Ni kweli kuna wale wageni wasiojua kweli bado wanavaa isivyo, ila nawe maelezo yako inaonekana unachungulia kabisa na sio kuepusha macho usione ubaya wake. Jifunze hata ukiwa nje ya kanisa kuepusha macho yako kuangalia maeneo uliyotaja hata kama kavaa vizuri. Mfano unaweza hitajika kumhudumia dada, mama au ndugu wa kike asiyekuwa na fahamu na nguo zimemtoka au zinamtoka sasa wewe kama unajenga hii hulka utapata matatizo bure, tazama pembeni kabisa hata wao wakiona wanapuuzwa utaona wanaacha wenyewe.Wana JF kuna jambo limekuwa likinisumbua sana kwa siku nyingi. Kila niendapo kanisani huwa najaribu kuangalia dada zetu wanavyovaa na huwa najiuuliza maswali mengi sana. Nashindwa kuelewa kama wanaenda kuuza sura kanisani au wanaenda kusali. Mfano mzuri ni kanisa la chuo kikuu cha Dsm. Hapa kuna mabinti wanaovaa vimini na wanakaa viti vya mbele. Wanapofika huwa wanajitahidi kubana miguu na kuvutavuta vijimini vyao lakini kipindi kinafika wanachia waziii wananika mapaja na viskintight vyao na wengine skintight hazionekani kwa maana watakuwa wameva bikini. Sasa naomba wenye uwezo wa kutoa onyo kwa hawa kina dada watusaidie. Nafikiri makanisa yote yangeweka sheria kwamba ni marufuku mwanamke kuingia kanisani na nguo zinazovuka magoti. Hebu angalia kina mama wa kiislamu wanapoenda msikitini wanajifunga mahijabu na makanga mengi tu. Kwa nini wakristu wasiwe na kanuni na taratibu za mavazi ya kuvaa siku za ibada. Waache kuwatia Ibilisi wachungaji na mapadre kwa kupanua mapaja yao kwenye viti vya mbele. Naomba tusaidiane kupambana na hili. Thanks in advance. May Almighty Father guide you and bless you so that you can come up with good and reasonable ideas on how to handle this damned matter.