Vioja vya JK: Atunukiwa tuzo ya kimataifa ya Kilimo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vioja vya JK: Atunukiwa tuzo ya kimataifa ya Kilimo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Sep 6, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Nimeiona hii taarifa ya Ikulu nimecheka sana. Hebu isomeni nanyi muone.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO LA KIMATAIFA LA KILIMO
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo Maalum ya Sera za Usalama wa Chakula na Uongozi Katika Sekta ya Kilimo ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wake na uongozi wake katika sekta hiyo ya kilimo.

  Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Mtandao wa Kutathmini Sera za Kilimo na Maliasili – Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) katika hafla maalum iliyofanyika jioni ya jana, Jumatano, Septemba 5, 2012, wakati wa mkutano wake wa mwaka unaofanyika kwenye Hoteli ya White Sands mjini Dar es Salaam.

  Rais Kikwete anakuwa kiongozi wa tano wa Afrika kupokea Tuzo hiyo ambayo kwa lugha ya Kiingereza inajulikana kama Food Security Policy Leadership Award tokea kuanzishwa kwa Tuzo hiyo mwaka 2008 wakati ilipotolewa kwa aliyekuwa Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika.

  Viongozi wengine ambao wamepata kutunukiwa Tuzo hiyo ni Rais Armando Emilio Guebuza wa Mozambique mwaka 2009, Rais Hifikepunye Pohamba wa Nambia mwaka 2010 na Malkia, Mama wa Mfalme Ntombi, Indlovukazi wa Swaziland.Akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo hiyo, Rais Kikwete aliwapitisha washiriki wa mkutano huo kwenye hatua zote ambazo Serikali yake inachukua kupambana na changamoto zote zinazokifanya kilimo cha Tanzania kubakia kwenye uduni ikiwa ni pamoja na kuongeza maeneo ya umwagiliaji, matumizi ya mbegu bora, matumizi ya madawa ya kuua wadudu, matumizi ya mbolea nyingi zaidi, uboresha wa miundombinu ya barabara vijijini, uimarishaji wa vikundi vya ushirika wa uzalishaji na upanuzi na uimarishaji wa masomo.

  Imetolewa na
  :

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu.

  Dar es Salaam
  .
  6 Septemba, 2012

  My Take: Kwa kipi alichokifanya kwenye kilimo? au ndio kutaka kutuonyesha kuwa ni kweli KILIMO KWANZA na sio ELIMU KWANZA kama EL alivyosema???
   
 2. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Kama huoni alichofanya..... basi, inawezekana una macho lakini hayaoni.
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Anastahili si majuzi tuu alionyeshwa akimenya mahindi aliyovuna shambani kwa Bagamoyo?
   
 4. m

  markj JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  kwa afrika uwenda ikawa yeye kuna kitu kafanya kuliko wenzake wote, mana viongozi wote wa africa ni walewale tu, mdomo mbele! labda yeye angalau wameona kaingiza matrekta mengi bandarini kwake, mana kuna nchi zingine za afrika hata mua hawalimi wanauza mapaka fisi! huwezi jua wametumia kigezo gani bana! watu wanalima sukari mpaka wanaziuza nje,so wanajua jamaa analima sana, mahindi mpaka yanabebwa na magari ya jeshi kwa mwambungu bana. kilimo kiko poa tu bongo, sema misingi na masahi kwa kuwawezesha wakulima hasa wadogo ndo bado sana, hapo ndo mistake ilipo kubwa! ili upate jibu zuri jaribu kulinganisha na nchi za africa wala hata usiende nchi za mbali nenda jirani zetu tu hapo, ndo utajua je jamaa kastahiki kwa hiki au lah! yangu ni hayo tu
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  hapo kweli kwa kabila la wakwer.e pale alihitaji tuzo maana kilimo huenda si jadi yao, ukienda kwa wafipa sumbawanga yale mahindi ni cha mtoto
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  nisaidie kiongozi, kafanya nini ili nami nijue?
   
 7. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sina kumbukumbu vizuri lakini mpaka miaka ya 1990+ kilimo ndiyo ilikuwa muhimili wa uchumi TZ ambapo Pamba, Kahawa, Karafuu, na mazao mengine ya Bihashara yalikuwa yanazalishwa kwa wingi nchini. Sasa ni kweli anastahili tuzo ilo maana yeye kafanya mapinduzi ya hali ya juu ambapo mazo ya Chakula kama Mpunga na Mahindi yamegeuka ya Kibihashara zaidi kiasi cha serikali kushindwa kuyazuia yasiuzwe magendo!. Na uchumi wetu hautegemei kilimo tena,
   
 8. M

  Moony JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ANAJITAHIDI.


  • Sera yake ya kilimo kwanza na kuruhusu investors wa kilimo kikubwa cha kisasa kama SAGCOT.
  • Ameruhusu ma settler kutoka Zimbabwe huko IRINGA na MBEYA. wazungu wamepewa mashamba makubwa wanalima sana kilimo cha kisasa huko na wanafanya export ya mazao japo taarifa hazitolewi. Karibu wazawa wa Iringa na Mufindi watanyang'anywa wote ardhi yao, hivyo wanamfagilia.
  • Aliahidi 10% YA BAJETI ya taifa itakuwa ya wizara ya kilimo, sasa sijui ndivyo alivyofanya au vipi, kama ndivyo anastahili.
  • Anapashwa kutoa dola 10000 kila mwaka kama mchango wa kuimarisha utafiti wa kilimo katika Africa. Kama hajatoa hiyo hela ningemshauri asipokee hii tuzo au amfukuze waziri wa kilimo kwa kumuangusha
  • Ana mabilioni ya JK. Kama amewapa wakulima wadogowadogo na siyo akina mheshimiwa MTAWA tu pale ikulu. basi anastahili kupata tuzo.
  • Tumshangilie rais wetu... hurrayyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyy
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Wewe mkulima?
   
 10. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  swali halijibiwi kwa swali. kama huna jibu tulia
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nimekuuliza kwa sababu unaongea mambo kama idiot. Unauliza serikali ya awamu ya nne imefanya nini kwenye kilimo? either wewe ni idiot au hauna touch kabisa na kilimo, ndio maana nimekuuliza wewe ni mkulima? Sasa jijibu mwenyewe kundi lipi kati ya hayo mawili linakufaa...
   
 12. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Sitakuwa na muda wa kukueleza kila kitu hapa. Ila waweza kufunguka macho kwa kusikiliza mara kwa mara RTD na kuangalia TBC1. Kuna vipindi vizuri sana vya mafanikio yetu kwenye kila nyanja ikiwa ni pamoja na kilimo. Utashangaa kwamba tumepiga hatua sana na dunia inasifia maendeleo yetu hususan kwenye kubadilisha kilimo.
   
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo tunapopoteza umaana wa hizi TUZO. Kulingana na jina la hiyo tuzo pamoja na maana yake, si kweli kama Tanzania tumepiga hatua mbele katika kilimo chetu. Zaidi tumezidi kurudi nyuma, tumeuwa mazao yetu ya biashara karibu yote na mazao ya chakula (mfano mahindi toka mikoa mitano ya nyanda za juu kusini) tumezidi kuididimiza kutokana na mfumo mbaya wa utoaji ruzuku pamoja na miundo mbinu mibovu. Nchi haina maghala ya Taifa, bali tunategemea kuwakataza wakulima wasiuze mazao nje ya nchi ambapo wangeweza kujipatia faida kubwa. Kilimo kwanza hatujaweza kuitekeleza kwa vitendo. Labda kama ameshinda kutokana na policy nzuri wanazozisoma, mikakati ya kilimo kwanza pamoja na ruzuku ambazo bado hazijamnufaisha mkulima.
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Anastahl pongez na tuzo kwani alishawah kupanda ndege kwa mil.600 kodi ya Watanzania kwenda kukagua nyanya zilizopandwa kwenye ndoo
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Sep 6, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Kama Obama alivyotunukiwa tuzo ya amani ya Nobeli.
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Taarifa nzima ya Ikulu haikwambii taasisi hiyo ni ya wapi!!!

  I mean mpaka sasa nikiangalia taarifa ya Ikulu siwezi kujua kwamba taasisi hii ni ya walevi wa Uwanja wa Fisi au ya Umoja wa Mataifa.
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Thread zingine hizi kuzisoma ni kujitafutia kuichefuwa roho yako bure. huyu mkwele si bure.
   
 18. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #18
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Asante sana kwa kuwa na akili nzuri sana na kuona kuwa JK kapiga hatua kubwa sana kwenye kilimo wakati mwanzo wa mwaka huu watu wamelalamika njaa manyara, singida na kilimanjari hadi serikali ikaruhusu kuingizwa kkwa mchele bila ushuru toka nje. Hii njaa imetokea mwaka huu kwenye nchi ambayo rais wake amepewa tuzo kwa kuboresha kilimo mwaka huu. Asante mkuu una akili sana wewe
   
 19. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  kwani hawaruhusu rais aliyekwisha wahi kupata tuzo hiyo kujirudia tena mara ya pili? bora wangerudia kumpa rais Hifikepunye pohamba wa Namibia kuliko Jk ambaye amekaa kimya kule kibaigwa dodoma ambapo wakulima wa mahindi wamenyang'anywa mashamba yao na halmashauri ya wilaya ya kiteto kuanzia mwakani soko kuu la kimataifa kibaigwa litafungwa maana sehemu yote ya ardhi wamenyang'anywa .
   
 20. peri

  peri JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  JK amejitahidi kulinganisha na watangulizi wake wengi, japokuwa naamini anauwezo wa kufanya zaidi has kwenye suala la umwagiliaji bado anachangamoto nyingi.
  Ktk aliyofanya ni kutoa ruzuku ya mbegu na mbolea kwa wakulima jambo ambalo halikuwepo.
  Kusaidia upatikanaji wa materekta madogo kwa makubwa kwa wakulima jambo ambalo limeongeza uzalishaji wa chakula, kwasasa tunajitegemea kwa asilimia 113% katika uzalishaji wa chakula.

  Naamini JK anauwezo wa kufanya zaidi katika kilimo, hili alilofanya ni 50% ya anachoweza kufanya, akiamua anaweza kabisa. Ajitahidi kuimarisha umwagiliaji na kutoa elimu zaidi hasa ya kilimo cha kisasa, ktk hili anaweza kabisa kulitekkeleza. Naamini uwezo anao, akiamua anweza kabisa.

  Lowasa anaesema elimu kwanza hajakosea sana ila aangalie hatua iliyopigwa kwenye elimu, japokuwa haitoshi na kunachangamoto nyingi asiibeze na asisahau bila kilimo hata elimu ni ndoto, hauwezi kusoma ukiwa na njaa na hao wazazi wanaosomesha wanategemea kilimo ili kuweza kusomesha.

  Hongera JK ila iwe chachu ya kuongeza juhudi, ukiamua unaweza.
  Huo ni mtazamo wangu.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...