur
Mwenyekiti
Mobile / Whatsapp 0625249605
 
Wanachama na Wana hisa wa Vitendo SACCOS wanategemea kuzindua na kuanza kazi miradi yao mitatu mipya hivi karibuni.

Miradi hiyo mitatu yote iliyo nje ya Vitendo SACCOS lakini imebuniwa na Wana VTS na itaendeshwa kwa njia ya kuchangiana mitaji na kugawana faida kwa muda maalum.

Miradi inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ni, mradi wa ukumbi wa sinema na mikutano, unaoweza kukaa watu 100, unatambulika kama mradi wa Vitendo Cinema Hall. Huu ni mradi wa muda mfupi kwa waliowekeza. Inatarajiwa kuwa mara tu utakapoanza hivi karibuni, wote waliowekeza kwenye mradi huu kuanza kupata mafao yao na faida ndani ya miezi sita.

Mradi mwingi unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni unaojulikana kwa jina la Vitendo Bricks, mradi huu ni wa muda wa kati. Mradi huu utajumuisha utengenezaji wa matofali ya aina tofauti tofauti na pia kwa siku za mwanzoni unatarajiwa kuwa na bidhaa tofauti zinazotokana na mchanga, kokoto na simenti.

Mradi huo pia unatarajiwa kuwa na uwezo wa kutengeneza bidhaa zote za ujenzi zinazotokana na simenti, kokoto na michanga.

Mradi mwengine kuanza hivi karibuni ni mradi wa kijiko (excavator) ya kuchimba na kupakilia mchanga. Mradi huu upo kwenye matayarisho ya mwisho na unategemewa kuanza hivi karibuni. Huu ni mradi unaotarajiwa kuanza kulipa mafao ya wawekezaji na kukamilika ndani ya siku 365 za kazi.

Tunawakaribisha nyote kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. Kwa faida ya wengi.

Vitendo SACCOS imedhamiria kufanya mabadiliko ya uwekezaji Tanzania. Na sasa unaweza kuanza kuwekeza na VTS kwa kuanzia Shillingi 10,000 tu.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa simu au whatsapp namba 0625249605.

Ahsanteni sana.
 
Je mmesajiliwa ns mamlaka husika?
Usajili wa SACCOS ni mlolongo mrefu wa kutimiza masharti yaliyoainishwa na Sheria ya vyama vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013.

Kwanza unatakiwa uwe na wanachama watarajiwa zaidi ya 20 ambao watapiga kura za kuchagua uongozi wa muda. Kabla ya kuchaguliwa huo uongozi ni lazima Afisa Ushirika awape semina elekezi ya uundwaji wa chama cha ushirika.

Tunashukuru stage hiyo tumemaliza tarehe 21/10/2017.

Baada ya stage hiyo inabidi sasa muwe na wanachama waliokwisha lipia kiingilio, kununua hisa na kuweka akiba. Tupo stage hii na tumekamilisha.

Kinachofatia ni Afisa Ushirika kuja kukagua na kujiridhisha kuwa tupo kweli zaidi ya wanachama 20 tuliotimiza masharti.

Licha ya masharti hayo ya uanachama, pia mnahitajika kuwa na mtaji usiopungua Shillingi million tano benki na ofisi za chama.

Mkitimiza yote hayo ndio mnasajiliwa rasmi.

Tunashukuru kuwa masharti hayo yote yapo ndani ya uwezo wetu na kinachosubiriwa ni semina elekezi ya pili kutoka kwa Afisa Ushirika ambayo itatuelekeza namna ya mfumo wa kuutumia kwa kuwa SACCOS yetu ni Bila Riba.

Baada ya hapo ni kukaguliwa na kusajiliwa. Kwani kama nilivyoeleza awali, masharti yote yapo ndani ya uwezo wetu na tupo kwenye harakati za usajili kisheria.

Karibu sana ujiunge nasi kwa faida ya wengi.
 
Unapata faida isiopungua 50% kwa miezi sita.

Ungeeleza hiyo faida inapatikana vipi, hiyo return ni kubwa sana kuwa sustainable. Mfano wakachanga watu zikafika milioni 500 utazalishaje faida ya mil 250 kwa miezi 6?? Isije kuwa ponzi scheme?...ambapo hiyo inYoitwa faida ni gawio kutoka makusanyo ya wachangiaji wapya.

Pyramid ikianza kuwa flat mfumo unakufa...yaani pale wanaoingia wapya wakiwa wachache kuliko waliopo. Mara nyingi ponzi scheme ambapo ni utapeli na illegal wanakwambia weka kiasi fulani upate kiasi fulani baada ya muda fulani, ambapo huwa ni kikubwa kuliko kawaida na hakuna mfumo wa uzalishaji bali ni zile zile fedha zinakuswanywa na kugawanywa kwa wachangiaji waliopo.

Mfano ni deci, d9 na nyinginezo zilizopigwa marafuku...na lugha zao huwa tamu kwa geresha fulani watakwambia tunabet au tumewekza kwenye hiki na kile lakini hawawezi kuthibitisha kihesabu. Kuwa mwangalifu. Ni mtazamo tu wa jicho tofauti, pengine siko sahihi.
 
Back
Top Bottom