Viongozi wa CCJ Wajiunga Rasmi na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa CCJ Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Jul 14, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jul 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Dakika chache zilizopita Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amewapokea waliokuwa viongozi wa CCJ, Richard Kiyabo aliyekuwa Mwenyekiti, Dickson Ng’hily aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CCJ Bara na Fred Mpendazoe aliyekuwa Msemaji Mkuu wa CCJ Taifa.

  Viongozi hawa wamejinga rasmi na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Mbowe mbele ya Waandishi wa Habari.

  Pamoja na kujiunga na CHADEMA Viongozi hawa pia wametoa tamko rasmi la kwanini wamejiunga na chama hiki,Find Attachment hapo chini. Vile Vile Viongozi hawa wametangaza nia ya kugombea Ubunge kupitia CHADEMA kama ifuatavyo;


  Dickson Ng’hily -Kugombea Jimbo la Temeke
  Richard Kyabo-Kugombea Jimbo la Bukene
  Fred Mpendazoe-Kugombea Jimbo la Segerea

  Matukio ya picha nadhani Waandishi wa Habari watarusha mambo yakiwa tayari

  Binafsi nimefurahishwa sana na uamuzi wa Viongozi hawa na furaha yangu itakamilika wakishinda Ubunge kwenye Majimbo yao.

  Wale wanaJF ambao ni wanachama wa CCJ wanashauriwa kujinga mapema na CCJ.

  Wenu katika Demokrasia na Maendeleo
  Gender Sensitive
   

  Attached Files:

 2. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa nzuri, lakini sijaona hii attachment.
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuna attachment mkuu tunaomba uirushe.

  Tunawakaribisha... Mzee wa Chadema mimi nilijiunga Chadema kwa sms lakini mpaka na nikaahidiwa kuwa ningetafutwa na viongozi wa eneo ninalokaa lakini mpaka leo. takribani mwaka umepita sijawaona au kusikia lolote kutoka Chadema.. kulikoni???
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Waliokuwa wanachama au wafuasi wao wameachwa wapi?
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  Nao watajiunga vyama vingine vya siasa including CCM kwa wale watakao kata tamaa na upinzani.
   
 6. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180

  by default wanachama=chadema si ndio waipiga debe/kura wao
   
 7. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ingependeza kwa wale wanchanma nao kujiunga ili kuleta upinzani wa kweli
  Aluta continua
   
 8. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  habari njema kwa Chadema ila hakuna attachment, labda unatudanganya?
   
 9. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Kwahiyo mzee Mwanakijiji naye kajiunga na CHADEMA?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wow.... GS, My friend;

  I am proud of CCJ leaders na pia i am very proud of CHADEMA for accepting this change. Hii ndiyo ndoto yangu kwenye upinzani, fighting the common enemy.

  Najua MMM naye atakua hepi na kusema ukweli huu ni uamuzi wa busara sana... UNGANENI NA KUWA NA SAUTI ZAIDI BUNGENI, ITS ONLY THEN NDIPO DEMOKRASIA YA KWELI ITAPATIKANA

  BTW, HEBU CORRECT HIZO SPELLING, HAO NI OFFICE MATES KWA SASA

  AT LIST THIS WILL ALSO SWING THE MEDIA ATTENTION TO UPINZANI
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Huu nao ni ufisadi, kwanini kiongozi mzima ukajiunge na kundi ambalo wewe una imani tofauti na wao? Hapa linakuja jibu kuwa wote wanaojiita upinzani ni vikundi vya kuganga njaa tuu, ramani ikiwa mbaya wanakimbilia kwingine. Mimi naamini katika mikono na miguu yangu
   
 12. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hahaaa hahahaaaaaa ninachoweza kusema kwa sasa ni "Kidumu Chama Cha Mapinduzi".
   
 13. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu Ntemi mfumo wa kusajili online bado haujatengemaa, kwani kuna masuala ambayo yanakuhitaji uwepo wako physically kama kulipia kadi na kusubmit picha, hivyo ushauri wangu ni kwako kufika katika ofisi ya chadema iliyo karibu nawe na ujisajiri. Kama uko Dar unaweza fika makao makuu pale kinondoni mtaa wa ufipa. Asante
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ngoja basi Bunge livunjwe ili tuone na wale vigogo wao kama watajiunga nao!
   
 15. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  swali hili nililijibu hivi
  sasa tena unaongelea viongozi!
  Labda sijakuelewa. Lakini ni dhahiri kuwa kuhama chama cha siasa n kujiunga na chama kingine ni ruksa na haki ya kila mtu. Na hiyo ndiyo demokrasia vinginevyo watu wasingehama vyama tawala kujiunga na upinzani.
   
 16. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Namsubiri MZEE MWANAKIJIJI atoe tamko kwanza!
   
 17. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  TAMKO LA VIONGOZI WA CHAMA CHA JAMII (CCJ) KUWATAKA
  WANACHAMA WA CCJ WAGOMBEE NAFASI ZA KUCHAGULIWA
  KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO KUPITIA CHADEMA
  UTANGULIZI
  Ndugu Viongozi, Wanahabari, Wanachama na Wananchi kwa ujumla.
  Tunayo furaha kubwa isiyo na kifani, kwa kuungana nanyi katika
  mkutano huu ambao unaandika historia mpya yenye kuleta mabadiliko
  ya kweli katika taifa letu la Tanzania. Historia ambayo itakumbukwa
  kizazi hata kizazi, historia itakayowafanya Watanzania wajivunie na
  kuifaidi nchi yao.
  Ndugu zangu kabla sijaeleza nini kimetuleta hapa, napenda
  kuwarudisha nyuma kidogo. January 18 mwaka huu sisi wananchi
  wazalendo tulikutana jijini Dar es Salaam kutekeleza wajibu wetu
  kikatiba wa kuunganisha mawazo yetu pamoja na kuunda chama cha
  siasa kwa jina la Chama Cha Jamii (CCJ).
  CCJ kilizingatia changamoto zote zinazoikabili nchi yetu tangu na
  baada ya uhuru na kilibeba matarajio ya wananchi wa leo na kesho,
  kikiwa na lengo kuu la kuleta mageuzi ya kitaifa ya kidemokrasia,
  kiuchumi, kijamii, na kisiasa kwa faida yetu sisi sote na vizazi vijavyo.
  USAJILI WA MUDA
  Mwezi huo huo CCJ ilipeleka maombi ya usajili wa muda katika ofisi ya
  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Na baada ya urasimu wa hapa na
  pale, hatimaye Machi 3, 2010 CCJ ilipata cheti cha usajili wa muda. Hii
  ilikuwa ni hatua ya mwanzo kabisa ili kiweze kuanza shughuli za
  kutafuta wanachana na hatimaye kikitimiza masharti yaliyopo kwa
  mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ya 1992, kiweze kupewa usajili
  wa kudumu.
  Hata hivyo, toka mwanzo ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini,
  imekuwa ikionyesha nia yake waziwazi ya kutotaka kukipa CCJ usajili
  wa kudumu hata kama kitatimiza masharti. Ndani ya siku si chini ya
  sabini (70), CCJ kilikamilisha masharti yote na kupeleka maombi ya
  usajili wa kudumu. Msajili kupitia vyombo vya habari kwa mara nyingine
  aliweka wazi nia yake ya kutotoa cheti cha usajili wa kudumu kwa CCJ.
  Ndugu wananchi, kutokana na shinikizo toka kwa watanzania wenye
  uchungu na nchi hii na wenye kutaka kuona mabadiliko, pia shinikizo
  toka kwa ofisi za kibalozi zilizopo nchini, chama cha wanasheria tawi la
  Arusha bila kusahau wanachama wa CCJ, hatimaye tarehe 3/5/2010
  msajili kwa shingo upande aliamua kufanya uhakiki wa wanachama wa
  CCJ kwa mikoa minne akianzia Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na
  baadaye Mjini Magharibi.
  Ndugu zangu nyote ni mashahidi wa hujuma tulizofanyiwa kiasi cha
  kupelekea kusitishwa kwa zoezi zima la uhakiki. Na kwa kuwa nia ya
  msajili ilikuwa ni kuichafua CCJ, alitangaza kuwa CCJ-Dar ina
  wanachama 13 tu, na licha ya kuwa tulimwandikia barua ya kusitisha
  zoezi la uhakiki bado aliendelea na Pwani kisha kutoa tamko kuwa
  CCJ-Pwani haina hata ofisi licha ya wanachama. Baadaye akasema
  Zanzibar tuna mwanachama mmoja, yote haya aliyafanya kwa
  makusudi ili CCJ ionekane si kitu.
  Msajili ameonyesha dharau na kejeli za wazi kwa watanzania,
  tungependa kuwafahamisha Watanzania kwamba, wananchi wengi
  sehemu mbalimbali za nchi yetu watu wa kila rika, dini mbalimbali
  wakiwepo wasanii, wakulima, wafanyakazi pamoja na wastaafu
  wamekikubali na kukipokea Chama Cha Jamii na wengi wamejiunga.
  Tarakimu zilizopo ofisini, mpaka sasa kuna watanzania takriban 9500
  wamejiunga na CCJ. Aidha wapo watanzania nje ya nchi kama vile
  Marekani, Japani, Uingereza, Korea ya Kusini na Afrika Kusini
  waliojiunga na CCJ.
  Watanzania hawa waliojiunga na CCJ, aidha walifika wao wenyewe
  ofisini au walishawishiwa na wananchi ambao walikuwa tayari
  wamejiunga awali ukiondoa wanachama 102 walio jiunga kwenye
  mkutano wa hadhara wa kuompokea Mh Mpendazoe uliofanyika pale
  Mwembeyanga.
  KUGOMBEA KUPITIA CHADEMA
  Kwa mda mrefu kumekuwa na mazungummzo kati ya CCJ na
  CHADEMA ya kuwa na ushirikiano na hususan katika uchaguzi mkuu
  utakaofanyika oktoba 2010, hii inatokana na ukweli kuwa vyama hivi
  vina itikadi na mwelekeo unaofanana. Ushirikiano huu ungeendelea
  hata baada ya CCJ kupata usajili wa kudumu. Sasa, kwa kuwa muda
  tuliobaki nao ni mchache kwa CCJ kupata usajili wa kudumu na
  kufanya maandalizi ya kutosha kuelekea uchaguzi mkuu, hivyo basi,
  tunatoa wito kwa wanachama wa CCJ wenye sifa na nia ya kugombea
  nafasi za uongozi wa kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao,
  kugombea kupitia CHADEMA.
  Ndugu zangu tunafanya hivi si kwa maslahi yetu au ya vyama vyetu,
  isipokuwa tunafanya hivi kwa maslahi ya Taifa. Ndio maana tumeamua
  kuachia nyadhifa zetu na kujiunga CHADEMA kama wanachama wa
  kawaida. Hivyo basi, tunawaomba wanachama wote wa CCJ bila
  kusahau wote wenye mapenzi mema na taifa hili, kuunga mkono
  maamuzi haya na kuwachagua wote watakaosimamishwa na
  CHADEMA.
  Kwa kuwa CCJ tunaamini kuwa Umoja ni Nguvu ya pekee ya wananchi
  katika kujenga Usawa na Uhuru na katika kuondoa Umaskini, Ujinga,
  Maradhi na kupambana na Ufisadi, na kwa kuwa CHADEMA kinaamini
  katika falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma ambayo inalenga katika
  kuwaamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwandaa Watanzania
  wachukue hatua kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao, hivyo
  basi tunatangaza rasmi kuwa Dickson Ngʼhily (Naibu Katibu Mkuu-
  Bara), Richard Kiyabo (Mwenyekiti-Taifa) na Fred Mpendazoe
  (Msemaji-Taifa) watagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu
  ujao kwa tiketi ya CHADEMA mara baada ya kuchukua kadi zao za
  uanachama wa CHADEMA.
  Ndugu zangu nyote ni mashahidi na mnaelewa juu ya utajiri mkubwa
  ambao Mwenyezi Mungu ameuweka ndani ya mipaka ya Tanzania.
  Hata hivyo ni jambo la kusikitisha kuwa wananchi wake ni maskini wa
  kutupwa, hiki ni kitendawili ambacho jibu lake ni la kusikitisha kwani jibu
  ni dhahiri, ni kutokana na uongozi usiojali wanyonge na usio na
  uzalendo wa CCM.
  Ni dhahiri kwamba watanzania wamechoshwa na hali hii na wanahitaji
  mabadiliko ya kweli katika uongozi na uendeshaji wa nchi, hii ni
  kutokana na ukweli kuwa CCM na serikali yake haviwezi kuleta
  mabadiliko hayo na kamwe haitaweza. Ni dhahiri kwamba watanzania
  wamechoka kuishi maisha yasiyo na matumaini, maisha yasiyo na
  mwelekeo wa kesho, hivyo mabadiliko yanahitajika.
  Na hili ndilo tumaini letu na tena hii ndiyo imani tunayoondoka nayo
  kuwa sote kwa pamoja tunahitaji mabadiliko ya dhati na kwa
  ushirikiano huu Tanzania yenye neema bila CCM inawezekana! Huu
  sio wakati wa kupigishwa porojo na kupewa kanga na Tshirts, ni wakati
  wa kusimama pamoja wanaume kwa wanawake, vijana na watoto
  kudai mabadiliko katika sanduku la kupigia kura. Narudia tena
  Tanzania yenye Neema Bila CCM inawezekana.
  Mungu ibariki Tanzania
  Asanteni kwa kunisikiliza.
   
 18. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #18
  Jul 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Pole sana Mkuu.Unapatikana wapi ili tuwasiliane na wewe au tuingie chemba(PM) ili tujadili mustakabali wa chama chetu.Usijali kadi utapata tu. Kuhusu attachement,hiyo hapo imeshawekwa..
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Jul 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Tamko lao limewaomba nao kujiunga na CHADEMA na wale waliokuwa na nia ya kugombea Udiwani au Ubunge wameombwa kugombea kupitia CHADEMA.Wengine tulikuwa nao pia kwenye Press hii..
   
 20. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  GS, Habari hii naiona haijakaa sawasawa hakuna uhakika wowote kwamba uliyotubandikia ni ya kweli.

  Hata hivyo, kama ni kweli hao waliotajwa wamejiunga na CHADEMA ili wawanie ubunge huo ni uamuzi wao na hauna uhusiano wowote na uamuzi wa wanachama wengine wa CCJ. Mie kama 'aliyekuwa mwanachama mtarajiwa' wa chama cha CCJ ambacho kwa sasa kimenyimwa usajili kwa mizengwe, sidhamirii kujiunga na CHADEMA ama chama chochote ambacho itikadi, sera na malengo yake hayajanigusa ipasavyo. Bado CHADEMA haijagusa moyo wangu ili nipate kuridhika kwamba chama hicho kina malengo thabiti ya kuhakikisha kuwepo kwa maendeleo yatakayolenga 'watu' - Watanzania wote. Mpaka sasa CHADEMA haijatuonyesha itakuwa na mikakati gani na itachukua hatua gani za makusudi kabisa kuhakikisha kwamba walioliibia taifa na kulihujumu wanachukuliwa hatua zinazostahili. Pia sijui CHADEMA kina mipango gani ya kuhakikisha hali za wanyonge wa Tanzania zinakuwa nzuri ndani ya miaka 5 ya uongozi wa CHADEMA, kwa sababu hilo linawezekana kabisa iwapo kuna mipango maalum. Hii blabla ya siasa za mrengo wa kati hazitoshi kututhibitishia chochote. Huenda nanyi kwa siasa zenu za mrengo wa kati mtazidi kukuza matabaka katika jamii.

  CHADEMA Siasa zenu za majimbo zina kasoro kwa wale tunaoamini juu ya kuendeleza ujenzi wa umoja nchini. Juzijuzi nilimsikia kiongozi mwandamizi wa CHADEMA akizungumza na kutetea kwa nguvu zote wagombea wanaowania uongozi - ubunge, udiwani nk. waruhusiwe kupiga kampeni kwa lugha za kikabila badala ya Kiswahili. Hizi ndio sera zenu CHADEMA za maendeleo za kutaka turudi kwenye kuongea kimatumbi na ki-barbeig majukwaani?

  Jingine lililonistua ni kumsikia kiongozi mmoja wa Taasisi moja ya Uchumi nchini (anaweza akawa mwanachama wa CHADEMA) akizungumzia habari ya kutaka kuwepo kwa "middle class" nchini na akawahamasisha Watanzania walio Marekani kuungana na walio nchini kuanzisha hiyo "middle class". Sasa huenda na ninyi CHADEMA siasa zenu za mrengo wa kati zina nia ya kutuletea na kujenga matabaka nchini kama ilivyo kwenye nchi za kibepari - wawepo Watanzania wa juu, wa kati na wa chini! CCJ isipokuwepo, ntaunga mkono chama kinachotetea kwa dhati kabisa usawa na haki sawa kwa kila Mtanzania katika mgawanyo wa keki ya Taifa.

  Kwa maoni yangu, kuwa na wapinzani wengi bungeni ambao hawana itikadi maalum inayowaunganisha nako ni kupoteza wakati na nguvu. Mwisho wa siku nchi itaendeshwa kwa mfumo gani?
   
Loading...