Vioja vya JK: Atunukiwa tuzo ya kimataifa ya Kilimo

Status
Not open for further replies.
kwa afrika uwenda ikawa yeye kuna kitu kafanya kuliko wenzake wote, mana viongozi wote wa africa ni walewale tu, mdomo mbele! labda yeye angalau wameona kaingiza matrekta mengi bandarini kwake, mana kuna nchi zingine za afrika hata mua hawalimi wanauza mapaka fisi! huwezi jua wametumia kigezo gani bana! watu wanalima sukari mpaka wanaziuza nje,so wanajua jamaa analima sana, mahindi mpaka yanabebwa na magari ya jeshi kwa mwambungu bana. kilimo kiko poa tu bongo, sema misingi na masahi kwa kuwawezesha wakulima hasa wadogo ndo bado sana, hapo ndo mistake ilipo kubwa! ili upate jibu zuri jaribu kulinganisha na nchi za africa wala hata usiende nchi za mbali nenda jirani zetu tu hapo, ndo utajua je jamaa kastahiki kwa hiki au lah! yangu ni hayo tu

Mzee Marx acha utani, ..., yaani hapo kwenye red umenichekeshi kweli! Be serious, una uhakika? Kama nchi gani? Yaani wakose hata swala wauze fisi?
 
Mzee Marx acha utani, ..., yaani hapo kwenye red umenichekeshi kweli! Be serious, una uhakika? Kama nchi gani? Yaani wakose hata swala wauze fisi?

mkuu uko wapi wewe! waulize alshababy wanauza nini? wakenya wanalishwa sana fisi na hawa jamaa
 
Hivi mnazungumzia tuzo aliyopewa ni ya haya Mahindi??
jk1xx.JPG
 
nisaidie kiongozi, kafanya nini ili nami nijue?

kafanya vingi sana.
1. Kafanya wakulima wengi wa kahawa kukata mikahawa yao kutokana na gharama ya uzalishaji kuwa kubwa kuliko ya uuzaji.

2. Bei ya pamba kuwa Tsh 800/=

3. Mbolea ya ruzuku inayoishia mikononi mwa matajiri.

4. Kuingiza power tela nyingi tena kwa kifisadi.
Hivi ni baadhi tu vipo vingi zaidi.
 
kafanya vingi sana.
1. Kafanya wakulima wengi wa kahawa kukata mikahawa yao kutokana na gharama ya uzalishaji kuwa kubwa kuliko ya uuzaji.

2. Bei ya pamba kuwa Tsh 800/=

3. Mbolea ya ruzuku inayoishia mikononi mwa matajiri.

4. Kuingiza power tela nyingi tena kwa kifisadi.
Hivi ni baadhi tu vipo vingi zaidi.

hahahaha asante mkuu naamini ujumbe nimeupata
 
Kule Chalinze kwao kuna Mananasi lakini katika picha hii alionekana anashangaa Mananasi yanayolimwa nchini Ghana katika shamba la Bomarts Farms! Huyo Muhindi nina wasiwasi naye kwakumpatia jamaa hiyo tuzo!
ga5.jpg
 
zawadi imetolewa kwa kusoma makabrasha yanayoelezea kilimokwanza; data za matrekta yaliyoagizwa; idadi ya ajira mpya katika kilimo na ongezeko la maafisa kilimo; ongezeko la umwagiliaji na vitu kama hivo. Kama pia wameengalia ongezeko la mavuno na hifadhi ya chakula (food security status) itakuwa vema. kaba ni makabrasha pekee basi ipo kasoro
 
Nimeiona hii taarifa ya Ikulu nimecheka sana. Hebu isomeni nanyi muone.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO LA KIMATAIFA LA KILIMO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo Maalum ya Sera za Usalama wa Chakula na Uongozi Katika Sekta ya Kilimo ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wake na uongozi wake katika sekta hiyo ya kilimo.

Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Mtandao wa Kutathmini Sera za Kilimo na Maliasili – Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) katika hafla maalum iliyofanyika jioni ya jana, Jumatano, Septemba 5, 2012, wakati wa mkutano wake wa mwaka unaofanyika kwenye Hoteli ya White Sands mjini Dar es Salaam.

Rais Kikwete anakuwa kiongozi wa tano wa Afrika kupokea Tuzo hiyo ambayo kwa lugha ya Kiingereza inajulikana kama Food Security Policy Leadership Award tokea kuanzishwa kwa Tuzo hiyo mwaka 2008 wakati ilipotolewa kwa aliyekuwa Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika.

Viongozi wengine ambao wamepata kutunukiwa Tuzo hiyo ni Rais Armando Emilio Guebuza wa Mozambique mwaka 2009, Rais Hifikepunye Pohamba wa Nambia mwaka 2010 na Malkia, Mama wa Mfalme Ntombi, Indlovukazi wa Swaziland.Akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo hiyo, Rais Kikwete aliwapitisha washiriki wa mkutano huo kwenye hatua zote ambazo Serikali yake inachukua kupambana na changamoto zote zinazokifanya kilimo cha Tanzania kubakia kwenye uduni ikiwa ni pamoja na kuongeza maeneo ya umwagiliaji, matumizi ya mbegu bora, matumizi ya madawa ya kuua wadudu, matumizi ya mbolea nyingi zaidi, uboresha wa miundombinu ya barabara vijijini, uimarishaji wa vikundi vya ushirika wa uzalishaji na upanuzi na uimarishaji wa masomo.

Imetolewa na
:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam
.
6 Septemba, 2012

My Take: Kwa kipi alichokifanya kwenye kilimo? au ndio kutaka kutuonyesha kuwa ni kweli KILIMO KWANZA na sio ELIMU KWANZA kama EL alivyosema???



siku hizi JF yapoteza mwelekeo, watu mnakuja juu nakututisha kutufungia, ila kiukweli JF tumekosa mwelekeo na ile sifa tuliyokuwa nayo inazidi kuyeyuka km theluji inapopigwa na jua. Rais JK ndio rais pekee Afrika group la G8 walimuita kwa ajili yaku share nae sera za kilimo, je hawa hawajui alichofanya? kuweni makini wana JF tunashusha hadhi jukwaa hili
 
Peri Lowasa hakusema eElimu kwanza wala hajasemakilmo sio kwanza, alichosema ni Elimu mbele, Kilimo kwanza, kitu amabacho nakikubali, maana hata kamani mkulima mdogo lakini kasoma atajua namna ya kupambanua hata mabadiriko yatabia ya nchi.(climate change). Lakini pia kwa tuzo hii Mh Rais anastahili. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
 
[h=2]Friday, September 7, 2012[/h] [h=3]RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI BORA KATIKA SERA ZA KILIMO NA CHAKULA[/h]
[h=5] [/h] Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012.
Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.
Source: [url]http://francisgodwin.blogspot.com[/URL]
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom