Serikali iingilie kati Mgogoro wa CWT dhidi ya Wanachama wake

Russia is not your enemy

JF-Expert Member
Feb 19, 2023
373
612
Ukimya sio Jibu, Serikali iingilie kati Mgogoro wa CWT dhidi ya Wanachama.

Ni miaka zaidi 20 Serikali na wanachama hawajatulia na CWT wanatoa majibu mepesi.

Nakumbuka CWT ilijinasibu kuwatekelezea walimu mahitaji yao ikaahidi mambo mengi sana kama benk yao, majimbo yao, nk.

Katika vikao mbalimbali wanachama wamekuwa wakidai haki yao bila majibu ya kueleweka.

Miaka mitatu hadi minne sasa viliibuka vyama kama CHAKUWAWATA, nk, tafsiri ya hii ni kwamba walimu wamechoshwa na hadaa ya CWT, kwamba serikali nayo imeziba masikio. 2% ya Makato ni kubwa mno, mishahara wenyewe haujitoshelezi.

Ikumbukwe katika ahadi ya CWT ni miradi ya kuwanifaisha wanachama badala yake CWT inaendelea kukusanya 2%, hii si sawa kabisa. Nimeshuhudia wazee wameanza na kustaafu bila manufaa ya moja kwa moja kutoka CWT. Imefikia wakati sasa kuachana na CWT au Serikali iingilie kati suala hili.

Wananchi walilalamika bila majibu.

Kuwa mwanachama wa chama Cha wafanyakazi siyo lazima. Wajitoe tu. Inabaki kulalamika makato Wakati unaweza kujitoa.

WAJIONDOE UANACHAMA.
 
Back
Top Bottom