Viongozi wa Dini na utawala wa Dr John Magufuli

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Viongozi wa dini zote wanalojukumu kubwa la kujenga mioyo ya wanachi kwa kutekeleza yale Mungu anayoyataka na kuya acha yale Mungu anayokataza. Hili linathibitika katika dini ya Kiislamu tunapo ambiwa katika Quar-an takatifu kuwa litoke kundi miongoni mwenu litakalowaamrisha watu mema na kuwakataza mambo mabaya (3:104).Vivyo hivo kwenye Bibilia …” tumepokea neema na agizo la kuwaongoza watu wa mataifa yote wasiomjua Mungu, wapate kumwamini na kumtii (Warumi 1:1-9:26).Hivyo utiii juu ya Mungu kwa kufanya mema na kuacha maovu ndio msingi mkubwa wa imani zote duniani.

Maovu duniani yanaongezeka na yamekuwa yakishangiliwa na kupewa chepuo kuliko mambo mema katika jamii.Mfano kijana kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kuoa limekua jambo la kawaida,ulevi,wizi,uzinzi,mavazi yasiyo na stara nakadhalika.Wimbi hili kubwa la kuongezeka maovu limeiweka dunia katika majanga mbalimbali yakiwemo maradhi,umaskini,ufisadi pamoja na kuondoka kwa amani katika jamii.

Mambo mengi ambayo Mungu anakataza yanahasara kubwa kuliko faida inayopatikana.Mfano uzinzi,dini zote zinakemea uzinzi kutokana na hasara zinazopatikana kwenye tendo hilo ambazo ni pamoja na magonjwa,ustawi wa jamii,kuzorota kwa uchumi nakadhalika.

Viongozi wa dini katika karne hii popote duniani wamekua na changamoto kubwa katika kuwaondoa waumini wao kutoka katika wimbi la maovu na kuwapeleka katika kumtii Mungu.

Katika awamu ya tano ya Raisi John Pombe Magufuli serikali yake imeweza kuwarahisishia Mapadri, Wachungaji, Mashekhe, Maimamu pamoja na viongozi wengine wa dini kazi zao za kuwaita waumini kumwabudu Mungu pamoja na kuondoa maovu katika jamii ya Watanzania.

Utawala wa awamu tano umepambana vikali na kutoa matokeo ambayo hayajawahi kupatikana katika historia ya Tanzania tangu na kabla ya kupata uhuru. Hii imepelekea viongozi wa dini zote kumuunga mkono kwa dhati Raisi John Pombe Magufuli kwa kutamka hadharani na katika madhabahu na mimbari zao.

Dua kutoka kwa Mashekhe na Maimamu zimekua zikifanyika mara kwa mara katika miskiti kumwombea Raisi John Pombe Magufuli afya nje ili aweze kutekeleza majukumu yake.Mashekhe wakubwa kama Shekh Mkuu Mufti Zubeir pamoja na Mashekhe wengine kama shekh Kishki wamekua wakimuombea kutokana na kazi yake kubwa ya kuondoa maovu ndani ya jamii ya Watanzania kwa kutekeleza kwa uadilifu kazi yake ya uongozi wa nchi.

Viongozi wa Makanisa na Mapadri nao wamekua msatari wa mbele katika kuhakikisha wanafanya maombi kwa Raisi ili aweze kuyatekeleza majukumu yake.Mchango huu wa viongozi wa dini kwa Raisi umekua ukimfariji na kuona vita aliyonayo dhidi ya machafu yaliyoidumbukiza nchi katika wimbi la umaskini inaungwa mkono na waumini wengi.

Ni ndani ya mwaka huu katika mashindano makubwa ya Kimataifa yaliyohusiha washiriki wan chi zote Africa ya Qur-an Mashekhe walitumia fursa hiyo kumwombwea Raisi John Pombe Magufuli.

Kwa uchache tuyaangalie mambo makubwa amabyo yamerahisisha kazi za viongozi wa dini na kuwafanya wawe na imani na serikali ya wamu ya tano chini ya Uongozi wa Raisi John Magufuli kama yafuatayo:-

1.Madawa ya Kulevya.
Janga la madawa ya kulevya kwa nchi ya Tanzania hasa maeneo ya mijini lilikua kubwa na la kuogopesha,madawa ya kulevya yaliuzwa wazi mchana kweupe na wale waliokuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu walijulikana na vyombo vya usalama.Watoto wengi wa Kitanzania waliangamia katika janga hili la madawa ya kulevya.
Baada ya Raisi Magufuli kuingia madarakani,vita ya kweli dhidi ya mtandao wa madawa ya kulevya ilipiganwa kwa dhati ambapo iliwagusa wafanyabiashara wakubwa na wakati.Hivi sasa biashara hiyo imekaribia kuisha kabisa na vijana wengi walioathirika wanapata matibabu.

2.Mapenzi ya jinsia moja
Dini zote zinakataza mapenzi ya jinsia moja,licha baadhi ya wanasiasa kuhamasisha utamaduni huu kwa manufaa yao binafsi,utawala wa Raisi John Pombe Magufuli umeweka wazi kuwa Tanzania ni nchi Takatifu kwa maana ushenzi huo haukubaliki na hatua za kisheria zitachukuliwa wale wote wanaofanya biashara hizo.

3.Ufisadi
Ufisadi ni chukizo mbele ya Mungu kwani unaleta maangamizi kwa jamii kwa kuikosesha mahitaji yake pamoja na kuangamiza makundi ya watu wengi.Ufisadi umepigwa vita katika awamu zote za uongozi,lakini awamu ya tano imeupiga vita na kutoa matokeo makubwa ambayo hayakuwahi kupatikana tangia kupatikana kwa Uhuru.

4.Rushwa
Rushwa huhubiriwa katika makanisa na misikitini ili waumini waondokane na hili janga ambalo linawakosesha wenye haki kupata haki zao.Awamu ya tano ya uongozi wa Raisi John Pombe Magufuli imepambana na Rushwa kiasi cha kushtusha jamii za kimataifa.Wanchi wanapata haki zao na hakuna dhulma inayofanyika kwa misingi ya rushwa.Wapo wanachi wachache ambao bado wanaendelea na uovu huu kwa njia ya siri kubwa.

Raisi Magufuli amaweka msisitizo kwenye masuala ambayo Mungu anayataka,mfano wa mambo ambayo ni kipaumbele cha Raisi Magufuli nikama yafuatayo:-

1.Elimu
Elimu ndani ya dini ya Kiislamu imepewa kipaumbele kikubwa kwa kufanywa aya ya kwanza kumshukia Mtume Mohamad.Mtume Muhamad aliambiwa soma kwa jina la Mola wako.

Raisi Magufuli amefanikisha kufanya elimu ya awali,elimu ya msingi mpaka sekondari kuwa bure kwa wanchi wote wa Tanzania.Raisi ameimarisha miundombinu ya masomo mashuleni kwa kuongeza madarasa,walimu pamoja na mahitaji mengine muhmu ya utoaji wa elimu.

2.Uwajibikaji
Watumishi wa umma wanawajibika kwa kutoa huduma kwa wananchi jambo ambalo ni la msingi kwa serikali yoyote ya wanachi.Urasimu serikalini umepungua kwa kiwango kikubwa na huduma kwa wanchi zinafika kwa wakati.

3.Miradi ya maendeleo
Serikali ya awamu ya Tano imekua ikitatua changamoto za kimaendeleo kwa wanchi kwa kuanzisha miradi ya kimaendeleo.Miradi mingi ya kimaendeleo imeanzishwa na wanachi wamekua wakiridhishwa na miradi hii.
Nimtakie Raisi wetu Afya Njema ili aweze kuendelea kuwatumikia wananchi
 
Viongozi wa dini zote wanalojukumu kubwa la kujenga mioyo ya wanachi kwa kutekeleza yale Mungu anayoyataka na kuya acha yale Mungu anayokataza. Hili linathibitika katika dini ya Kiislamu tunapo ambiwa katika Quar-an takatifu kuwa litoke kundi miongoni mwenu litakalowaamrisha watu mema na kuwakataza mambo mabaya (3:104).Vivyo hivo kwenye Bibilia …” tumepokea neema na agizo la kuwaongoza watu wa mataifa yote wasiomjua Mungu, wapate kumwamini na kumtii (Warumi 1:1-9:26).Hivyo utiii juu ya Mungu kwa kufanya mema na kuacha maovu ndio msingi mkubwa wa imani zote duniani.
Maovu duniani yanaongezeka na yamekuwa yakishangiliwa na kupewa chepuo kuliko mambo mema katika jamii.Mfano kijana kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kuoa limekua jambo la kawaida,ulevi,wizi,uzinzi,mavazi yasiyo na stara nakadhalika.Wimbi hili kubwa la kuongezeka maovu limeiweka dunia katika majanga mbalimbali yakiwemo maradhi,umaskini,ufisadi pamoja na kuondoka kwa amani katika jamii.
Mambo mengi ambayo Mungu anakataza yanahasara kubwa kuliko faida inayopatikana.Mfano uzinzi,dini zote zinakemea uzinzi kutokana na hasara zinazopatikana kwenye tendo hilo ambazo ni pamoja na magonjwa,ustawi wa jamii,kuzorota kwa uchumi nakadhalika.
Viongozi wa dini katika karne hii popote duniani wamekua na changamoto kubwa katika kuwaondoa waumini wao kutoka katika wimbi la maovu na kuwapeleka katika kumtii Mungu.
Katika awamu ya tano ya Raisi John Pombe Magufuli serikali yake imeweza kuwarahisishia Mapadri,Wachungaji,Mashekhe,Maimamu pamoja na viongozi wengine wa dini kazi zao za kuwaita waumini kumwabudu Mungu pamoja na kuondoa maovu katika jamii ya Watanzania.Uawala wa awamu tano umepambana vikali na kutoa matokeo ambayo hayajawahi kupatikana katika historia ya Tanzania tangu na kabla ya kupata uhuru.Hii imepelekea viongozi wa dini zote kumuunga mkono kwa dhati Raisi John Pombe Magufuli kwa kutamka hadharani na katika madhabahu na mimbari zao.
Dua kutoka kwa Mashekhe na Maimamu zimekua zikifanyika mara kwa mara katika miskiti kumwombea Raisi John Pombe Magufuli afya nje ili aweze kutekeleza majukumu yake.Mashekhe wakubwa kama Shekh Mkuu Mufti Zubeir pamoja na Mashekhe wengine kama shekh Kishki wamekua wakimuombea kutokana na kazi yake kubwa ya kuondoa maovu ndani ya jamii ya Watanzania kwa kutekeleza kwa uadilifu kazi yake ya uongozi wa nchi.
Viongozi wa Makanisa na Mapadri nao wamekua msatari wa mbele katika kuhakikisha wanafanya maombi kwa Raisi ili aweze kuyatekeleza majukumu yake.Mchango huu wa viongozi wa dini kwa Raisi umekua ukimfariji na kuona vita aliyonayo dhidi ya machafu yaliyoidumbukiza nchi katika wimbi la umaskini inaungwa mkono na waumini wengi.
Ni ndani ya mwaka huu katika mashindano makubwa ya Kimataifa yaliyohusiha washiriki wan chi zote Africa ya Qur-an Mashekhe walitumia fursa hiyo kumwombwea Raisi John Pombe Magufuli.
Kwa uchache tuyaangalie mambo makubwa amabyo yamerahisisha kazi za viongozi wa dini na kuwafanya wawe na imani na serikali ya wamu ya tano chini ya Uongozi wa Raisi John Magufuli kama yafuatayo:-
1.Madawa ya Kulevya.
Janga la madawa ya kulevya kwa nchi ya Tanzania hasa maeneo ya mijini lilikua kubwa na la kuogopesha,madawa ya kulevya yaliuzwa wazi mchana kweupe na wale waliokuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu walijulikana na vyombo vya usalama.Watoto wengi wa Kitanzania waliangamia katika janga hili la madawa ya kulevya.
Baada ya Raisi Magufuli kuingia madarakani,vita ya kweli dhidi ya mtandao wa madawa ya kulevya ilipiganwa kwa dhati ambapo iliwagusa wafanyabiashara wakubwa na wakati.Hivi sasa biashara hiyo imekaribia kuisha kabisa na vijana wengi walioathirika wanapata matibabu.
2.Mapenzi ya jinsia moja
Dini zote zinakataza mapenzi ya jinsia moja,licha baadhi ya wanasiasa kuhamasisha utamaduni huu kwa manufaa yao binafsi,utawala wa Raisi John Pombe Magufuli umeweka wazi kuwa Tanzania ni nchi Takatifu kwa maana ushenzi huo haukubaliki na hatua za kisheria zitachukuliwa wale wote wanaofanya biashara hizo.
3.Ufisadi
Ufisadi ni chukizo mbele ya Mungu kwani unaleta maangamizi kwa jamii kwa kuikosesha mahitaji yake pamoja na kuangamiza makundi ya watu wengi.Ufisadi umepigwa vita katika awamu zote za uongozi,lakini awamu ya tano imeupiga vita na kutoa matokeo makubwa ambayo hayakuwahi kupatikana tangia kupatikana kwa Uhuru.
4.Rushwa
Rushwa huhubiriwa katika makanisa na misikitini ili waumini waondokane na hili janga ambalo linawakosesha wenye haki kupata haki zao.Awamu ya tano ya uongozi wa Raisi John Pombe Magufuli imepambana na Rushwa kiasi cha kushtusha jamii za kimataifa.Wanchi wanapata haki zao na hakuna dhulma inayofanyika kwa misingi ya rushwa.Wapo wanachi wachache ambao bado wanaendelea na uovu huu kwa njia ya siri kubwa.

Raisi Magufuli amaweka msisitizo kwenye masuala ambayo Mungu anayataka,mfano wa mambo ambayo ni kipaumbele cha Raisi Magufuli nikama yafuatayo:-
1.Elimu
Elimu ndani ya dini ya Kiislamu imepewa kipaumbele kikubwa kwa kufanywa aya ya kwanza kumshukia Mtume Mohamad.Mtume Muhamad aliambiwa soma kwa jina la Mola wako.
Raisi Magufuli amefanikisha kufanya elimu ya awali,elimu ya msingi mpaka sekondari kuwa bure kwa wanchi wote wa Tanzania.Raisi ameimarisha miundombinu ya masomo mashuleni kwa kuongeza madarasa,walimu pamoja na mahitaji mengine muhmu ya utoaji wa elimu.
2.Uwajibikaji
Watumishi wa umma wanawajibika kwa kutoa huduma kwa wananchi jambo ambalo ni la msingi kwa serikali yoyote ya wanachi.Urasimu serikalini umepungua kwa kiwango kikubwa na huduma kwa wanchi zinafika kwa wakati.
3.Miradi ya maendeleo
Serikali ya awamu ya Tano imekua ikitatua changamoto za kimaendeleo kwa wanchi kwa kuanzisha miradi ya kimaendeleo.Miradi mingi ya kimaendeleo imeanzishwa na wanachi wamekua wakiridhishwa na miradi hii.
Nimtakie Raisi wetu Afya Njema ili aweze kuendelea kuwatumikia wananchi
NDIO SABABU WAUIMINI WANA TANGATANGA KWA VIONGOZI WAS KUKUSA MSIMAMO.
 
Wewe huna hoja nimeamua nikupuuze rasmi sasa
Bado hujafa na viongoz wako wa dini! Wewe ndiye wa kupuuza unayeunga mkono MAUAJI YA RAIA. Mimi sikupuuzi kwa vile wewe ni MUUAJI! Nyerere angelimpuuza Idd Amin, Kagera ingelikuwa sehemu ya Uganda.
 
Ni kiongozi wa dini mchumia tumbo tuu anaekubaliana na mwenendo wa sasa hivi. Kwani Inapotokea kiongozi wa dini tena hadharani anasifia kwa kusema Tanzania kuna viongozi bora ilhali kuna waumini wametekwa wamepigwa risasi hadharani na wengine kutojulikana walipo hadi leo.Viongozi wa aina hii wanajitoa ufahamu kwa ajili ya matumbo yao
 
Viongozi wa dini walitakiwa wabaki peke yao humo kwenye nyumba za ibada ili wakose sadaka watafungua mdomo wenyewe juu ya mambo yanayoendelea nchini.
 
3.Ufisadi
Ufisadi umepigwa vita katika awamu zote za uongozi,lakini awamu ya tano imeupiga vita na kutoa matokeo makubwa ambayo hayakuwahi kupatikana tangia kupatikana kwa Uhuru.
Duh! Kazi mnayo kweli ya kuua mende kwa nyundo.

1.Elimu
Raisi ameimarisha miundombinu ya masomo mashuleni kwa kuongeza madarasa,walimu pamoja na mahitaji mengine muhmu ya utoaji wa elimu.
Walimu gani aliowaongeza? Ivi umetembelea maeneo ya vijijini kuona hali ya miundombinu ya majengo na madarasa? Wanafunzi wote wana madawati?

3.Miradi ya maendeleo
Serikali ya awamu ya Tano imekua ikitatua changamoto za kimaendeleo kwa wanchi kwa kuanzisha miradi ya kimaendeleo.Miradi mingi ya kimaendeleo imeanzishwa na wanachi wamekua wakiridhishwa na miradi hii.
Nimtakie Raisi wetu Afya Njema ili aweze kuendelea kuwatumikia wananchi

Taja mfano wa miradi ya kimaendeleo iliyoanzishwa na Magufuli ambayo wanainchi wamekuwa wakiiridhia iliyo tofauti na awamu zingine za uraisi.
 
Back
Top Bottom