Waziri Aweso Amshukuru Rais Samia ukarabati Chuo cha Maji, atoa maagizo mazito

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso, amefanya kikao kazi na watumishi wa Chuo cha Maji pamoja na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu ambayo mchakato aliuanzisha na Rais Samia kuridhia kutoa fedha na tayari Ukarabati wa Mabweni umekamilika na sasa kazi ya ujenzi wa Maktaba kubwa ya kisasa unaendelea.

Waziri Aweso ameridhishwa na hatua ujenzi ulipofika na kuipongeza menejimenti ya Chuo cha Maji kwa kutekeleza maelekezo yake kwa vitendo na zaidi akimshukuru Mhe Rais Samia kwa kuridhia na kutoa fedha za Ukarabati wa Chuo hiki.

Katika kikao hicho, Waziri Aweso ametoa pongezi kwa Chuo cha Maji kwa kazi kubwa wanayofanya na amewataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na ubunifu.

Ameelekeza kwamba mafunzo yote ya kujenga uwezo kwa viongozi wa Wizara ya Maji yafanyike kwenye Chuo cha Maji.

Amesema kuwa chuo hicho kina wataalamu wa kutosha, vifaa, na miundombinu inayofaa kutoa mafunzo hayo kwa kiwango kinachostahili.

Aidha, ameagiza Menejimenti ya Wizara ya Maji ifanye kikao na menejimenti ya Chuo cha Maji ili kuweka mpango wa kuajiri vijana waliohitimu chuo hicho na kuwaingiza kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za Sekta ya Maji.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameeleza kuwa yeye ni mdau mkubwa wa Chuo cha Maji. Amezungumzia jinsi alivyokuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) na kuajiri wafanyakazi zaidi ya 1200 kutoka Chuo cha Maji.

Amewasifu wafanyakazi hao kwa weledi wao kazini na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Chuo cha Maji ili kuendeleza uzalishaji wa wataalamu wenye sifa katika Sekta ya Maji.

Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt Adam Karia amemshukuru Waziri wa Maji kwa kutoa mchango mkubwa katika kukiendeleza Chuo, tangu akiwa Naibu Waziri wa Maji mpaka sasa. Aliendelea kumshukuru waziri kwa kumwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasan Shilingi Bilioni 1.5 za kukarabati mabweni yaliokuwa yamechakaa.

WhatsApp Image 2023-08-27 at 19.37.27.jpeg
 
Aweso ni miongoni mwa vijana wachache wakujivunia.
HUYU AWESU KWA WASIOMFAHAMU WANAWEZA KUFIKILI NI MTU MZURI SANA KWA HIZI SANAA ZAKE ZA MEDIA. NI MWIZI SANA NA MLA RUSHWA MKUBWA HAFAI HATA KUWA BALOZI NYUMBA 10. NI VILE MATITHI YETU NAYO OVYO WAMEZOEA KULINDA CCM BADALA YA NCHI. HUYU ALIPASWA KUWA JELA. REJEA TAARIFA KIGOGO 2014 NA ZINGINE ZA WAFANYAKAZI WA WIZARA
 
Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso, amefanya kikao kazi na watumishi wa Chuo cha Maji pamoja na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu ambayo mchakato aliuanzisha na Rais Samia kuridhia kutoa fedha na tayari Ukarabati wa Mabweni umekamilika na sasa kazi ya ujenzi wa Maktaba kubwa ya kisasa unaendelea.

Waziri Aweso ameridhishwa na hatua ujenzi ulipofika na kuipongeza menejimenti ya Chuo cha Maji kwa kutekeleza maelekezo yake kwa vitendo na zaidi akimshukuru Mhe Rais Samia kwa kuridhia na kutoa fedha za Ukarabati wa Chuo hiki.

Katika kikao hicho, Waziri Aweso ametoa pongezi kwa Chuo cha Maji kwa kazi kubwa wanayofanya na amewataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na ubunifu.

Ameelekeza kwamba mafunzo yote ya kujenga uwezo kwa viongozi wa Wizara ya Maji yafanyike kwenye Chuo cha Maji.

Amesema kuwa chuo hicho kina wataalamu wa kutosha, vifaa, na miundombinu inayofaa kutoa mafunzo hayo kwa kiwango kinachostahili.

Aidha, ameagiza Menejimenti ya Wizara ya Maji ifanye kikao na menejimenti ya Chuo cha Maji ili kuweka mpango wa kuajiri vijana waliohitimu chuo hicho na kuwaingiza kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za Sekta ya Maji.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameeleza kuwa yeye ni mdau mkubwa wa Chuo cha Maji. Amezungumzia jinsi alivyokuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) na kuajiri wafanyakazi zaidi ya 1200 kutoka Chuo cha Maji.

Amewasifu wafanyakazi hao kwa weledi wao kazini na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Chuo cha Maji ili kuendeleza uzalishaji wa wataalamu wenye sifa katika Sekta ya Maji.

Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt Adam Karia amemshukuru Waziri wa Maji kwa kutoa mchango mkubwa katika kukiendeleza Chuo, tangu akiwa Naibu Waziri wa Maji mpaka sasa. Aliendelea kumshukuru waziri kwa kumwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasan Shilingi Bilioni 1.5 za kukarabati mabweni yaliokuwa yamechakaa.

View attachment 2731259

Sawa.
 
Hongera sana Waziri kwa kumpongeza Rais.

Ushauri wangu kwa Serikali na viongozi wa Serikali ngazi mbali mbali hasa mamlaka ya Urais, siku moja moja muwapongeze watanzania walipa kodi kwa bidii ya kulipa kodi za aina mbali mbali na kuwezesha miradi mingi kukamilika.

Ahsante.
 
Kila mwaka akija kwenye graduation anatoa ahadi hiohio ya ajira ila haitimizwi..ni mwaka na nne namsikia..mh.aweso we ni boss wangu nakuomba anza na hizi mamlaka wafanyakazi wengi hawajaToka maji
 
Back
Top Bottom