mzungu wa roho
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 209
- 141
wanakufa na fashion
Kula like mkuuHumo huwa kuna vyumba vyao.
Yani begi self contained.. Lina boxer, jeans, t-shirts, vests, toothpaste, toothbrush, hair combs, shoebrush, nail cutter na vitamba ya kijifutia raba zao.
Usisahau lotion na perfume.. Wanakuambia kambi popote..
Kama hutoki namtumbo wewe ni bahati...!!
!
Habari wadau wa jukwaa hili!
Mnisamehe sana kama nitawakwaza na swali langu.
Hivi haya mabegi ya mgongoni ambayo watu wanakuja nayo hadi kwenye sehemu za starehe huwa wanabeba vitu gani?
Hasa ndugu zetu wa dar ambao huombea mvua inyeshe ili wavae masweta yenye Kofia.
Umemaliza mkuu,,hasa mikoani huku..Wengi wao wenye hayo mabegi ni mafundi ujenzi
Man umenifurahisha sana ,watu wako kitahadhari zaidiWengi wao wanaweka mawe, si unajua Dar hii, saa yoyote ugomvi unaweza kutokea, zana muhimu.
He mkuu kumbe wanabeba hamna kitu? Mimi nilidhani kuna madaftari au laptop. Mimi siyo kijana lakini naweka laptop na nisipoenda na gari naweka begi mgongoni na ndani mna laptop. Basi vijana ni washamba. Begi ni kuhifadhi vitu siyo urembo.Sijui wanaweka nini humo ndani, maana ni kama fashion kwa sasa.
Juzi wakati nipo Taifa kuna kijana nilikaa nae jirani wakati anafungua nikachungulia, Ajabu katoa headphone ya simu na hamkuemo na kitu kingine cha ziada ndani nilichoka sana.
Binafsi naona kama ni ushamba fulani hivi ambao vijana wanalimbukia bila kujielewa.
siku hizi vijana WA DARSijui wanaweka nini humo ndani, maana ni kama fashion kwa sasa.
Juzi wakati nipo Taifa kuna kijana nilikaa nae jirani wakati anafungua nikachungulia, Ajabu katoa headphone ya simu na hamkuemo na kitu kingine cha ziada ndani nilichoka sana.
Binafsi naona kama ni ushamba fulani hivi ambao vijana wanalimbukia bila kujielewa.
We mtoto upo?!Haaa haaa ...huu Uzi ni wa zamani ila nimeupenda!
mkuu nimecheka mwenyewe hapa kama zuzuKuna mwingine niliona ameweka deki chakavu ya SUMSUNG ili ionekane kama laptop, sasa nikawa naona hiyi laptop kila siku hatoi, kuna siku nilasema ngoja nichungulie, nilichoka!