Mkuu,naomba nipingane nawe katika suala la kuhamasisha uwepo wa tabaka la kati.Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa katika dunia tunayoishi sasa hakuna uwezekano wa kuwa na jamii isiyo na matabaka (classless society).Tatizo sio uwepo wa matabaka bali mahusiano kati ya matabaka hayo (class relations).
Katika Tanzania yetu ya sasa ambapo civil society imeelemea zaidi upande wa tabaka tawala (na hapo tunaweka kando udhaifu wa civil society),tabaka la kati linaweza kuziba ombwe hilo iwapo litawajibika kikamilifu kupambana na ukandamizaji wa tabaka tawala kwa tabaka la walalahoi.Wengi wetu hapa JF tayari by default ni sehemu ya tabaka hilo la kati unalolihofia.Tatizo hadi sasa ni kuwa licha ya udogo na udhaifu wa tabaka hili linaloweza kuchochea mabadiliko ya kweli,wengi wa waliomo humo wanahangaika zaidi aidha kuishi kama tabaka tawala au wanatamani wawe member wa tabaka hilo la juu.Kinachopuuzwa ni ukweli kuwa tabaka hili linapaswa kuwa karibu zaidi na tabaka la chini (walalahoi) hasa kutokana na mahusiano yao ya kila siku (eg wale wenye vibarua lakini bado wanaishi na wazazi wao) na ukweli kwamba matabaka yote hayo mawilo ni wahanga wa matendo,mbinu na hila za tabaka tawala (rejea sakata la mishahara ya kima cha chini).
Ningeweza kuandika kwa kirefu ila muda na nafasi havitoshi.Ila ningependa kukutoa hofu kuwa uwepo wa tabaka la kati ni jambo hatari kwa jamii.Lililo hatari ni mahusiano kati ya matabaka na kwa tabaka la kati kuelemea upande wa tabaka tawala (kama ilivyo sasa kwa civil society) nakutelekeza wajibu.Pasipo kuziba ombwe lililopo kati ya tabaka tawala na walalahoi ni ndoto kwa mabadiliko yenye manufaa kwa walio wengi kujiri.