Abdul Ghafur
JF-Expert Member
- Sep 18, 2017
- 610
- 749
- Thread starter
- #101
Ukifatilia kwa makini katika nyuzi zetu za miradi humu utaona kuwa miradi yetu yote na uwekezaji una limitation.Ungeeleza hiyo faida inapatikana vipi, hiyo return ni kubwa sana kuwa sustainable. Mfano wakachanga watu zikafika milioni 500 utazalishaje faida ya mil 250 kwa miezi 6?? Isije kuwa ponzi scheme?...ambapo hiyo inYoitwa faida ni gawio kutoka makusanyo ya wachangiaji wapya.
Pyramid ikianza kuwa flat mfumo unakufa...yaani pale wanaoingia wapya wakiwa wachache kuliko waliopo. Mara nyingi ponzi scheme ambapo ni utapeli na illegal wanakwambia weka kiasi fulani upate kiasi fulani baada ya muda fulani, ambapo huwa ni kikubwa kuliko kawaida na hakuna mfumo wa uzalishaji bali ni zile zile fedha zinakuswanywa na kugawanywa kwa wachangiaji waliopo.
Mfano ni deci, d9 na nyinginezo zilizopigwa marafuku...na lugha zao huwa tamu kwa geresha fulani watakwambia tunabet au tumewekza kwenye hiki na kile lakini hawawezi kuthibitisha kihesabu. Kuwa mwangalifu. Ni mtazamo tu wa jicho tofauti, pengine siko sahihi.
Hatuchangishi zaidi ya kinachohitajika kwa mradi fulani.
Mfano tulikuwa na mradi wa mchanga tukachangisha million 30 tu. Tukafunga uwekezaji. Mradi wa excavator million 40 tukafunga uwekezaji.