Viongozi wa Afrika na Umri Wao

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
14,510
17,128
Afrika tuna sifa ya kuongozwa na wazee sana. Vile vile idadi ya viongozi wa Afrika ambao wamekuwapo madarakani kwa zaidi ya miaka 10 ni kubwa kidogo. Kama nchi nyingi zilivyoanza kuwa na term limits, kuna haja ya kuweka age limit pia kwa viongozi. Mzee wa Miaka 75 kweli anahitaji kuwa mshauri to kwa vile katika umri huo hawezi kupambana na purukushani ziendazo na majukumu yake ipasavyo. Huishia kuwa wanatuma wasaidizi wawafanyie mambo na hivyo kuruhusu makosa mengi ya kiutendaji. Angalia jedwali lifuatalo linaloonyesha jina la kiongozi, umri wake, nchi anayoongoza na muda wake madarakani:
 • Group A: Above 60 Years of Age
  • Above 70 Years of Age
   1. Robert Mugabe - 83 - Zimbabwe (1980-Todate = 27 years)
   2. Abdoulaye Wade - 81 -Senegal (2000-Todate = 8 years)
   3. Hosni Mubarak - 79 - Egypt (1981 - Todate = 26 years)
   4. Anerood Jugnauth - 77 - Mauritius (2003 - Todate =4 years)
   5. Mwai Kibaki - 76 - Kenya (2002-Todate = 5 years
   6. Paul Biya - 74 - Cameroon (1982-Todate = 25 years)
   7. Bingu wa Mutharika - 73 - Malawi (2004- Todate = 3 years)
   8. Lansana Conté - 73 Guinea (1984-Todate = 23 years)
   9. Abdullahi Yusuf Ahmed - 73 - Somali (2004 - Todate = 3 years)
   10. Hifikepunye Pohamba - 72 - Namibia (2005- Todate = 2 years)
   11. Omar Bongo - 72 - Gabon (1967 - Todate = 40 years)
   12. Zine El Abidine Ben Ali - 71 Tunisia ( 1987-Todate = 20 years)
   13. Abdelaziz Bouteflika - 70 -Algeria (1999- Todate = 9 years)
  • Above 60 Years of Age
   1. John Kufuor - 69 - Ghana (2001-Todate =7 years)
   2. Ellen Johnson-Sirleaf - 69 Liberia (2006-Todate = 2 years)
   3. Sidi Ould Cheikh Abdallahi - 69 -Mauritania (2007 - Todate = 1 year)
   4. Tandja Mamadou - 69 - Niger (1999-Todate = 7 years)
   5. João Bernardo Vieira - 68 -Guinea-Bissau (2005 -Todate = 2 Years)
   6. José Eduardo dos Santos- 66 - Angola (1979-Todate =28 years)
   7. Thabo Mbeki - 65 -South Africa (1999-Todate =8 years)
   8. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo - 65 -Equatorial Guinea (1979 - Todate = 29 Years)
   9. Muammar al-Gaddafi - 65 - Libya (1969 - Todate = 39 years)
   10. Armando Guebuza - 64 -Mozambique (2005-Todate = 2 years)
   11. Denis Sassou Nguesso - 64 - Congo Brazaville (1997-Todate =10 years)
   12. Festus Mogae - 68 - Botswana (1998- Todate = 9 years)
   13. Yoweri Museveni - 63 -Uganda (1986 - Todate =21 years)
   14. Omar al-Bashir - 63 - Sudan (1989- Todate = 19 Years)
   15. Laurent Gbagbo - 62 -Ivory Coast ( 2000 - Todate = 7 Years)
   16. François Bozizé - 61 - Central African Republic (2003 - Todate = 4 years)
 • Group B: Below 60 Years of Age
  • Above 50
   1. Amadou Toumani Touré - 59 - Mali (2002-Todate = 5 Years)
   2. Levy Mwanawasa - 59 - Zambia (2002 - Todate = 5 years)
   3. Jakaya Kikwete - 57 - Tanzania (2005 - Todate = 2 years)
   4. Blaise Compaoré - 56 - Burkina Faso (1987- Todate =20 years)
   5. Idriss Déby - 55 - Chad (1990- Todate =17 years)
   6. Boni Yayi - 55 - Benin (2006 - Todate = 1 year)
   7. Ernest Bai Koroma - 54 - Sierra Leone (2007 - Todate = less than 1 year)
   8. Meles Zenawi - 52 - Ethiopia (1995 - Todate = 12 years)
   9. Marc Ravalomanana - 58 - Madagascar (2002 - Todate = 5 years)
   10. Paul Kagame - 50 - Rwanda (2000- Todate = 8 years)
   11. Umaru Yar'Adua - 51 - Nigeria (2007 - Todate = less than 1 year)
  • Below 50
   1. Pierre Nkurunziza - 44 -Burundi (2005 - Todate = 2 years)
   2. King Mohammed VI - 44 - Morocco (1999- Todate =8 years)
   3. King Letsie III - 44 - Lesotho (1990 - Todate = 17 Years)
   4. Yahya Jammeh - 42 - Gambia (1994 - Todate = 13 years)
   5. Faure Gnassingbé - 41 - Togo (2005 - Todate = 2 years)
  • Below 40
   1. King Mswati III- 39 - Swaziland (1986 - Todate =21 years)
   2. Joseph Kabila - 36 - Congo (2001 - Todate = 6 Years)
 
Ahsante kwa list Kichuguu.

Tatizo uki question tu hao above 60, watakwambia kuwa umri ni wisdom...
Angalia mtu kama Kibaki, just like Mkapa wetu Tanzania, instead ya ku retire kwa hekima na thawabu kubwa, wote wataondoka na historia za kuhuzunisha kizazi hiki na kijacho kutokana na tamaa zao! mmoja kung'ang'ania kubakia madarakani na mwingine kujifanya mjasiriamali ikuluni..

Tuangalie tu hao wenye umri mdogo, akina Kabila and the likes... je mambo ni yale yale... huchelewi tukajikuta Kabila anatawala maisha kama Fidel Castro!!


SteveD.
 
Tunaweka term limits na age limits. Kwa sasa hivi kutokuwepo kwa age limit kunasababisha vyama vinateua watu wazee kabisa, mradi tu walikuwa kwenye system; kwa lugha nyingine madaraka yanapasiwa kutoka mzee mmoja kwenda mzee mwingine kama ilivyokuwa Namibia
 
1. Hili wazo la kutoa age limits za wazee- siyo kuwabagua? Hata Kabila amemteua PM wenye miaka 81 au 82 kama sijakosea!

2. Hivi kuna limit kikatiba pia kuwa na minimum age limit? Is this important?
 
Our social norms(religion and traditions) permit this. The articulation of our elders. Sadly it is a way of life.

Lakini ibadilike with a principal, Wananchi kama hawawataki.(wazee),wang'atuke.Wananchi hapa ndio jamii yenyewe(watu wenye umri mbali mbali)waheshimu matakwa yetu.

Age limit siyo solution.
I submit!
 
Mwl. Kichuguu,

Ukiangalia vizuri hili jedwali utaona lina mambo mengi sana ambayo ni kikwazo kikubwa cha maendeleo barani Africa.

Inaelekea umri ni tatizo kubwa. Vilevile mataifa yaliyoendelea yameisha shtukia hichi kikwazo. Ukiangalia watu waliompigia kura Obama kule Iowa kwa mfano, ni watu wenye umri kati ya miaka 18 na 40; na wote hawa wanataka mabadiliko.

Afrika unawatu wale wale, wanafanya vitu vile vile kutumia njia zile zile matokeo yake huwezi kupata matokeo tofauti. Ninadhani kuna haja ya kuzingatia umri tunapowachagua viongozi wetu kutokana na mabadiliko ya siku hizi. Kwani hata Kikwete inaonekana ni kiongozi ambaye amepitwa na wakati kutokana na jinsi anavyofanya shughuli zake.

Lakini, kikwazo chechu ni utamaduni na imani zetu za kiafrika kuwa wazee wanabusara na hekima tunasahau kuwa dunia ya leo tofauti kabisa na wakati uliopita.
 
Naona Omar Bongo na Gaddafi wanamkimbilia "The Great Leader" Kim Il-Sung wa North Korea (miaka 46 uongozini mpaka alipokufa, akaja kurithiwa na mwanaye!).

Ongeza miaka michache pamoja na (ashakum) uwezekano wa kuondoka kwa Castro, wanaweza hata kuchukua medali hii ya Olimpiki maalum ya kuhodhi madaraka.

Ni rahisi kukubali kishawishi kwamba umri ni tatizo, lakini ningependa kuondoa umri kama tatizo.Kwa kweli ningependa kuondoa hata umri wa chini wa kugombea urais kutoka miaka 40 ya hivi sasa mpaka miaka ya kupiga kura 18, si imesemwa katika misahafu kwamba yaliyofichwa kwa wazee wenye busara yatafunuliwa kwa watoto?

Ni rahisi sana kuweka vikwazo kwa kutumia kura, kama wananchi hawataki viongozi wazee wananchi hao hao wanaweza kuwakataa kwa kutowapigia kura.Tukiweka vikwazo vya kiumri tunaweza kukosa nafasi ya kumchagua kiongozi mzuri kwa msingi huo.Kama vile tulivyoona kwamba sio kila kiongozi kijana ni mzuri, sio kila kiongozi mzee ni mbaya.

Wanaharakati wanaweza kutuambia kuwa kuwakatalia wazee wetu nafasi za kutuongoza hakuna tofauti sana kimantiki kukilinganishwa na kuwafyeka kwa mapanga wazee wenye macho mekundu.Maembe na machungwa yote ni matunda, haya nayo yote ni masuala ya ubaguzi wa umri.Tutakuwa tunatafuta "mchawi" asiyepo katika swala ambalo dawa yake tunayo wenyewe, kura.

Ningependa kuona wanachi wanaelimika zaidi kuhusu haya maswala ili kuwezeshwa kupiga kura zinazoleta maendeleo.
 
Tatizo linalokwamisha maendeleo Afrika ni moja: Waafrika Ndivyo Tulivyo! Sasa ktk hili tatizo moja, ndani yake kuna mambo lukuki lakini ukichanganua kila kipande kwa undani zaidi utajikuta unarudi palepale kwenye Waafrika Ndivyo Tulivyo!! Kwa hiyo hata tuweke age limit (which can be discriminatory) haitakua utatuzi wa matatizo yetu.
 
Tatizo linalokwamisha maendeleo Afrika ni moja: Waafrika Ndivyo Tulivyo! Sasa ktk hili tatizo moja, ndani yake kuna mambo lukuki lakini ukichanganua kila kipande kwa undani zaidi utajikuta unarudi palepale kwenye Waafrika Ndivyo Tulivyo!! Kwa hiyo hata tuweke age limit (which can be discriminatory) haitakua utatuzi wa matatizo yetu.

Kwa vile hukufafanua maana ya Waafrika ndivyo tulivyo, nimeshindwa kukuelewa vizuri lakini napingana na wewe kuhusu hili nililo wekea maandishi mekundu.
Age limit siyo discriminatory. Ndiyo maana kuwa mandatory retirement age; ufanisi katika kazi nyingi sana hufuata pia umri wa mhusika. Huwezi kuwa Miss Tanzania ukiwa na miaka 60, huwezi kucheza mpira wa miguu au kukimbia riadha ukiwa na umri wa miaka 60, huwezi kuwa mpiganaji kwenye jeshi miguu (infantry) ukiwa na miaka 60, na kadhalika kwa nini iwe ni swa wewe kuongoza watu kwa kazi ambazo wewe mwenyewe huwezi kuzifanya?

Ulishamwona Mugabe akiwa kwenye mikutano (tena ya kimataifa)?

mugabe-sleeping-magaisa.jpg
.......
 
JK is in middle 50's is he any better? sasa kuwaweka washkaji wake ktk kila sehemu na haya mambo ya usanii je if he were 80 or 40 would it make a diffrence?

Saa ingina uwezo wa kuongoza ni kipaji- sii tu umri, viongozi vijana ndo hao akija Joeseph Kabila na Nrurunzinza- je kuna maajabu yoyote tunayaona DRC na Burundi kwa sasa?
 
Kwa vile hukufafanua maana ya Waafrika ndivyo tulivyo, nimeshindwa kukuelewa vizuri lakini napingana na wewe kuhusu hili nililo wekea maandishi mekundu.
Age limit siyo discriminatory. Ndiyo maana kuwa mandatory retirement age; ufanisi katika kazi nyingi sana hufuata pia umri wa mhusika. Huwezi kuwa Miss Tanzania ukiwa na miaka 60, huwezi kucheza mpira wa miguu au kukimbia riadha ukiwa na umri wa miaka 60, huwezi kuwa mpiganaji kwenye jeshi miguu (infantry) ukiwa na miaka 60, na kadhalika kwa nini iwe ni swa wewe kuongoza watu kwa kazi ambazo wewe mwenyewe huwezi kuzifanya?

Ulishamwona Mugabe akiwa kwenye mikutano (tena ya kimataifa)?

mugabe-sleeping-magaisa.jpg
.......

Kwenye hili la umri napingana na wewe kwa sababu uraisi ni nafasi ya kisiasa and in politics (and even in leadership) there is no age limit.
 
Kwenye hili la umri napingana na wewe kwa sababu uraisi ni nafasi ya kisiasa and in politics (and even in leadership) there is no age limit.

Kama age siyo issue, kwa nini Katiba ya Tanzania inazuia vijana chini ya miaka 45 wasigombee Urais? Je hiyo nayo ni discrimination kwa vile umri unaotambulika wa mtu mzima ni kuanzia miaka 18?
 
Nyani,
'I think there should be an age limit. Angalia ile picha ya Mugabe. You think he knows what is going on in Zimbabwe? Mwangalie Kibaki katika ile video ya kuapishwa. There should be an age limit.
 
Nyani,
'I think there should be an age limit. Angalia ile picha ya Mugabe. You think he knows what is going on in Zimbabwe? Mwangalie Kibaki katika ile video ya kuapishwa. There should be an age limit.

Hiyo limit iwe miaka mingapi? Na kutumia hiyo picha ya Mugabe akiuchapa usingizi si sawa hata kidogo na haithibitishi chochote. Unakumbuka ile picha ya baadhi ya viongozi wa bongo waliofotolewa wakiwa wamesinzia? Unataka kunambia wale wote walikuwa umri wa Mugasbe? Hapo Mugabe usikute alikuwa ameboreka na akaamua kuuchapa.

Kichuguu, hivi kweli unataka kuniambia kati ya wanafunzi wako wote hamna wanaosinzia darasani?
 
Kama age siyo issue, kwa nini Katiba ya Tanzania inazuia vijana chini ya miaka 45 wasigombee Urais? Je hiyo nayo ni discrimination kwa vile umri unaotambulika wa mtu mzima ni kuanzia miaka 18?

Ndiyo, hii nayo ni discrimination kwa sababu kama mtu anaweza akapiga kura akiwa na umri wa miaka 18 sioni sababu kwa nini asiweze kugombea nafasi yoyote ile hata uraisi. Sasa vyama binafsi vinaweza vikawa na taratibu na vigezo vyao wenyewe lakini katiba ya nchi isizuie watu wenye uwezo wa kuongoza kwa vile tu umri wao ni mkubwa. In the US the legal drinking age is 21 but you have 18, 19, and 20yr olds in Iraq fighting in a war and some of them actually kill but when they come back to their country they can't purchase alcohol.....puuuuh-lease!!!
 
Kusinzia mara nying huwa unatokea mchana baada ya lunch wakati metabolism inatokea- je ni mara ngapi umewaona hawa viongozi wanazinzia asb?

Basi kama wanasinzia asb may be hawakulala vizuri- au ni walevi wa ma.xx.zi ya alfajiri nayo huwa huweza huchosha! Hii wake zao wanaweza kerekebisha tu!

Au kama wanasinzia asb. huwa walichelewa kulala au ni hang over ya kinywaji cha week end!

Kuna siku nimeona JK wakati wa msiba wa Akikweti amesinzia- je nae ni umri sawa na Mugabe?

Saa ingine joto kali na humidity hufanya mtu asinzie!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom