Viongozi wa dini mkanyeni Makonda!!

Viongozi wa dini mkanyeni Makonda!!

Watu na awamu hii kwani watu hawafanyi kazi? Kama unaona hawafanyi kazi piga kimya hii ni open forum by the way umenikumbusha baba paroko Mapunda miaka 2000 parokiani Nyakato Mwanza
 
Hilo neno kutoka kwa makonda wala silioni kuwa lina tatizo.

Simply amemaanisha kuwa yupo na Mwenyeezi Mungu na anasimamia haki.
Alivyolitamtaka na mfuatano wa maneno na matendo yake hakuhusiani na kutenda haki. Halafu kigezo kwamba anatenda haki inayotambuliwa na kukubaliwa na Mungu amekipata wapi?
 
Nawezaje kujibu swali la kiujumla? Mtu akikuuliza ile nguo yako imeivaa. utamjibuje?
Basi Allen. Tuishie hapo.Maana unajua nakuuliza nini.
Ila unakata kona hutaki kuzungumzia hilo. Basi tuishie hapo mkuu.
Siku njema.
 
Mtoa post mungu wa daslam anakuona.
1481525301870.jpg
 
Kunukuliwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akisema kuwa anapokuwa amesimama yeye basi anakuwa amesimama Mungu, kumeleta mfadhaiko miongoni mwa watu wenye akili timamu wanaojua nini inamaanishwa inaposemwa neno "Mungu". Lakini kauli hiyo pia imezifedhehesha dini zote zilizoko duniani.

Kila watu wakienda wanakoabudu wanaambiwa wanamuabudu "Mungu", halafu anasimama mtu na kusema akisimama yeye anakuwa amesimama Mungu, hili ni dharau kwa waabudu Mungu. Makonda anataka kusema yeye ni Mungu ama ni Mwakilishi wa Mungu?

Kama waislamu wanasema "hakuna apaswaye kuabudiwa ila ni Mungu pekee..." nao ndugu zao Wakristo wanasema "Mungu ni mwenye wivu.." inakuwaje wanakaa kimya mtu mwingine anapojifananisha na Mungu? Au viongozi wa dini nao wanaamini anaposimama Makonda anakuwa amesimama Mungu?

Ukimya wa viongozi wa dini juu ya kauli ya Makonda kuhusu Mungu unapalilia ile dhana kwamba viongozi wa dini Tanzania wana Shirika na viongozi wa Serikali wanaotokana na CCM. Maana kuna wakati watu waliuliza inakuwaje viongozi wa vyama vya upinzani huwa hawaalikwi kwenye yale matamasha ya "amani"? Kumbe inawezekana waandaji labda huwa wanaogopa kumuudhi Mungu kwa kuwaalika Mashetani.

Hata kama aliahidi kusaidia kujenga Makao Makuu ya BAKWATA ama alimtembelea Kadinali Pengo Ofisini kwake, ni lazima Makonda aonywe na akemewe hadharani kwa tendo lake la kujilinganisha na Mungu. Viongozi wa dini huo ukereketwa wenu wa CCM unawaondolea sifa ya kuwa viongozi wa dini kwani sifa mojawapo ya kuwa kiongozi wa dini ni kuzuia Mungu KUDHIHAKIWA!!
chuki.
 
Allen unazeeka vibaya.

Unayaacha ya Mbowe kumuuza sanane unakalia ya makonda
 
Alivyolitamtaka na mfuatano wa maneno na matendo yake hakuhusiani na kutenda haki. Halafu kigezo kwamba anatenda haki inayotambuliwa na kukubaliwa na Mungu amekipata wapi?

Ndugu yangu hebu achana na kupinga kila kitu kwa kuwa u mpinzani tu.

Upinzani wa kweli ni kufanya mbadala wa hayo unayoona kuwa Makonda kakosea.

Ulitaka asikemee wala asifatilie watu walioshirikiana kwa yule mrithi wa halali kudhulumiwa? Au hujasikiliza vizuri kilichokuwa kinaendelea mpaka akasema hayo?

Ningefurahi zaidi ningeona upinzani unatumia wanasheria wake "wasomi" japo kuwapeleka mahakamani wale waliodhulumu na kuhakikisha haki ya mrithi inapatikana na wale wote walioshiriki kwenye hiyo dhuluma wanachukuliwa hatua badala ya kukaa hapa na kutafuta Makonda kasema nini uanze kumpinga.

Huo ni upunguani wa hali ya juu.

Action speaks louder than words.
 
FaizaFoxy kadhia nzima nimeifuatilia. Neno huwa halina maana ila jinsi linavyotamkwa. Makonda hakulitamka kwa kumaanisha kwamba yeye yupo pale kutenda haki bali alilitamka kwa kiburi cha kimamlaka. Kwenye Khadithi za kwenye za Biblia wakristo wanafahamu kile kisa cha "mene mene tekeli na peresi" kilianzia kwenye kiburi cha Nebukadreza kujilinganisha na Mungu.Mtu muungwana angesema mimi natenda haki kama mungu alivyoagiza tutende haki!!

Upunguani mwingine si wa kuutetea badala yake wewe unayeutetea ndiye utaonekana juha!!
 
FaizaFoxy kadhia nzima nimeifuatilia. Neno huwa halina maana ila jinsi linavyotamkwa. Makonda hakulitamka kwa kumaanisha kwamba yeye yupo pale kutenda haki bali alilitamka kwa kiburi cha kimamlaka. Kwenye Khadithi za kwenye za Biblia wakristo wanafahamu kile kisa cha "mene mene tekeli na peresi" kilianzia kwenye kiburi cha Nebukadreza kujilinganisha na Mungu.Mtu muungwana angesema mimi natenda haki kama mungu alivyoagiza tutende haki!!

Upunguani mwingine si wa kuutetea badala yake wewe unayeutetea ndiye utaonekana ****!!

Weka "context" nzima maneno ya para moja kabla na para moja baada ya hilo neno ili tuuone "ukweli" wako.

Ukishindwa kufanya hivyo basi unakuwa ni ufataani tu.

Fata ushauri niliokupa juu huko.
 
Akili ya Makonda imedukuliwa. ndio maana sitaki kumsikiliza kwa chochote maisha yangu yote.
 
Mambo ya Mungu mwachieni Mungu mwenyewe, Mungu kwa wakristo hapiganiwi wala hatetewi..... yeye ndio hutupigania sisi ndio maana alimtoa Mwanae atufie kwa ajili yetu.....
 
VIONGOZI WA DINI NI WAPIGA DILI, BORA MNATOA SADAKA NA KUWASUJUDIA BASI!
 
Kunukuliwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akisema kuwa anapokuwa amesimama yeye basi anakuwa amesimama Mungu, kumeleta mfadhaiko miongoni mwa watu wenye akili timamu wanaojua nini inamaanishwa inaposemwa neno "Mungu". Lakini kauli hiyo pia imezifedhehesha dini zote zilizoko duniani.

Kila watu wakienda wanakoabudu wanaambiwa wanamuabudu "Mungu", halafu anasimama mtu na kusema akisimama yeye anakuwa amesimama Mungu, hili ni dharau kwa waabudu Mungu. Makonda anataka kusema yeye ni Mungu ama ni Mwakilishi wa Mungu?

Kama waislamu wanasema "hakuna apaswaye kuabudiwa ila ni Mungu pekee..." nao ndugu zao Wakristo wanasema "Mungu ni mwenye wivu.." inakuwaje wanakaa kimya mtu mwingine anapojifananisha na Mungu? Au viongozi wa dini nao wanaamini anaposimama Makonda anakuwa amesimama Mungu?

Ukimya wa viongozi wa dini juu ya kauli ya Makonda kuhusu Mungu unapalilia ile dhana kwamba viongozi wa dini Tanzania wana Shirika na viongozi wa Serikali wanaotokana na CCM. Maana kuna wakati watu waliuliza inakuwaje viongozi wa vyama vya upinzani huwa hawaalikwi kwenye yale matamasha ya "amani"? Kumbe inawezekana waandaji labda huwa wanaogopa kumuudhi Mungu kwa kuwaalika Mashetani.

Hata kama aliahidi kusaidia kujenga Makao Makuu ya BAKWATA ama alimtembelea Kadinali Pengo Ofisini kwake, ni lazima Makonda aonywe na akemewe hadharani kwa tendo lake la kujilinganisha na Mungu. Viongozi wa dini huo ukereketwa wenu wa CCM unawaondolea sifa ya kuwa viongozi wa dini kwani sifa mojawapo ya kuwa kiongozi wa dini ni kuzuia Mungu KUDHIHAKIWA!!
Chaburuma eti ni kweli ulisema hii kauli?
Jibu kwanza afu nkusaidie
 
Mwendawazimu akikunyang'anya taulo wala usimkimbize, chuchumaa!!!!
 
h

Hakuna Askofu wala Sheikh aliyekemea kauli hiyo. Wameridhika, wapiga dili!
 
Mkuu, umelala na kuamka. Na kifungua kinywa chako ni Makonda?
Chakula chako cha machana na jioni ni Makonda?

Tafadhali NENDA KAFANYE KAZI iliuendelee na ujenzi wa taifa.
HOJA ama MADA hiyo ilishajibiwa zamani.
Hivyo ni STALE news/KIPOLO cha habari ambacho si kitu cha muhimu KUKIRUDIA RUDIA.
Taifa lina mambo muhimu zaidi kuliko hizo fitina ndogo ndogo.
By the way,
Je umefikia wapi na huo MRADI wako uliouanzisha????
Unatetea nn we
 
Padre Mapunda, Sheikh Khalifa na Sheikh Ponda ndio wanajinasibu kuisemea jamii. Wengine naona kama wanaogopa kufutiwa leseni zao. Wapo kimyaa na jana huyo Mheshimiwa alikuwepo kwenye ibada siti ya mbele kabisa na hakuna wa kumwambia kwamba hilo alilonena ni upotovu.
Alikuwa kwenye ibada ya wapi..
Kanisa au mskiti
 
Back
Top Bottom