Hilo neno kutoka kwa makonda wala silioni kuwa lina tatizo.
Simply amemaanisha kuwa yupo na Mwenyeezi Mungu na anasimamia haki.
Nakubaliana na wewe Faiza 100%, hao maadui wa Makonda wanataka kupotosha maana halisi ya kile alichokuwa anaelezea. Makonda yuko pale kuwatetea wanyonge wanaooonewa na hawa wenyeviti wa mitaa na maafisa ardhi ili wapate haki kama MUNGU alivyoagiza . Wanaomkashifu Makonda ni hao ambao wanafaidika na uhalifu wanaofanya kwa mfano wenyeviti wa mitaa ambao kwa kushirikiana na wajumbe wao huficha uhalifu; mfano ni huku Mbezi Beach A ambako walikamatwa wauza madawa ya kulevya na watu wenye silaha za vita!! Inashangaza pale ofisi ya mwenyekiti wa mtaa inapotumika kuwanyanyasa wale wanaowataja wahalifu hawa kwenye mikutano ya hadhara!!! Makonda hakikisha unawalinda hawa raia wema hapo ndipo wananchi watawasaidia polisi kulinda usalama wa raia.