lwambof07
JF-Expert Member
- Jul 12, 2016
- 4,643
- 5,348
sasa kuweka mbele na kuweka nyuma wapi salama zaidiWengi wenye hayo mabegi hasa mida ya asubuhi na jioni huwa wanaelekea ama kutoka maofisini, darasani na huwa wamebeba laptop, karatasi ama vitabu muhimu kwa siku hiyo. Hivyo kuwaambia wasibebe hayo mabegi ni sawa na kumwambia mkulima aende shambani bila jembe huku ukihimiza afanye kazi.
Tatizo la kumpa mtu akushikie au kuliweka mbele ukizubaa kuna wajanja wengine wanaweza kulifungua na kuchukua vilivyomo ndani au kushuka nalo kabisa, hii hutokea mara nyingi kutokana na msongamano mkubwa kwenye vyombo hivi vya usafiri.
Wengine wanaweza kukuwekea kitu ndani na ukazushiwa kesi ushukapo kituoni.
Tatizo mjini maadili yameshaharibika na hakuna wa kumwamini.