Utapeli unaofanywa na baadhi ya "maajenti" wasio waaminifu pale Magufuli Bus Terminal ukomeshwe!

Bull Bucka

Member
Oct 5, 2023
34
46
Pamoja na kwamba Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kimetengeneza ajira kwa watu wengi, lakini kuna jambo moja linaloendelea pale na linaonekana kufumbiwa macho na mamlaka husika. Jambo hilo ni utapeli.

Juzi nikiwa kwenye pitapita zangu, nikaona watu wamemzingira mama mmoja wa makamu. Mama huyo alikuwa akiangua kilio kwamba yeye alikuwa ameteremka kwenye daladala za Kinyerezi na wakati yupo kwenye daraja la juu la watembea kwa miguu linalounganisha upande wa Kituo cha Daladala cha Mbezi Louis na Magufuli Bus Terminal, alikutana na “ajenti” wa mabasi ya mikoani.

“Ajenti” yule alimshawishi mama yule na kumuuzia tiketi ya kwenda Kondoa na akamuandikia na kukabidhi kisha alipoingia ndani ya stendi akamwambia asubiri kwenye moja ya mabenchi mpaka basi lake litakapofika dakika ishirini baadaye.

Kutokea hapo hakumuona tena bwana yule. Na tiketi aliyokuwa amepewa haikuwa halali. Kwanza haikuwa tiketi halali ya gari aliloahidiwa, na pili gari hilo halifanyi safari za huko alipokuwa anaenda. Basi mama yule akawa amepoteza fedha zake.

Lakini hiyo haikuwa mara ya kwanza kusikia kuhusu watu kutapeliwa pale Magufuli. Kuna taarifa nyingi kuwa wale wanaojiita “maajenti” baadhi yao wako pale kwaajili ya kuchungulia fursa za kuwatapeli abiria wanaoenda mikoani. Inaelezwa kuwa kuna watu wengi safari zao zimekomea pale baada ya “kupigwa” na matapeli.

Ni sawa kwamba kinachoendelea kinatoa ajira kwa watu wengi, lakini kunaweza kuwa na utaratibu mzuri tu. Ni muhimu hao “maajenti” kama wanatambulika na makampuni ya usafirishaji wavae vitambulisho au sare. Kuna baadhi huwa wanavaa hivyo, lakini wengi wao hawana sare wala vitambulisho. Wanauza maneno tu. Tena wanawadaka wateja wanaposhuka tu kwenye daladala. Yaani kabla hujashuka unaona watu wamejaa mlangoni wanakuwania kama mpira.

Mamlaka ziliangalie hili na ziweke msimamo thabiti dhidi ya jambo hilo. Kila ajenti awe na kitambulisho na sare fulani inayomtambulisha, au namba kwenye kizibao au utaratibu mwingine wowote ule utakaofanya hawa watu watambulike kirahisi.

Lakini pia, hata wale maajenti ambao wanatambulika basi wasaidie kuwatambua wale wanaowaharibia kazi kazi yao.
 
Hiki kituo kina malalamiko mengi

Screenshot_20231011-063251_Chrome.jpg
 
Hakuna cha ajira wala nini, kwanza ajira ya Maneno Asilimia kubwa ni utapeli, Kapige kazi za mikono huko.
Kuna Mstari mwembamba sana unamtenganisha Agent na Tapeli.

Kitu chochote ukiweka exeption ndio unaanza kuharibu, hakuna cha Agent wala dalali, nani karne hii ashindwe kusafiri kisa hajaona basi la aendako? Wahudumu wa Basi wa 3 wanatosha.

Ule utitiri pale ni kelo, Pale pamejaa wizi. Asipokuibia nauli yote, atakuibia sehemu ya nauli. Yaani mtu kirahisi tuu nitoke huko kwa tumbo niende pale ndio unajifanya kunielekeza gari? Kwamba bila wewe sisafiri?

Hawa wapuuzi tuna waendekeza, ingekua tunawakazia wangeondoka wenyewe.
 
Ukiwaita maajenti umewapa cheo kikubwa sana,wale wanaitwa masalange ukizubaa hadi mabegi wanakuibia. Kwa upande wangu naona tuzidi kupeana elimu ya kufika direct ofisini kukata tiketi na sio zaidi ya hapo. Ukiona mtu anajifanya kukuonea huruma na hakujui tambua kuwa kifuatacho ITV.
 
Mamlaka ziliangalie hili na ziweke msimamo thabiti dhidi ya jambo hilo. Kila ajenti awe na kitambulisho na sare fulani inayomtambulisha, au namba kwenye kizibao au utaratibu mwingine wowote ule utakaofanya hawa watu watambulike kirahisi.

Lakini pia, hata wale maajenti ambao wanatambulika basi wasaidie kuwatambua wale wanaowaharibia kazi kazi yao.
Kinachotakiwa ni elimu kwa uma,

Ticket ifuatwe sehemu stahiki.
 
Uongozi wa Magufuli Terminal wekeni bango kubwa kuwa tiketi za mabasi zinakatwa ghorofa ya 2; Abiria wajue kuwa ofisi za mabasi zipo ghorofa ya 2 na tiketi ndio zinapatikana huko.

Bango liwe kubwa na liwepo chini na pia kwenye ukuta juu kama lilivyo la KAIRUKI hospital nk

Maana ya uwepo wa uongozi ni pamoja na kuhakikisha usalama wa abiria watarajiwao, sio kukusanya mapato tu.
 
Mkuu ndio shida ya kuishi in a pithole country, ticket ilitakiwa ukate popote anapotaka msafiri, smart phone pia zingekua na uwezo huo, supermarkets, wakala wa M pesa hawa wote wangekua na uwezo huo, ila safari hii bado sana maana hata life books hatuna kama watanzania, nchi ipo kama choo cha public,unaingia na kutoka utakavyo, tuanze upya kutoa ID za kidigitari ili zirahisishe maisha yetu, tuanzia na birth certificate kwa watoto wote wanaozaliwa,mzazi asiruhusiwe kurudi nyumbani bila ya birth certificate yenye ID number (number hii itaishi nayo na kufa nayo)
 
Pamoja na kwamba Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kimetengeneza ajira kwa watu wengi, lakini kuna jambo moja linaloendelea pale na linaonekana kufumbiwa macho na mamlaka husika. Jambo hilo ni utapeli.

Juzi nikiwa kwenye pitapita zangu, nikaona watu wamemzingira mama mmoja wa makamu. Mama huyo alikuwa akiangua kilio kwamba yeye alikuwa ameteremka kwenye daladala za Kinyerezi na wakati yupo kwenye daraja la juu la watembea kwa miguu linalounganisha upande wa Kituo cha Daladala cha Mbezi Louis na Magufuli Bus Terminal, alikutana na “ajenti” wa mabasi ya mikoani.

“Ajenti” yule alimshawishi mama yule na kumuuzia tiketi ya kwenda Kondoa na akamuandikia na kukabidhi kisha alipoingia ndani ya stendi akamwambia asubiri kwenye moja ya mabenchi mpaka basi lake litakapofika dakika ishirini baadaye.

Kutokea hapo hakumuona tena bwana yule. Na tiketi aliyokuwa amepewa haikuwa halali. Kwanza haikuwa tiketi halali ya gari aliloahidiwa, na pili gari hilo halifanyi safari za huko alipokuwa anaenda. Basi mama yule akawa amepoteza fedha zake.

Lakini hiyo haikuwa mara ya kwanza kusikia kuhusu watu kutapeliwa pale Magufuli. Kuna taarifa nyingi kuwa wale wanaojiita “maajenti” baadhi yao wako pale kwaajili ya kuchungulia fursa za kuwatapeli abiria wanaoenda mikoani. Inaelezwa kuwa kuna watu wengi safari zao zimekomea pale baada ya “kupigwa” na matapeli.

Ni sawa kwamba kinachoendelea kinatoa ajira kwa watu wengi, lakini kunaweza kuwa na utaratibu mzuri tu. Ni muhimu hao “maajenti” kama wanatambulika na makampuni ya usafirishaji wavae vitambulisho au sare. Kuna baadhi huwa wanavaa hivyo, lakini wengi wao hawana sare wala vitambulisho. Wanauza maneno tu. Tena wanawadaka wateja wanaposhuka tu kwenye daladala. Yaani kabla hujashuka unaona watu wamejaa mlangoni wanakuwania kama mpira.

Mamlaka ziliangalie hili na ziweke msimamo thabiti dhidi ya jambo hilo. Kila ajenti awe na kitambulisho na sare fulani inayomtambulisha, au namba kwenye kizibao au utaratibu mwingine wowote ule utakaofanya hawa watu watambulike kirahisi.

Lakini pia, hata wale maajenti ambao wanatambulika basi wasaidie kuwatambua wale wanaowaharibia kazi kazi yao.
Aisee matapeli ndio wale wale madalali wa tiketi na wanajuana.

Mamlaka ichukue hatua watu wote wanaofanya kazi mule shughuli yoyote ya kuhudumia abiria wahakikiwe na kupewa vitambulisho na wachunguzwe mara kwa mara
 
Uongozi wa Magufuli Terminal wekeni bango kubwa kuwa tiketi za mabasi zinakatwa ghorofa ya 2; Abiria wajue kuwa ofisi za mabasi zipo ghorofa ya 2 na tiketi ndio zinapatikana huko.

Bango liwe kubwa na liwepo chini na pia kwenye ukuta juu kama lilivyo la KAIRUKI hospital nk

Maana ya uwepo wa uongozi ni pamoja na kuhakikisha usalama wa abiria watarajiwao, sio kukusanya mapato tu.
Viongozi wanalijua hilo na unaweza ukawa ni sehemu ya mradi wao na pendekezo km hili hawawezi kulifanyia kazi sababu litawaondolea maokoto ya juu kwa juu kwa njia ya utaperi wa abiria, kingine cha maana ni kupiga TANGAZO kwenye spika kubwa kua 'abiria wote mnaoenda mikoani tiketi zinakatwa gorofa la Pili epuka matapeli tiketi haikatwi uchochoroni au barabarani ofisi za mabasi zipo gorofa la Pili'
 
Ukiwaita maajenti umewapa cheo kikubwa sana,wale wanaitwa masalange ukizubaa hadi mabegi wanakuibia.Kwa upande wangu naona tuzidi kupeana elimu ya kufika direct ofisini kukata tiketi na sio zaidi ya hapo..ukiona mtu anajifanya kukuonea huruma na hakujui tambua kuwa kifuatacho itv

Tatizo wakijua tu wewe ni msafiri utazongwa mpaka usifike huko kwenye ofisi za kukata tiketi. Na ukiwa na mizigo ndo kabisa utasumbuliwa kila tapeli anavuta begi lake kwa gia anakusaidia kukupeleka ofisini.

Kwa kifupi uongozi wa Stendi kuu ya Magufuli umefeli pakubwa sana.
 
Mie huwa nawapa Rizki wanawake/Wadada wale wanaosimama nje wanauliza naenda wapi ili wapate cha juu.. huwa nawakunjulia moyo.

Kuna siku nimemkunjulia mmoja wao alivyo fala akaenda kuni direct kwa jamaa mwingine.. nae ni ajent wa mchongo.

Akanipandisha gari baya sijapata kuona.. nauli kubwa na safari ilikuja kuanza 5 hrs baadae (Ilikuwa usiku nilitaka nifike Dodoma Asubuhi so nilienda magufuli pale saa 1 usiku nikaja kuanza safari saa 6 usiku huko)

Niliapa kwa miungu yangu yote kwamba sitakuja kuwaonea huruma tena.

Pia nilivumilia kwa kuwa nia yangu niingie Dom asubuh bas ikabidi niwe mpole....
 
Pamoja na kwamba Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kimetengeneza ajira kwa watu wengi, lakini kuna jambo moja linaloendelea pale na linaonekana kufumbiwa macho na mamlaka husika. Jambo hilo ni utapeli.

Juzi nikiwa kwenye pitapita zangu, nikaona watu wamemzingira mama mmoja wa makamu. Mama huyo alikuwa akiangua kilio kwamba yeye alikuwa ameteremka kwenye daladala za Kinyerezi na wakati yupo kwenye daraja la juu la watembea kwa miguu linalounganisha upande wa Kituo cha Daladala cha Mbezi Louis na Magufuli Bus Terminal, alikutana na “ajenti” wa mabasi ya mikoani.

“Ajenti” yule alimshawishi mama yule na kumuuzia tiketi ya kwenda Kondoa na akamuandikia na kukabidhi kisha alipoingia ndani ya stendi akamwambia asubiri kwenye moja ya mabenchi mpaka basi lake litakapofika dakika ishirini baadaye.

Kutokea hapo hakumuona tena bwana yule. Na tiketi aliyokuwa amepewa haikuwa halali. Kwanza haikuwa tiketi halali ya gari aliloahidiwa, na pili gari hilo halifanyi safari za huko alipokuwa anaenda. Basi mama yule akawa amepoteza fedha zake.

Lakini hiyo haikuwa mara ya kwanza kusikia kuhusu watu kutapeliwa pale Magufuli. Kuna taarifa nyingi kuwa wale wanaojiita “maajenti” baadhi yao wako pale kwaajili ya kuchungulia fursa za kuwatapeli abiria wanaoenda mikoani. Inaelezwa kuwa kuna watu wengi safari zao zimekomea pale baada ya “kupigwa” na matapeli.

Ni sawa kwamba kinachoendelea kinatoa ajira kwa watu wengi, lakini kunaweza kuwa na utaratibu mzuri tu. Ni muhimu hao “maajenti” kama wanatambulika na makampuni ya usafirishaji wavae vitambulisho au sare. Kuna baadhi huwa wanavaa hivyo, lakini wengi wao hawana sare wala vitambulisho. Wanauza maneno tu. Tena wanawadaka wateja wanaposhuka tu kwenye daladala. Yaani kabla hujashuka unaona watu wamejaa mlangoni wanakuwania kama mpira.

Mamlaka ziliangalie hili na ziweke msimamo thabiti dhidi ya jambo hilo. Kila ajenti awe na kitambulisho na sare fulani inayomtambulisha, au namba kwenye kizibao au utaratibu mwingine wowote ule utakaofanya hawa watu watambulike kirahisi.

Lakini pia, hata wale maajenti ambao wanatambulika basi wasaidie kuwatambua wale wanaowaharibia kazi kazi yao.
Hao watu tunawalea wenyewe kwa ushirikiano wa raia na serikali. Raia wa tz wengi si wadadisi, si wenye kuhoji. Mpaka leo kuna mtu anafika stendi hajui A wala B. Elimu hazitusaidii. Serikali wala haijali, wahalifu wanajulikana. Askari wapo. Siku serikali ikiweka mapepo kando ikianza zimamoto kuwafukuza matapeli, watz wenyewe tutawatetea matapeli.

Na hili nalo mpaka tupoteze pesa kupeleka watu kwenda kujifunza Rwanda?
 
Nakumbuka mwaka 2021 jamaa mmoja nilipanda nae daladala ya kutoka rangi tatu asa sijui alinioteaje sehwmu ninayoenda.
Tunakaribia kufika mbezi akawa ananipigisha stori mi nikajua abiria mwenzangu.
Ile tumeshuka tu kwenye daladala ananiuliza kwani wewe unaenda wapi.
Mi nikamjibu naelekea mwanza.
Tufupishe story jamaa na agent mwenzie walinipiga 15000 extra kwenye nauli ya kawaida.
Tokea hapo huwa sikati tiketi physically ni online tu tena kwenye kampuni aminika.
 
Dawa pakee ukifika pale ni kuingia ndani ya stendi na kuhakikisha unakata tiketi nje ya basi husika, na baada ya hapo unaingia kwenye basi.

Ukiingia tu mkenge na kuwapa hela wale wahuni wa pale nje, unaweza ukajikuta umepigwa! Au hata kupakizwa kwenye basi tofauti kabisa na lile ambalo unataka.
 
Matapeli wengi sana pale MAGUFULI STAND. Me mwenyewe juzi kati hapa nilikua na safari ya kwenda Tanga sasa nilipofika pale kuna dogo akawa ananichombeza, nikamwambia me naenda tanga basi tukawa tunaongozana kuingia ndani ya Stand nikiamini pengine tunaenda office zilipo, mara akatokea jamaa mwingine akaanza kuongea na yule dogo, huyu anaenda wapi yule dogo akasema Tanga powa twenzetu cha ajabu hata hatujafika ndani yule Agent uchwara akaanza kuniuliza eti unazijua nauli zake lakini, nikamwambia Ndiyo si 15000! Jamaa akanijia juu, hivi upo sawa wewe, unaishi nchi hii wewe inamaana hujui kama mafuta yamepanda bei. Nikamwambia kwani Bei gani? eti 25000TZS. Niakmwambia basi poa Acha kuna mtu nimpigie simu nimuulize maana yeye kasafiri siku si nyingi

Nikamuona mdogo mdogo yeye na mwenzake wanaondoka tena akawa anazuga anaongea na simu, kimtindo kama walijua dili Lao linaendq kubuma

Nikaamua niingie ndani then Kuna jamaa nilikutana nae yeye ndiye akanipa info za kutosha na akaniambia subiri kesho Hasubuhi ukate tiketi palepale yanapoondoka nikafanya hivyo.

nilifanikiwa kukata tiket japo nilipigwa badala ya elfu20 yule agent akaniambia elfu22 buku mbili akifinya.

Upigaji hii nchi hauwezi kwisha na hii yote ni kutokana na tatizo la Ajira nchini kwetu vijana hawataki kufanya kazi ngumu.
 
Ukiwa mkazi wa Mbezi, wale jamaa wanaganda kila mtu.. kila wanaemuona wanadhani ni msafiri.. wanaweza kukusindikiza safari yako wakidhani unaenda kukata tiketi na husemi..
Mimi nawaachaga wawe mabodigadi wangu kwa kunisindikiza mpaka pale watakapojua hawajui. Juzi nimesindikizwa na kundi la watu wanne kwenda kuchukua kijibahasha kidogo kutoka mkoani.
 
Wenye mamlaka au wamiliki wa magari wange tengeneza mfumo ili Kila anaetaka kusafiri akate tiketi yake kwa njia ya mtandao, yani ajue kabisa zimebaki siti ngapi kwenye gari husika sio habari za kuuziana siti moja kwa watu wawili ukifika stand ni kupanda gari na kuondoka tuu
 
Back
Top Bottom