We Mateso! Sentensi yako umeianza vibaya, ukienda kanisani unakwenda kusali na kumwomba Mungu, sasa wewe unapata muda wapi wa kuangalia wasichana? Hayo mambo ya Macho hayana pazia ni excuse ya kizamani sana. Kama nia yako ni kusali huwezi kuangalia angalia wasichana, unless wewe pia unakwenda kuangalia madada.
Kuhusu wakina dada kuvaa nguo fupi mie naomba tu kusema kwamba, kila vazi lina mahali pake. Beach, disco, kazini, kanisani, etc. Kila mahali kuna mavazi rasmi, basi tujitahidi kuvaa kuendana na mazingira tunayokuwemo
Wewe kama unalifahamu kanisa la UDSM kuna pande huwa zinakaa kwa kutizamana sasa kama binti atakaa mbele na kimini chake na wewe unaangalia upnde huo ukamwona huko ni kuchungulia? Be reasonable.
Hakuna anayemtamanisha mwenzake, kiini cha tamaa kipo na hutoka ndani ya atamaniye. tamaa huletwa na fikra na hisia na malengo ya mtu. Wapo wanaume wengine ambao huwatamani wanawake wa kiislamu kwa mavazi yao ya baibui. Mwanamume anajenga hisi kwa kuutazama mwonekano wa mwanamke mwenye kuvaa baibui na kufikiria atakachokuwa anakiona wakati anapoitoa hiyo baibui. Fikra zake zinamwelekeza kuwa kitu kilichofichwa ndani ya hilo vazi jeusi lazima kitakuwa kizuri na chenye thamani kubwa. Baada ya hapo anapata matamanio na kuweka lengo la kumtafuta na kumnasa mhusika.
Lakini ikiwa wakati unatoka nyumbani kwako mawazo na fikra zako umezielekeza na kuzikita kwenye Ibada ya Misa. Utakapokuwa ndani ya Kanisa au nyumba nyingine ya Ibada hutaviona vimini, Skintaiti, bikini wala mapaja. Hebu fikiria watu wanavyoweza kuwa na mawazo kiasi cha kutojuwa kuwa anavuka barabara au mtu unamsalimia lakini hakusikii. Vivyo hivyo tukizamisha fikra zetu kwenye kuwasiliana na mungu hatutakwazika kamwe
Na Bakora zitembee!!! Kufukuzwa haitoshi.Hii ni tabia mbaya na lazima viongozi wetu wa dini na waumini wakemee na ikiwezekana wanaovaa vimini makanisani wafukuzwe.