Waziri wa Tamisemi Mhe. Bashungwa leo amesisitiza mabasi yote yaendayo Mikoani pamoja na nchi jirani lazima yapakie na kushushia abiria katika kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wadau wa usafirishaji.
Ni vyema waziri kalizungumzia hilo maana hali ilipo kuwa imefikia ilikuwa ni vurugu yaani kama vile hakuna wasimamizi wa sheria au hakuna viongozi maana kila basi illikuwa inaamua ikapakie abiria wapi na ikashushie wapi!! askari wapo! wanaangalia jinsi watu wanavyo vunja sheria!!
Hapana, lazima kituo chetu cha Magufuli kitumiwe kama ilivyo kusudiwa, hivyo ni vyema wenye mamlaka wakasimamia hilo.
===
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa siku saba kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kukutana na LATRA, Wadau na Wamiliki wa Mabasi kuweka uratibu mzuri wa kusimamia maelekezo ya Serikali kwa mabasi yote kushusha na kupakia abiria ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.
Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Mei 30, 2022 wakati akikagua mradi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Magufuli Bus Terminal) kilichopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Amesema, Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 50 kujenga kituo hicho, hivyo Serikali haitakubaliana na watu ambao hawazingatii utaratibu uliowekwa katika kituo hicho.
“Ninafahamu kuwa Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla ameshapokea changamoto ya Mabasi kutoingia ndani ya kituo hiki cha Magufuli na mimi nimekuta changamoto bado iko pale pale, sasa kwa sababu ameshanza kulifanyia kazi nampa siku saba awe amekutana na LATRA pamoja na wadu wa mabasi (TABOA) kuangalia utaratibu wa mabasi yote kuingia ndani ya kituo kushusha na kupakia abiria,”amesema Bashungwa.
Pia Mheshimiwa Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James kuweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara na Wadau wa Kituo cha Magufuli, Mawakala na Makalani ili kusikiza na kuweka utaratibu wa kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika kituo hicho na kuzifanyia kazi kwa ushirikiano.

Waziri Bashungwa atoa siku saba Stendi Kuu ya Magufuli-Dar