Viongozi wa vyama vingi vya Ushirika wa zao la kahawa Wilayani Mbinga wanafanya kazi kwa lengo la kujinufaisha

Maguguma

Member
Mar 13, 2023
13
6
Viongozi wa vyama vingi vya Ushirika wa zao la kahawa Wilayani Mbinga wanafanya kazi kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe badala ya wakulima wa zao hilo.

Wakulima wa zao la Kahawa wanafanya kazi wakati wa mvua na jua kwa kipindi cha mwaka mzima, lakini kwa asilimia kubwa wanaonufaika ni viongozi wanaokaa Ofisini tu, bila kuvuja jasho.

Mkulima ananyunyiza dawa shambani,anaweka mbolea na anaondoa magugu. Wakati wa mavuno anachuma kahawa kwa mikono yake, anasafirisha zao lake hadi sehemu ya kuuzia kisha anapangiwa bei na watu wengine tena kibabe na mara nyingi toka anapoanza kuhudumia shamba lake mwezi wa kwanza anapata malipo yake baada ya miezi 13 hadi 15. Wakulima wanaambiwa na viongozi kwenye mkutano kuwa mwaka huu tutawalipa shilingi 450 (kwa kilo), bila kujali wamekubali au wamekataa.

Viongozi wa vyama vidogovidogo vya Ushirika, Chama Kikuu “MBIFACU” na Maafisa kilimo hawawasikilizi wakulima, wanafanya kazi chini ya mwavuli wa “ADUI WA HAKI” yaani Rushwa. Wakulima wengi wanateseka.

Habari nyingi zinazoandikwa kuhusu Vyama vya Ushirika Mbinga ni zile za kusifia tu, waandishi wengi wanawahoji watawala badala ya wakulima wenyewe. Wakulima hawana mtetezi wa kweli, watetezi wao wanakula meza moja na wala Rushwa, wakati wao wamekaa chini ya mti mkavu.

Kuuza mazao kupita Vyama vya ushirika sio kitu kibaya ila vyama hivyo vimegeuzwa kuwa Kaburi la wakulima na Viongozi wake. Vipo vyama vichache vyenye viongozi wazuri lakini vyama vingi havina nia njema na wakulima.

Miaka ya 1990 wazee wengi walipoteza Kahawa yao kupitia ushirika (MBICU), hawajalipwa hadi leo. Suala hilo lilienda hadi Bungeni, huku wakulima wa kipindi hicho wakiwa na matumaini makubwa ya kupata haki zao, lakini mwisho wa siku giza likatawala.
images (2).jpeg
 
Mwamba umejiunga jf March 13 na tarehe 15 March umeshusha uzi wa wazee wa Kahawa.. karibu sana .. . Uzi toka 15 March hadi leo.. 0 comments inaonesha wakulima wa kahawa hawapo jf
 
Mwamba umejiunga jf March 13 na tarehe 15 March umeshusha uzi wa wazee wa Kahawa.. karibu sana .. . Uzi toka 15 March hadi leo.. 0 comments inaonesha wakulima wa kahawa hawapo jf
Mimi nimepata madaraka Leo, ngoja nikawashughulikie, nipo tayari waniloge
 
Back
Top Bottom