Vijana wa Matolori Ubungo Bus Terminal na 'vipaseli'

Vijana wa Matolori Ubungo Bus Terminal na 'vipaseli'

Thegame

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
2,273
Reaction score
2,402
Jana nilikuwa nasafiri kwa bus kwenda Mkoani. Wakati nasubiria muda wa kuondoka, nikawa nabadilishana mawazo na baadhi ya vijana wanaobeba Mizigo kwa matolori.

Mara likaingia basi la Meridian kutoka Mkoani Arusha, abiria wakashuka akiwemo binti mmoja wa miaka Kati ya 17-18 hivi. Inavyoonekana binti aliahidiana na mtu aje ampokee pale ubungo, akawa anamsubiri. Hata baada ya lisaa limoja kupita, yule binti bado alikuwa anamsubiri mwenyeji wake aje amchukue bila mafanikio. Ndipo kijana mmoja akaniambia " Bro leo naweza kupata kipaseli kipya" nikamuomba anifafanulie alimaanisha nini?

Akasema, ma binti wengi mikoani huwa wanapata marafiki wa kiume wa Dar kupitia Facebook!Hawa jamaa wana waita ma binti hao waje Dar! Wakikubaliana jamaa anamtumia nauri binti ya kumleta hadi ubungo huku akimuahidi kumpokea ubungo.

Lakini wakati basi linafika ubungo nakushusha abiria, jamaa hawajitokezi fasta mpaka wamthaminishe kwanza binti kama analipa. Kwahiyo hapo maswali ya umevaaje, uko eneo gani? Huwa ya kutosha.

Jamaa akimuona binti atamcheki kama analipa atamfuata na kumpokea.

Shida inakuja kwa ma binti ambao hawajafikia viwango vya hao wanaothaminisha! Jamaa wanawazimia simu nakupotea kimya kimya na kuwatelekeza ma binti wa watu hapo ubungo terminal.

Hao ma binti waliotelekezwa ambao hata nauri ya kurudia makwao hawana, ndio huwa ni vipaseli ambavyo vijana wa matolori hujisevia bila hata kutongoza.

"Hapa bro kwa mwezi tupata paseli si chini ya tano! Nikashangaa.

Jamani mikoani huko wapeni tahadhari mabinti wenu na marafiki wa mitandaoni, wengi ni shida tu! Wataishia kuwa vipaseli ubungo.
 
asante kwa taarifa ziwafikie wahusika popote walipo
 
  • Thanks
Reactions: rpg
Na virusi wanapata vingapi kwa mwezi

Mkuu nadhani tatizo la maambukizi ni hatari zaidi kwa hao mabinti! Wengi wao ni innocent poor girls from the villages where HIV infections are too low!
 
Na virusi wanapata vingapi kwa mwezi


Ile kinga tunayoshauriwa kutumia haifanyi kazi siku hizi?
Dunia itakuwa sehemu salama ya kuishi kama kila mmoja akijua anawajibu katika kufikia lengo hilo. Unatuma nauli 'then' unamkimbia mtoto wa watu matokeo yake anabakwa au kubebeshwa ujauzito. Siku ukiona taarifa ya habari binti katelekeza watoto kwa masista bovu linakutoka, ''Oooh wazazi wa leo hawana upendo''.
 
asee itabidi niungane nao katika hiyo kazi, kumbe kuna papuch za bure huko!!!
 
lkn na ww binti jitu hulijui linakutumia nauli unapanda basi unakuja tu......hujihurumii wala nini......hufikirii mbele
 
Mkuu nadhani tatizo la maambukizi ni hatari zaidi kwa hao mabinti! Wengi wao ni innocent poor girls from the villages where HIV infections are too low!

Kweli kabisa mkuu Mungu atunusuru kwa kweli
 
nakumbuka enzi hizo kabla ya facebook kulikua na mchezo wa kubahatisha namba..
 
Ujinga mwingine ni zaidi ya ujinga wenyewe utatumiwaje pesa ya nauli kwenda kwa mtu mliyekutana mtandaoni kupenda vya bure kunaumiza
 
Back
Top Bottom