Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

mkuu mimi nafanya jazi ya ulinzi, siwez kutoka na minguo yangu ta kazi kutoka mbezi mpaka posta, acha asubuhi nipige mtoko vizur kama wewe unaefanya kazi TRA alaf wote tuepekee posta 'kazini' minguo yangu ya kilinzi naitupia kwe begi ukiniuliza nakwambia kuna laptop
 
Habari wana JF,

Najua kama mabegi hutumika kuweka vitu mbalimbali ila kero yangu ni kwa wale wanayoyavaa mgongoni kwenye daladala/mwendokasi kama tunavyojua zinavyajaza bora hata uweke mbele au umuombe mtu akushikie kuna wengine wabishi kuyaweka vizuri hata ukimwambia halafu kwanini sikuhizi yamekuwa mengi sana tofauti na zamani?

Sasa usiombe gari lifunge brake ghafla utaipata flesh hata mikoba ya wanawake nayo ni kero kubwa.

Kama hupendi kero nunua usafiri wako
 
Mleta mada umegusa pale pale, yaaani hii kero ya vibegi imezidi. Wenyewe wanaita swagga. Utakuta mtu anageuka gafla kwenye mrundikano wa watu bila kujali kwamba ana kibegi matokeo yake uliye nyuma yake unapigwa kikumbo na lile begi! Acheni kuiga kila kitu vijana, igeni mbinu za kusaka pesa.
 
Mkuu sasa unafikiri watabebea nini material?

Mfano mwanafunzi anakaa Hostel Mabibo alafu anatoka kwenda Campus kupiga kitabu,we unafikiri atabeba vitabu na vitini mikononi? Huko kuna laptop pia ili kumuwezesha kwenye mambo mbalimbali.

Hebu wavumilieni maana hakuna jinsi. Cha msingi wawe waelewa tu!
 
mkuu mimi nafanya jazi ya ulinzi, siwez kutoka na minguo yangu ta kazi kutoka mbezi mpaka posta, acha asubuhi nipige mtoko vizur kama wewe unaefanya kazi TRA alaf wote tuepekee posta 'kazini' minguo yangu ya kilinzi naitupia kwe begi ukiniuliza nakwambia kuna laptop
sawa kaka mi mwenyewe nabeba sana ila simkeri mtu nikifika kwenye daladala naangalia utaratibu kama kumpa mtu anishikie au kama kuna sehemu niweke ikishindikana sana naweka kwa mbele
 
Mleta mada umegusa pale pale, yaaani hii kero ya vibegi imezidi. Wenyewe wanaita swagga. Utakuta mtu anageuka gafla kwenye mrundikano wa watu bila kujali kwamba ana kibegi matokeo yake uliye nyuma yake unapigwa kikumbo na lile begi! Acheni kuiga kila kitu vijana, igeni mbinu za kusaka pesa.
Hapo umenena
 
Mkuu mbona unalalamika sana. Kwani hii pia ilipaswa iwe thread?
 
Mkuu sasa unafikiri watabebea nini material?

Mfano mwanafunzi anakaa Hostel Mabibo alafu anatoka kwenda Campus kupiga kitabu,we unafikiri atabeba vitabu na vitini mikononi? Huko kuna laptop pia ili kumuwezesha kwenye mambo mbalimbali.

Hebu wavumilieni maana hakuna jinsi. Cha msingi wawe waelewa tu!
Hapo sawa "WAWE WAELEWA" nimeipenda hiyo,ukiwa muelewa ukiingia kwenye daladala utaangalia namna nzuri ya kuweka begi lako vizuri usiwakere wengine
 
Kwa hio wewe unataka wabebe mifuko ya rambo?
 
Wengi wenye hayo mabegi hasa mida ya asubuhi na jioni huwa wanaelekea ama kutoka maofisini, darasani na huwa wamebeba laptop, karatasi ama vitabu muhimu kwa siku hiyo. Hivyo kuwaambia wasibebe hayo mabegi ni sawa na kumwambia mkulima aende shambani bila jembe huku ukihimiza afanye kazi.

Tatizo la kumpa mtu akushikie au kuliweka mbele ukizubaa kuna wajanja wengine wanaweza kulifungua na kuchukua vilivyomo ndani au kushuka nalo kabisa, hii hutokea mara nyingi kutokana na msongamano mkubwa kwenye vyombo hivi vya usafiri.

Wengine wanaweza kukuwekea kitu ndani na ukazushiwa kesi ushukapo kituoni.

Tatizo mjini maadili yameshaharibika na hakuna wa kumwamini.
 
Habari wana JF,

Najua kama mabegi hutumika kuweka vitu mbalimbali ila kero yangu ni kwa wale wanayoyavaa mgongoni kwenye daladala/mwendokasi kama tunavyojua zinavyajaza bora hata uweke mbele au umuombe mtu akushikie kuna wengine wabishi kuyaweka vizuri hata ukimwambia halafu kwanini sikuhizi yamekuwa mengi sana tofauti na zamani?

Sasa usiombe gari lifunge brake ghafla utaipata flesh hata mikoba ya wanawake nayo ni kero kubwa.
Kweli mkuu mi juzi nimegombana na jamaa alikuwa kabeba beg mgongoni kumbe ndani kaweka samaki wabichi wanatiririsha mimaji ya barafu alafu na yeye kesha loa kwenye koti alokuwa amewaa hana habari si akanipaka maji!!asee nilimchenchia sana
 
Back
Top Bottom