Easymutant
R I P
- Jun 3, 2010
- 2,564
- 1,135
USINIONE NIKO KIMYA NASUBIRI UROPOKE.......Ndicho kilichomtokea Mkapa
Na Makongoro Nyerere alivyokuwa NCCR Mageuzi mwaka 1995 hakuwa mtoto wa Nyerere?. Ila wewe baba una kazi ngumu sana ya kudanyanya watu
Pasco pamoja na uandishi wake wa habari anataka kutuambia amesahau kuwa 1995 Makongoro aligombea ubunge kupitia NCCR tena wakati babayake akiwa hai . Vilevile hakumbuki pia kuwa Mwalimu aliposema "CCM siyo mama yangu" alikuwa ana maana gani?? Sasa hizo chembechembe za DNA za CCM sijui ziko wapi kwenye huo ukoo wa Nyerere.
Ndiyo hivyo tunavyodanganywa na wana CCM mpaka akina Mkapa pamoja na uzee wao bado wanadai wamezaliwa na kukulia CCM!! Sasa sijui akina Nchimbi watasemaje??
Wenzako wanasema mwl alikuwa amegoma kwenda kutibia, ila sasa wanajaribu kupindisha alikuwa anataka kwenda usa. KAma umesoma sredi yote kuna mjumbe amesema hivi.
"Mkapa alipoenda pale butiama na kumtaka mwl akatibie, mwl alimuuliza hivi, hivi wewe ulikuwa hujui mda wote huo mrefu naugua leo ndo unakuja?"
kweli hapa tumejaa wazushi, Je unafahamu kuwa Mwalimu ndiye aliyekwenda Washington DC kumwakilisha Mkapa enzi hizo kuongea na Wolfehson akiwa Rais wa Benki ya Dunia kuinusuru NBC na NMB? na Mwalimu alifanya hivyo? Na ndiye maana Leo bado zipo! Kama silo Mkapa kushirkiana na Mwalimu, leo hii mngebakiwa na Meridian Biao🙂 na mabenki ya nje tu!
kuhusu kubinafishwa kwa NBC na MNB Mkapa amegeuzwa Baniani, kiatu chake dawa🙂 na mumshukuru Mwalimu kuridhia kufana kazi hiyo kwa niaba ya Mkapa🙂 ushauri wa wakubwa ulikuwa tusiwe na mabenki yetu wenyewe!
Mtu anaweza kuzidiwa na kufa wakati wowote, lakini kama alienda akiwa anaongea lazima sababu ya kuzidiwa ghafla na kwa standard ya hospital likokwenda ungetegemea unafuu zaidi ya mauti. Kuna maswali ya msingi yanayo hitaji majibu zaidi ya kusema ni mapenzi ya MunguBinafsi siamini kama kifo cha Mwalimu kuna mkono wa Mkapa. No way!!! Ila naona kuna watu manapiga propanda tu humu. Wewe unasema alilazimishwa akatibiwe wakati VN anasema aliondoka akiwa na afya njema............ Sasa unataka kutuambia kuwa VN alikuwa hajui kuwa mzee wao alikuwa mgonjwa. Inawezekana kabisa wakati anaondoka alikuwa hajui tatizo lake............... mpaka ulipokwenda kule. Lakini kama ni kweli alishajua kuwa anaumwa then sioni ni kwa nini Mkapa alaumiwe kwa kumbembeleza akatibiwe.
Madaktari pia tunaomba watushauri hapa............ hivi hiyo cancer ya damu huwa inachukua muda gani kuua?? Maana kuna dada alikuwa anaumwa huo ugonjwa lakini baada ya kugunduka ilichukuwa zaidi ya miezi sita kufa. Kwa jinsi ugonjwa ulivyo lazima angekuwa alishadhoofika kabla ya kwenda huko!!
Kumbukumbu zangu zinaonyesha NMB ilizaliwa katika mchakato wa kutekeleza mpango wa kuiuza NBC, Kwahiyo sidhani kwamba unayoyaandika kuhusu NBC na NMB ni sahihi kiasi hicho. Nakumbuka kuanzishwa kwa NMB ilikuwa ni katika kuhakikisha kwamba nchi inabaki kuwa na benki yetu wenyewe badala ya kutegemea mabenki ya kigeni baada ya kukamilika kwa dili la kuuzwa kwa NBC.
Utapeli wa meridian biao bank unajulikana na sidhani kama una uhusiano wowote na kuuzwa kwa NBC.
Wa Kukaya ninayasikia sana,
CCM huwa wananishangaza sana, huwezi kuwatenganisha Mkapa, Rostam, Chenge, Mramba na Yona [wote wana sifa kuu moja ni mafisadi]. Sasa hizi tuhuma za kumuua Mwalimu zinazidi kumpaka matope Mkapa, sasa subiri kimya chake au povu litakavyomtoka atakapokuwa anajitetea ili aonekane ni Mr Clean!
Mtuhumiwa namba moja wa kuivuruga CCM ni Mkapa, halafu leo ndio anaitwa kwenda kupiga kampeni as if yeye ndo msafi kuliko wote. Mwanakijiji juzi alihoji, iweje CCM imvishe jezi namba 10 Bwana Mkapa ilihali anajulikana wazi kwamba ni fisadi mkuu na ushahidi upo kwamba alijigawia Kiwira na kupitisha madudu kibao zama za utawala wake?
Yale aliyoyasema Vicent Nyerere, yanatosha sana kwa sasa. Wao [CHADEMA] waendelee kujikita kwenye hoja na kero zinazogusa maisha ya kila ya wananchi wa Arumeru Mashariki. Huko Kaskazini ule mtaji wa udini haufanyi kazi na ndio maana Mkapa amekuja na mtaji wa matusi na hoja zisizo na mashiko. CHADEMA wakikaa vizuri wanaweza kushinda kirahisi sana.
Wana JF leo katika viwanja vinne tofauti vya kampeni Mbunge wa Musoma Mjini ambae ndie Meneja Kampeni wa Arumeru Mashariki (Vincent Nyerere) amemjibu Mkapa kuwa.
Aache unafiki wa siasa kwani ana Siri nzito juu yake ambayo ni muda muafaka sasa kwa Watanzania kuijua,na kudai kuwa yeye si mtoto wa Julius Nyerere kama anavyopotosha Mkapa ila ni wa Josephat Nyerere
Josephat na Julius ni mtu na Mdogo wake(kama hataki ajinyonge) huku akishangiliwa na umati mkubwa Sana uliohudhuria katika viwanja vya mkuytano uliofanyika Sing'si alimtaka Mkapa ajibu na aweke wazi juu ya Kifo cha baba wa Taifa aliyeondoka Butiama akiwa Mzima aliyekwenda tu kupima Afya na kurudi Mfu, huku umati ukipiga Mayowe kwa kushangilia, alitaka aweke wazi kilichomuua baba wa Taifa huku akimwaga Hadharani tofauti zilizojitokeza na Ugomvi kati yake na Mwalimu kilichopelekea Mkapa kuamua na kulazmisha mwalimu apelekwe London kutibiwa (kuuwawa) huku Nyuma akimyamazisha Daktari wa Mwalimu kwa kumpa Uwaziri ili asiseme kilichotokea.
Na alisema ilikuwaje Mkapa ataje Ugonjwa wa mwalimu ili hali Daktari wake yupo?alihoji, amemwaga vitu vingi ambavyo kwa kweli vitaleta Maswali Mengi juu ya wananchi wa Tanzania na dunia kwa ujumlaa...
Nikiripoti kutoka Uwanja wa Mapambano wa Arumeru ni mimi Mgosi Mgeni wenu wa JamiiForums
HOW STRANGE FOR THE 'EMINENT' AFRICAN LEADER MKAPA STRIPPING-OFF THE NYERERE CLAN BEDROOM-ISSUES ON A PUBLIC POLITICAL PODIUM IN ARUMERU MASHARIKI, WHO TO BLAME???
Ni nani kati ya viongozi wetu hapo nje ambaye ano uhakika kwa 100 % kwamba yeye ni MTOTO WA BABA YAKE huyo nayemuona hapo barazani kwao??
Hili la Rais Mstaafu kuanza kuchungulia unyumba na zawadi zake kwa wana-ukoo wa Mwalimu Nyerere na hata kwenda mbele zaidi kwa kuwasemea hadharani kwenye majukwaa ya siasa kwamba NI YUPI HASA NI UZAO WA YAI la kwa Chifu Burito hakika huu ni mshango wa mwaka.
Sote htunaa kumbukumbu zozote kama Mzee Mkapa amewahi kutawazwa na kabila la Kizanki kuwa mmoja kati ya wzee na msemji rasmi wa ule ukoo.
Na kama ni lazima sna awe msemaji waa ule ukoo basi aanze kwanza na zoezi zito zaidi kitifa kutuwekea wazi kilichomuua Mwalimu Nyerere. Uchungu wa Baba wa Taifa tunaujua WaTanzania tunaozulumiwa na CCM kila kona ya taifa hili.
Hata siku moja tusisikie mwana Ukoo wa Mwalimu Nyerere yeyote yule KAPATWA NA HOMA WALA KWIKWI baada ya taarifa hizi sasa kuwekwa hadharani kutokana na kubwatuka ovyo kwa Mzee Mkapa huku akidhani ni sifa.
Nasema siku zote wahenga hututaadharisha kwamba mtu UNAPOISHI KATIKA NYUMBA YA KIOO HATA SIKU MOJA USIPENDE SANA MCHEZO WA KURUSHA MAWE ovyo!!!
hivi NMB imeanzishwa lini?
maelezo ya kina atatna wapi?