Mulhat Mpunga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 27,650
- 16,722
Nisaidie namba zao mkuuHabari zenu wakuu.
Nimevumilia sasa nimechoka aisee. Continental kama mmechoka basi tangazeni kufilisika na mfunge kurusha matangazo na kudanganya wateja.
Mlitoa ving'amuzi bila kadi. Baadae mkatangaza kuwa kadi ni bure. Ukifika kwenye ofisi zenu kadi mnauza 11,800/.
Hiyo inaweza kuwa sio ishu sana maana tunajua mnasaka hela.
Baada ya kutuuzia kadi siku hizi hapa Kibaigwa ndio hakuna kabisa matangazo yenu kwa antennae (external). Mwezi wa pili sasa mara muwe na channels mara hampo hewani.
Wakipigiwa simu hazipokelewi, emails hawajibh. Sasa sijui nini maana ya costomer care kwenu.
TCRA hawa jamaa sasa ishatosha. Maana sisi wenye ving'amuzi vyao badala ya kufurahia tunasikitika na kujutia kuwa navyo.
Naomba kuwasilisha.
Mi nnayo star times na nipo dar,anayekitaka aje pm nimpe,hawa jamaa ovyo kabisa,hamna bbc,cnn,citizen,sa wanataka tuangalie ma tangazo cha chama kwenye tv ya taifa!Najuta kugawa star times yangu.
Niligawa star times nikanunua continental, aisee hii kitu n majanga,
Channels
Well said mkuu,
Hata hii inatokea kila siku.
Kunasiku ntakipasua potelea mbali
mimi nashauri leseni sheria na taratibu zinazosimamia mambo haya ziangaliwe upya. Kuna thread nyingine inawahusu Azam pia. TCRA kuweni makini vinginevyo mtakuwa mnashirikiana nao ktk uovu huu. Simaanishi wote ila inawezekana kuna vishoka au wafanyakazi wanaofaidika na utoaji mbovu wa huduma hizo.Mimi nina uchungu nao hawa jamaa, najuta kununua king'amuzi chao
Ila mkuu umechunguza ukagundua kuwa yanayosemwa sio kweli au umeamua tu kutizama hili jambo kwa mtizamo huo? Kwahiyo watu wache kusema kuhusu king'amuzi A kwasababu tu jana kilisemwa king'amuzi B?Hii vita ya biashara inaenda kubaya sasa. Kila siku zinaibuka nyuzi za kuponda kisimbuzi kingine.
Jana nilisoma uzi wa kisimbuzi cha Azam, nadhani kesho nitasoma cha TING au Startimes au hata Easy au DStv.
Ni mwendo wa kuharibiana biashara tu hadi kieleweke.
Ova
Ila mkuu umechunguza ukagundua kuwa yanayosemwa sio kweli au umeamua tu kutizama hili jambo kwa mtizamo huo? Kwahiyo watu wache kusema kuhusu king'amuzi A kwasababu tu jana kilisemwa king'amuzi B?
Tutaendelea kuibua madudu ya kila king'amuzi (kulingana na kila mtu anvoguswa) bila kujali kama kuna kingine kimekwishajadiliwa na hapa hakuna vita ya kibiashara ni kutafuta mtosheko kwa mteja.
Kuna ubabaishaji mwingi kwenye hivi ving'amuzi na TCRA tusaidieni walaji kupata huduma bora.
Kama dikoda ni ya dish, haiwezi kutumia terestrial antenna. UsijisumbueNauliza kama naweza nikatumia antena nikadaka chanel bila shida kwa decoda iliyokuwa ya dish? antena bei gani? nipo mwanza meco.