Vimini makanisani

akina dada wa dizaini hii ni hatari sana kwani wanashawishi wenzao kuenda dhambi muhimu ni kutoa kanuni za kuzuia mavazi mabaya kanisani , nakumbuka kipindi fulani nikiwa mwanza kuna mapadri fulani wa parokia moja ya mjini walikuwa wana watoa nnje wale wote wanaovaa mavazi yasiokuwa ya heshima hata wavulana waliokuwa wanavaa milegezo walitolwa pia.
kanisani ni sehemu ya ibada na ni mahali patakatifu lazima paheshimiwe ni sehemu ya ibada,
ila duh juzi nimemuona na chenge nae alikuwa church tena akishiriki karamu ya bwana kwenye mazishi ya askofu mayala mhhh sijui ningekuwa paroko ningemtoa nduki akatubu kwanza.
 
watanzania tumezidi kulalamika, mbona nchi za ughaibuni watu wanaenda kanisani na vimini au short pants watu hawalalamiki? Kwani kanisani ulienda kumuomba Mungu au kuangalia watu wamevaaje? Au nyie wanaume waafrika mpo tofauti na wanaume wa huko ughaibuni, au nyie ndio mnajua kuhisi sana mnapoona msichana kavaaa nguo fupi?
We Muteso kama unaenda kanisani nenda kasali, usiende kuangalia wasichana wamevaaje. Wasichana wengine wanapovaa nguo fupi sio kwamba ili kuwavutia wanaume, ila mwingine nguo fupi ndio anayopenda.
Mungu anaangalia moyo na sio mavazi, kinachotakiwa ni kuwa na moyo msafi mbele zake.
Pretty hao wa ughaibuni hawako sahihi kwa kila kitu.Hivyo basi siyo watu wakujilinganisha nao;kwasababu na wao wanakosea pia kama wewe unavyokosea halafu unataka kwenda nao sawa wakati na wao wanachemsha/kutokota kabisa.Naomba tuache kuwa wanafiki,sidhani kama kuna mahali katika maandiko na maadili katika sehemu husika yanakubaliana na hilo vazi!
 
Pole sana ndugu yangu,iaelekea kwa kiasi fulani hofu ya Mungu bado ipo ndani yako.Hongera.

Naomba niseme kwamba mambo hayo ya akina dada zetu kuvaa nguo zisizofaa hayapo hapo Chuo Kikuu tu,yako kwenye makanisa yote.Hiyo ni mbinu ya shetani kuwafanya waumini wasiweze ku-concentrate kusikiliza neno la Mungu,na ni effort ya muda mrefu sana ya ibilisi kupeleka watu kuzimu.Lakini pia wanatumia mbinu zingine nyingi kama watoto kulia ovyo wakati wa ibada,kutembea tembea huku wakiwa wamevaa viatu vinavyopiga kelele,kuwaletea watu usingizi usio eleweka wakati wa ibada n.k.,ili mradi ku-distract attention.Wengine kati ya hawa wanatumiwa na shetani bila kujua,lakini wengine wako kwenye ajira kabisa huku wakijua kwa uhakika kabisa wanalo lifanya!It's a pity kwamba wengi hatujui upumbavu huu.

Kuwakemea hawa haitasaidia sana, kwa vile tutakacho kuwa tunafanya ni kuwafanya wautawale mwili kwa ukali.Pia mbinu zinazotumiwa ni za kishirikina mno ambazo sisi kimwili hatuwezi kuzikabili,bila kuwa na nguvu za Mungu.Kwa hiyo ni wazi kuwa tunahitaji nguvu za Mungu.Hata hivyo nia ya kuacha tabia hiyo inatakiwa itoke moyoni.Kwa bahati mbaya viongozi wa dini ambao ndio walio pashwa kuwapa waumini wao mafundisho ambayo yangeweza kuwafanya wasiingie kwenye mitego na vishawishi vya shetani, nao wametekwa na shetani,kwa hiyo hawana uwezo huo tena.

Ninalo weza kukushauri ni kwamba ikiwa unamtafuta Kristo Yesu kweli na hujatawaliwa na mifumo hii ya kishetani ya dini,tafuta sehemu ambayo kutoka moyoni mwako unaona Yesu wa kweli ana abudiwa halafu abudu hapo.Naomba uwe makini sana katika jambo hili kwa vile siku hizi ni siku za hatari sana.Unaye dhani ndiye kumbe siye.Katika hili una takiwa uwe unafahamu maandiko vizuri ili uweze kuchambua chuya na mchele.Kama huna hakika ya mahali panapofaa tafuta mtu unaye unaamini anaweza kukusaidia akusaidie.Usione aibu,hata kama una wadhifa mkubwa kiasi gani jambo hili ni la muhimu sana na la msingi katika maisha yako.Tuko jioni sana,Yesu anakuja kulichukua kanisa lake!

Wana JF kuna jambo limekuwa likinisumbua sana kwa siku nyingi. Kila niendapo kanisani huwa najaribu kuangalia dada zetu wanavyovaa na huwa najiuuliza maswali mengi sana. Nashindwa kuelewa kama wanaenda kuuza sura kanisani au wanaenda kusali. Mfano mzuri ni kanisa la chuo kikuu cha Dsm. Hapa kuna mabinti wanaovaa vimini na wanakaa viti vya mbele. Wanapofika huwa wanajitahidi kubana miguu na kuvutavuta vijimini vyao lakini kipindi kinafika wanachia waziii wananika mapaja na viskintight vyao na wengine skintight hazionekani kwa maana watakuwa wameva bikini. Sasa naomba wenye uwezo wa kutoa onyo kwa hawa kina dada watusaidie. Nafikiri makanisa yote yangeweka sheria kwamba ni marufuku mwanamke kuingia kanisani na nguo zinazovuka magoti. Hebu angalia kina mama wa kiislamu wanapoenda msikitini wanajifunga mahijabu na makanga mengi tu. Kwa nini wakristu wasiwe na kanuni na taratibu za mavazi ya kuvaa siku za ibada. Waache kuwatia Ibilisi wachungaji na mapadre kwa kupanua mapaja yao kwenye viti vya mbele. Naomba tusaidiane kupambana na hili. Thanks in advance. May Almighty Father guide you and bless you so that you can come up with good and reasonable ideas on how to handle this damned matter.
 
You all have spiritual problems. Those who truly believe in GOD, have the spirit and power to withstand all the temptations of this world. MATESO, I pray for you that GOD gives you all that you need to defy the temptation triggered by the kind of dresses (skirts) your sisters in Christ put on. Moreover, you need not to take time soliciting views from other people. What you need to do as a Christian is to faithfully go straightforward to them and sincerely tell what you think they need to do as daughters of GOD. I think that's what GOD told us. That is, when you see you relative, friend, or any other person doing things which does not praise the His name, don't hesitate, go and tell him or her but also pray for him/her. However, you need first to pray so that GOD gives you His Holy spirit to guide you in the entire exercise.

GOD blesses you as you prepare to take that step. AMEN.
 
GOD blesses you as you prepare to take that step. AMEN
 
Wana JF kuna jambo limekuwa likinisumbua sana kwa siku nyingi. Kila niendapo kanisani huwa najaribu kuangalia dada zetu wanavyovaa na huwa najiuuliza maswali mengi sana. Nashindwa kuelewa kama wanaenda kuuza sura kanisani au wanaenda kusali. Mfano mzuri ni kanisa la chuo kikuu cha Dsm. Hapa kuna mabinti wanaovaa vimini na wanakaa viti vya mbele. Wanapofika huwa wanajitahidi kubana miguu na kuvutavuta vijimini vyao lakini kipindi kinafika wanachia waziii wananika mapaja na viskintight vyao na wengine skintight hazionekani kwa maana watakuwa wameva bikini. Sasa naomba wenye uwezo wa kutoa onyo kwa hawa kina dada watusaidie. Nafikiri makanisa yote yangeweka sheria kwamba ni marufuku mwanamke kuingia kanisani na nguo zinazovuka magoti. Hebu angalia kina mama wa kiislamu wanapoenda msikitini wanajifunga mahijabu na makanga mengi tu. Kwa nini wakristu wasiwe na kanuni na taratibu za mavazi ya kuvaa siku za ibada. Waache kuwatia Ibilisi wachungaji na mapadre kwa kupanua mapaja yao kwenye viti vya mbele. Naomba tusaidiane kupambana na hili. Thanks in advance. May Almighty Father guide you and bless you so that you can come up with good and reasonable ideas on how to handle this damned matter.

BAADA YA KUIPITIA HII THREAD NIMEONA WAZI HAWA NDUGU ZETU JINSI WALIVYO WAJINGA MWENZIWAO AMELEZA MADHIIFU AMBAYO YAPO WAZI HATA WOTE WANAYASHUHUDIA KAMA SIO JAMBO ZURI LAKINI BAAADA YA KUTUOA MCHANGO JINSI GANI YA KULIONDOA TATIZO HILO ETI WANAMPONDA HUYU MWENZIWAO AMBAE AMELISEMA TATIZO HILO NADHANI WAO WANALISAPOTI NA PIA NIKUONYESHA HII DINI SASA HAINA TENA WAUMINI BAADAE WATAENDA HATA NA CHUPI NA WATADAI MUNGU HAAANGALII CHUPI.

NDUGU KARIBU KWENYE UISLAM HUTAYAKUTA HAYO DINI AMBAYO MUNGU AMEIWEKEA MIPAKA KATIKA KILA NYANJA.

QURAN: SURA 2.
135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina. ***
136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake. ***

QURAN: SURA TU NUR.
31. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa. ***

AL-AHZAB.
59. Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. </B>***
 
ukiona wadada wanakuja kanisani na vimini nadhani ndio sehemu nzuri Mungu kuongea nao kupitia mafundisho mbalimbali ya watumishi wake. Kanisani ni sehemu nzuri kwa wote wenye matatizo mbalimbali kumwomba Mungu wao awasaidie na wenye furaha na raha kumshukuru na kuendelea kumtukuza kwa mema na mazuri yote anayowatendea. Ukiona makahaba, walezi, wazinzi, vibaka wakubwa na wadogo, wafuta marijuana wanaingia kanisani ni jambo lakushukuru sana....ndio sehemu yakupata tiba ya kiroho na kimwili pia. Mwenye afya hana haja yakumwona daktari ila mwenye udhaifu...
Mafundisho ya kanisani yakiwaingia vizuri then watajua kwamba matendo, mavazi yao ni staha kwa eneo la ibada au la?
Zaidi sana endelea kumwomba Mungu akisaidie kizazi hiki cha nyoka...na ikiwezekana ongea nao au wazee wa kanisa kwa hekima jinsi yakuwasaidia dada zetu hasa sehemu za ibada.
In His Service
 
Suala la kusimamia mavazi ya heshima halikwepeki na nadhani lina umuhimu wa pekee kwamba kama mtu anashindwa kuwa mkweli na nafsi yake akiwa nyumba ya ibada anawezaje kuwa mwaminifu sehemu ya kiza?

Ni muhimu kwa makanisa kuweka bylaws ambazo zipo systematic na kuwa enforced kuhakikisha kuwa waumini hawaifanyi nyumba ya ibada kuwa sehemu ya unajisi. Kuwepo na askari wa kike na kiume kusimamia kuwa mavazi yanakuwa na heshima na adabu yasiyowakwaza wengine, kwa pande zote mbili.
 
Kwenye maofisi ya serikali vimini ni marufuku. Inashangaza kuona watu wanashabikia ati ni sawa vimini kuvaliwa makanisani!
 
Mbona Maaskofu, mapadri na Masister wanavaa vizuri.

Ni muhimu sana kwa kanisa kuliangalia hilo kwa ukali zaidi. Kwani kanisani watu wanakenda kuomba mungu na sio kufanya biashara ya kutamanishana kingono.

Mola awalaani wale wote wanaokwenda kwenye nyumba za ibada kwa nia ya kutamanisha wenzao kishetani
 
Ni kweli maneno yako, naongezea hapo... Ukitazama na kutamani, umezini...!

Lakini vipi yule mwenye kumtamanisha mwingine... mpaka yule mtazamaji akajikuta akitamani kwa kule kutamanishwa na mtamanishaji!?

Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa
mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
1Tim 2:9

Hakuna anayemtamanisha mwenzake, kiini cha tamaa kipo na hutoka ndani ya atamaniye. tamaa huletwa na fikra na hisia na malengo ya mtu. Wapo wanaume wengine ambao huwatamani wanawake wa kiislamu kwa mavazi yao ya baibui. Mwanamume anajenga hisi kwa kuutazama mwonekano wa mwanamke mwenye kuvaa baibui na kufikiria atakachokuwa anakiona wakati anapoitoa hiyo baibui. Fikra zake zinamwelekeza kuwa kitu kilichofichwa ndani ya hilo vazi jeusi lazima kitakuwa kizuri na chenye thamani kubwa. Baada ya hapo anapata matamanio na kuweka lengo la kumtafuta na kumnasa mhusika.

Lakini ikiwa wakati unatoka nyumbani kwako mawazo na fikra zako umezielekeza na kuzikita kwenye Ibada ya Misa. Utakapokuwa ndani ya Kanisa au nyumba nyingine ya Ibada hutaviona vimini, Skintaiti, bikini wala mapaja. Hebu fikiria watu wanavyoweza kuwa na mawazo kiasi cha kutojuwa kuwa anavuka barabara au mtu unamsalimia lakini hakusikii. Vivyo hivyo tukizamisha fikra zetu kwenye kuwasiliana na mungu hatutakwazika kamwe
 
Acha nginjera hizo. Kama mwanadamu uliekamilika haswa huna matatizo basi utakuwa na matamanio. na matamanio siku zote yana nguvu sana kiasi ni watu wachache sana waliokuwa na uwezo wa kuyazuia.

Rejea vitabu vya Dini. Aliyeeza kushinda matamanio ni Nabii Yusuf alipotamaniwa na mke wa Mfalme.

sasa tujiulize kuna akina Yusuf angapi hivi sasa? watu hawapigiwi wanacheza.

Tukemee ka nguvu zote kuvaa vimini kanisani . tuvae vzr kama wanavofanya viongozi wetu wa dini na masister.
 
Hapana, husiwaombee laana kwa MUNGU ila waombee wabadilike na kufanya yale yaliyo mema kwa MUNGU na binadamu wenzao
 
Tatizo la wa TZ hatuna uelewa wa kujua kipi kifanyike wapi na kwa wakati gani,ndio maana mavazi ya arusini yanavaliwa ofisini na ya Beach kanisani.Hao wadada wanapaswa kuelimishwa kwanza kabla ya kulaumiwa.
Vilevile kanisani sio mahali pa watu watakatifu pekee,hata shetani huwa anaenda kanisani(soma kitabu cha Ayubu katika Biblia).Hivyo wakienda kanisani ndipo mahali pekee pa kubadilika baada ya kuhubiriwa injili na kuombewa.
Mfano mzuri ni pale kwa kakobe.wanawake wote wanatakiwa wavae vilemba kichwani,lakini ukienda bila kilemba haufukuzwi ila wewe mwenyewe kama unataka kusali hilo kanisa utabadilika tu baada ya muda
 
Rejea vitabu vya Dini. Aliyeeza kushinda matamanio ni Nabii Yusuf alipotamaniwa na mke wa Mfalme.

sasa tujiulize kuna akina Yusuf angapi hivi sasa? watu hawapigiwi wanacheza.
QUOTE]
Blue: Aisee sidhani kama siku hizi kuna akina Yusuph
Red: Teh teh teh teh teh teh! Watu wanadundika tu, kazi kweli kweli
 
Suala siyo makwazo tu ya huo uvaaji. Suala hapa ni kwamba uvaaji wa namna hiyo haustahili Kanisani kwa sababu Kanisa ni NYUMBA ya Mungu. Watu wanaoenda hapo lazima waende kwa ADABU na UCHAJI WA MUNGU kwani kanisa ni nyumba takatifu ya Mungu. Siyo kilabu cha pombe au ukumbi wa senema. Kumbe mtu anayeingia kaniasani kavaa ovyo anamkosea Mungu kwa nafasi ya kwanza kabisa.

Kwa nafasi ya pili, labda ndiyo yanakuja hayo makwazo kwa watu wenye kuangaza macho kwa mabinti, jambo ambalo naona wengi mmemkaba koo mleta mada.

Kumbe tuwe tunawaangalia au hatuwaangalii hao wadada waliovaa vibaya, ijulikane kuwa wanafanya utovu wa nidhamu mbele ya Mungu. Kuvaa nguo fupi kanisani ni machukizo kwa Mungu aliye mtakatifu. Please, tuiheshimu nyumba yake.
wewe ndo una-set standards za nidhamu? kama mkware mkware tu. nani kasema kuangalia mapaja kanisani ni dhambi zaidi ya kuangalia barabarani au kwenye daladala au darasani in that matter?

mdhambi ni mvaaji au muangaliaji? na ukiangalia unatenda kosa? au ukitamani ndo kosa?
 
jumapili ilopita nilipata nafasi ya kusali ibada yangu katika kanisa moja la mkoa wa Tanga, wale jamaa wameenda mbali zaidi kwani wameanzisha utaratibu maalum wa kuweka pale nje khanga nyingi sana ambazo huwavika wale wanawake wote wanaovaa vimini.waumini wameuzoea huo utaratibu,wameshaona ni wa kawaida.May be this can be a remedy!
 
Unaenda kuangalia wanawake kanisa la UDSM kwani ile TBS siku hizi imekufa? Pale ATB kwa nyuma,unatazama kule chini library, kwa mbele kuna kanjia kakuelekea kule faculty of law, kwa huku kuna pahali wanapanda ngazi wanakuja ARD etc, kwa kule kuna kanjia kanaelekea darajani then Daruso/posta. Kakae TBS uoshe macho mpaka uchoke sio kanisani bana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom