Viongozi wa CCJ Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Viongozi wa CCJ Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Sijaelewa kidogo kwenye hilo tamko lao: je, wemeunganisha vyama kama ASP na TANU mwaka 1977? Kama ndio basi wanachama wote wa CCJ ni Chadema. Kama ni wao tu wameamia Chadema na CCJ kuendelea kuwepo, je viongozi wa juu wa CCJ ni akina nani? Kama bado ni wao je, sheria inaruhusu jambo hilo?
 
Wanachama wa CCJ na viongozi waliobaki waiunge CHADEMA kwenye uchaguzi huku wakiwa bado ni wanachama na viongozi wa CCJ alafu baada ya uchaguzi CCJ iendelee kupigania usajili wa kudumu na kuendeleza itikadi yake? Nilifikiri sasa hivi tutasikia mwanachama mmoja wa CCJ akitake over nafasi za Viongozi wa CCJ waliohama.

sorry Signature yako ni outdated (sorry for offpoint)
 
Hakuna attachment mkuu tunaomba uirushe.

Tunawakaribisha... Mzee wa Chadema mimi nilijiunga Chadema kwa sms lakini mpaka na nikaahidiwa kuwa ningetafutwa na viongozi wa eneo ninalokaa lakini mpaka leo. takribani mwaka umepita sijawaona au kusikia lolote kutoka Chadema.. kulikoni???

Kama umejiunga na CHADEMA kwa kua unaunga mkono na wazipenda harakati na sera zao za kuleta maendeleo TZ basi na fanya kazi ya kuijenga CHADEMA. Wasipokutafuta na watafute mpaka kieleweke NA hapo utakua umewafundisha kuwajibika - hamna sababu ya kuwauliza 'kulikoni' humu kwenye forum. Naamini wanachama ni wengi. Kumfuata kila mwanachama mpya ni hali ya kusadikika, si halisi. Mchango wako ndio utaiimarisha CHADEMA na si mchango wa CHADEMA kwako.
 
Sijaelewa kidogo kwenye hilo tamko lao: je, wemeunganisha vyama kama ASP na TANU mwaka 1977? Kama ndio basi wanachama wote wa CCJ ni Chadema. Kama ni wao tu wameamia Chadema na CCJ kuendelea kuwepo, je viongozi wa juu wa CCJ ni akina nani? Kama bado ni wao je, sheria inaruhusu jambo hilo?

Wamehamia chadema hawajaunganisha vyama, ndiyo maana wanawaomba na wanachama wengine wa ccj wajiunge chadema
 
Kama namwelewa Mwanakijiji hakuwahi kuwa mpenzi wa Chadema bali alikuwa ni mwana CCM aliyechoshwa na uvundo uliotanda katika bonde CCM ilipopiga kambi na hivyo akawa anatafuta upenyo wa kupata hewa safi. Chadema hawakuweza kumhakikishia hiyo hewa safi kwa asilimia 100% lakini CCJ iliweza kumpa matumaini kwani si tu iliitia wasi wasi CCM na kuipiga tobo bali iliingia kwa staili na gia isiyo ya kawaida. Mimi ni moja wa watu waliomshangaa na wanaoendelea kumshangaa Mwanakijiji kwa msimamo wake huo lakini sasa namhakikishia kuwa huu upepo unaoanza kuvuma ni dalili ya ujio wa tsunami hivyo akae chonjo kwani tsunami haizuiliki. Nachukua hii nafasi pia kuwaomba wale wote walio na mapenzi mema na taifa hili wasikae tena kando kama watazamaji bali washiriki kwa vitendo, Tanzania yawahitaji - nchi inateketea !

Siku zote CCM imekuwa ndiyo mpiga zumari na watu kujimwaga ukumbini lakini safari hii waanze kufanya mazoezi ya kulisakata kwani muziki huu mpya ni moto wa kuotea mbali na una staili yake. Wamezoea kulikoroga na kuwaachia wanywaji, safari hii watalinywa wenyewe kwani tayari wazalendo wa kweli wamewasha indiketa na inabidi mafisadi wakae chonjo. CCJ haikufa bali ina evolve kama ilivyotarajiwa, lazima mkumbuke kuwa kuna walioshughulikiwa kimya kimya na sasa ni wenye sababu, uthubutu, ujasiri na nia ya kweli na thabiti ndiyo watabaki wamesimama baada ya kimbunga kupita, tukae tukijua hilo - Heko Chadema !

Mkuu pamoja na point zako za muhimu lakini naona umenikoti mimi,sijasema popote kwamba Mwanakijiji amewahi kuwa mwanachama wa CHADEMA..Nadhani umenielewa vibaya
 
Ndugu zangu suala la CCJ kuhamwa na Viongozi wake sijuwi limeacha funzo gani kwetu. kwangu mimi limeacha mambo yafuatayo:

1. Vyombo vyetu vya habari kutokuwa na waandishi wachuguzi ambao kabla ya kuandika habari wanatakiwa kuzifanyia uchunguzi. Maana habari za CCJ kuchukua "VIGOGO" wa CCM ziliandikwa kwa HERUFI NA WINO mzito na karibu magazeti yote Tanzania. Mimi sijuwi kama kweli Tanzania tunao waandishi waliobobea katika fani hiyo kwa maana ya mfano mtu kuwa na taaluma ya sayansi, Sheria, Utawala, Misitu, wanyama, Siyansi ya Siasa na Jamii, Polisi hata kwa kiwango cha shahada ya kwanza kisha akawa anaandika habari zinazolenga taaluma yake. Hili hakuna Tanzania. Mtu anapata kiwango cha alama ya daraja la IV shule ya Sekondari anakwenda kusomea Uandishi wa habari kwa miezi 8 kisha anapewa jukumu la kuandika habari za kisiasa au kiuchumi, au mazingira, au utawala n.k. matokeo yake ni kuandika UDAKU kuanzia magazeti ya kawaida hadi yale ya UDAKU. Na kwa kweli ni bora usome magazeti ya UDAKU maana yana habari za kweli.

1. Hawa ndo aina ya wanasiasa wetu wa Tanzania, badala ya kuhangaika kuibua hisia za wananchi wao wanafikilia kuingia katika siasa ili wawe wabunge, wanaleta UNAFIKI katika siasa, wanatumia WAANDISHI HABARI uchwala na tanzania hatuna waandishi wa habari tunao wanao nukuu habari. Magazeti yote ukisoma utaona, alisema, akasema, akasisitiza, akaongeza, akahimiza, akaendelea kusema, sasa wanasiasa wanawatumia hawa wanukuu habari kujitangaza hata kama ni wabovu.
 
SIKU moja baada ya baadhi ya vigogo wa chama kipya cha kisiasa cha CCJ kutimkia Chadema, katibu mkuu wa chama hicho, Renatus Muabhi amesema uamuzi wa waliohama unatokana na uchu wa madaraka.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana Muabhi alieleza kuwa uamuzi wao hautakiua chama hicho kilichoanzishwa kwa kishindo lakini kikakosa usajili wa kudumu kukiwezesha kushiriki uchaguzi wa mwaka huu.

Alisema kitendo cha viongozi hao kutangaza kugombea ubunge kwa tiketi ya Chadema kinaonyesha kuwa walijiunga na CCJ kutafuta umaarufu binafsi na uchu wa madaraka.

Kwa mujibu wa Muabhi kama vigogo hao wangekuwa na dhamira ya kweli ya kujenga siasa zilizoanzishwa na sera nzuri ya CCJ, wasingehama chama hicho.

Kuhusu hatua ya viongozi hao kumlalamikia Msajili wa Vyama vya Siasa, Muabhi alisema madai yao hayana msingi kwani usajili wa chama hufanywa kwa mipango na sio kukurupuka.

“Chama cha Jamii (CCJ) hakikuanzishwa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu pekee; ni chama chenye malengo mengi na ya muda mrefu. Sisi baada ya kuondoka hao, tutakutana, tufanye uchaguzi ili tuendelee na taratibu za kukisajili chama chetu,” alisema Muabi.

Muabi alieleza dhamira ya CCJ kurejesha misingi bora iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere bado ipo na chama kinaendelea kuhakikisha kinafikia lengo hiyo.

“Ingawa uamuzi wa mtu kujiunga na chama chochote cha sisasa ni haki yake, kikatiba hawa ndugu zangu wamepoteza mwelekeo kwa kuchagua njia ya mkato ya kujitafutia madaraka,” alisema Muabi.

Juzi CCJ ilimpoteza mwanachama wake maarufu, Fred Mpendazoe baada ya mbunge huyo wa zamani wa Kispahu kutangaza kujiunga na Chadema.

Pia mwenyekiti wa chama hicho, Richard Kiyabo, naibu katibu mkuu, Nickson Ng'ihily na msemaji wa CCJ, walikabidhiwa kadi za Chadema jijini Dar es Salaam na mwenyekiti Freeman Mbowe.

Muda mfupi baada ya kupokea kadi hizo, viongozi hao walitangaza nia kugombea ubunge katika majimbo tofauti nchini kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

Mpendazoe ametangaza nia ya ubunge wa jimbo la Segerea, wakati Kiyabo atagombea Bukene na Ng'ihily anagombea jimbo la Temeke.

source: gazeti la mwananchi
 
Mlango mmoja ukifungwa haimaanishi milango yote imefungwa.

Hawa ndugu wametumia haki yao ya kidemokrasia ambayo katiba ya nchi imewapa.Hivyo kwanini tunawaone dongo na hoja ambazo hazina kichwa wala miguu?Hizi analysis zenye ombwe ndio inyowafanya waandishi wengi wa habari wa Tanzania waonekane kuwa na upeo mdogo wa kuchambua mambo na kuandika habari za kichambuzi.

title kama hii inaonesha ni jinsi gani huyu mwandishi asivyojua haki za raia kama ilivoainishwa na katiba.Wote wanaogombea, akiwemo Raisi Kikwete, wana uchu wa madaraka na ni wachache sana ambao wamekwenda kuwatumikia wananchi.Sijaamini kabisa hii piece imetoka katika gazeti la Mwananchi, labda walikuwa na lao jambo (kisiasa zaidi)
 
so CCJ haina mwenyekiti, huyu muabi si ndo aliibiwa kariakoo akikata mbuga kwa miguu.
 
Hii CCJ toka kuanzishwa kwake ilionekana haiko strong. Kilichoonyeshwa kwenye Star TV jana kuanzia ofisi zao zilipo mhhh niliongeza mashaka na chama hiki.
Kama chama kinahamwa na viongozi wa ngazi za juu, ina maana hakina mwenyewe?
 
SIKU moja baada ya baadhi ya vigogo wa chama kipya cha kisiasa cha CCJ kutimkia Chadema, katibu mkuu wa chama hicho, Renatus Muabhi amesema uamuzi wa waliohama unatokana na uchu wa madaraka.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana Muabhi alieleza kuwa uamuzi wao hautakiua chama hicho kilichoanzishwa kwa kishindo lakini kikakosa usajili wa kudumu kukiwezesha kushiriki uchaguzi wa mwaka huu.

Alisema kitendo cha viongozi hao kutangaza kugombea ubunge kwa tiketi ya Chadema kinaonyesha kuwa walijiunga na CCJ kutafuta umaarufu binafsi na uchu wa madaraka.

Kwa mujibu wa Muabhi kama vigogo hao wangekuwa na dhamira ya kweli ya kujenga siasa zilizoanzishwa na sera nzuri ya CCJ, wasingehama chama hicho.

Kuhusu hatua ya viongozi hao kumlalamikia Msajili wa Vyama vya Siasa, Muabhi alisema madai yao hayana msingi kwani usajili wa chama hufanywa kwa mipango na sio kukurupuka.

"Chama cha Jamii (CCJ) hakikuanzishwa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu pekee; ni chama chenye malengo mengi na ya muda mrefu. Sisi baada ya kuondoka hao, tutakutana, tufanye uchaguzi ili tuendelee na taratibu za kukisajili chama chetu," alisema Muabi.

Muabi alieleza dhamira ya CCJ kurejesha misingi bora iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere bado ipo na chama kinaendelea kuhakikisha kinafikia lengo hiyo.

"Ingawa uamuzi wa mtu kujiunga na chama chochote cha sisasa ni haki yake, kikatiba hawa ndugu zangu wamepoteza mwelekeo kwa kuchagua njia ya mkato ya kujitafutia madaraka," alisema Muabi.

Juzi CCJ ilimpoteza mwanachama wake maarufu, Fred Mpendazoe baada ya mbunge huyo wa zamani wa Kispahu kutangaza kujiunga na Chadema.

Pia mwenyekiti wa chama hicho, Richard Kiyabo, naibu katibu mkuu, Nickson Ng'ihily na msemaji wa CCJ, walikabidhiwa kadi za Chadema jijini Dar es Salaam na mwenyekiti Freeman Mbowe.

Muda mfupi baada ya kupokea kadi hizo, viongozi hao walitangaza nia kugombea ubunge katika majimbo tofauti nchini kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

Mpendazoe ametangaza nia ya ubunge wa jimbo la Segerea, wakati Kiyabo atagombea Bukene na Ng'ihily anagombea jimbo la Temeke.

source: gazeti la mwananchi

RA at work
 
ndugu Renatus Muabhi {katibu mkuu wa CCJ} anajaribu kuonyesha kuwa kujiunga kwaNdugu Mpenzazoe na viongozi wengine wa CCJ si uamuzi wa chama {kwa ujumla} bali individual decisions na haimaanishi chama kimekufa, ambacho sikielewi na kinachonipa mashaka ni yeye kuanza kuona kuwa haki ilitendeka kuwanyima usajili wa kudumu ,
 
Na wale wanaotumia fedha za kifisadi kuhonga wapiga kura,nguvu za dola kudhoofisha upinzani tuwaiteje? Hawa wamehama kwa kuona kuwa wasingefikia malengo yao ya kuleta ukombozi wa kweli kupitia ccj, sasa ulitegemea wafanyeje?Hakuna sababu ya kuwalaani kwani hawajavunja sheria yoyote, wametumia haki yao ya kikatiba kushiriki siasa kuptia chama kilichosajiliwa, azma ambayo wasingeweza kuitekeleza kupitia ccj.
 
Wanahaki ya kikatiba; lakini kwa kuhama kwao tumegundua kumbe yale manjonjo ya mara ya kwanza ni zuga tu!!

Wanafanana na woote wenye uroho wa madaraka!!
 
anatambua kuwa msajili kakataa kuwapa usajili kwa sababu za msingi.

wameambiwa kuwa na wanachama mmoja mji mkongwe zanzibar, hawana ofisi Tanga n.k

hichi chama ni mazinga ombwe tu
 
Si cha CCJ wala CHADEMA...mambo ni kama hapa chini!

SafeRedirect.aspx
 
Hongera zangu kwa uamuzi wa busara waliochukua Mheshimiwa Mpendazoe na wenziwe. Sasa huko waendako waende na dira ya kuunganisha wapinzani na sio kuzidi kuwavuruga ama kuchukulia vyama hivyo kama backup plan ya so called Wapiganaji/wapambanaji/etc. Janga la Mrema Factor na athari yake katika ukuaji wa demokrasia makini linatosha....

omarilyas
 
Back
Top Bottom