macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,796
- 39,596
Gender Sensitive,
Mkuu ni muhimu sana mnapoona mnashinda kitu mjue adui yenu kajiandaa vipi kukabiliana nanyi. CCM wanayo plan B kwa kila move au hatua waliyoichukua wakitegemea outcome fulani. Kama nilivyokwisha sema historia inatufunza mengi tumewaona kina Kolimba, Malima, Mwaikambo, Dr.Omar na wengine wengi ambao wameondolewa kimazingara na hakuna lililofanyika kabla wala baada ya..
Tumewapoteza viongozi hao na hakika tumebakia tukizungumza maneno tuliyolishwa kuhusiana na mapungufu yao badala ya nia ya wapiganaji hao. Hivyo Chadema mnatakiwa kujipanga kuweka guard ya kila mkijengacho kwani ni rahisi sana kwaCCM kupenya ndani na kuharibu kila mnalokusudia hasa ikiwa muda wenyewe ndio umebakia miezi tu. Hamna nafasi ya kujipanga upya..
Kuhusiana na mzee Mwanakijiji huyu mwache, ni mwandishi makini ambaye anataka kujua baada ya ushindi Chadema watafanya nini tofauti na CCM ktk maswala mengi ya kiitikadi hali mimi nimeisha mwambia huwezi kuingia vitani na biblia mkononi kama silaha yako hasa unapopigana vita na mwarabu. Shinda vita kwanza, kisha utahubiri biblia kwa hatua kwani Tanzania yetu leo hii wananchi wake hawafahamu kabisa kuhusiana na mfumo wa ITIKADI kutokana na UJINGA na kibaya zaidi UMASKINI wetu unaweza kupongeza itikadi inayowahubiri kwa zawadi na misaada kuwa ndiyo iliyo bora zaidi.
Maneno ya maana sana haya. Wengi hawajui siasa za Afrika zinaenda kiafrika.....