Hivi kwa mfano umevaa suti huu mkoba wako unaufanyaje? maana nimefuatilia hii thread naona imejaa watoto na wavaa tshirt na jeans. mikoba ni muhimu kwa kina mama na siyo wanaume na inategemea dressing code.
Swali zuri sana
Matola...kwa upande wa mavazi nakubaliana na wewe na nitakuongezea kwenye umri pia.
Kwanza nakataa ukisema mikoba kama hii hasa kama huu wangu niliouonyesha hapo juu eti ni special for lady's only.
Ukweli ni kwamba mikoba wanayobeba wamama au wadada inaeleweka na kufahamika machoni vizuri sana kiasi kwamba
mwanaume yeyote akatokea kubeba mkoba huo basi hata jamii inayomzunguka itamshangaa sana kwani kama nilivyosema kuwa mikoba ya kike inajulikana sana.
Kwenye mavazi nakubaliana kabisa na wewe...ni kweli huwezi kuwa kwenye vazi la suti then ubebe mkoba kama huo wangu.
Binafsi sipendi vazi la suti ila nililivaa siku moja tu siku ambayo niliingia kanisani kumuoa mwanamke ninayempenda hadi leo...na sitarajii kuvaa vazi hilo tena kwenye maisha yangu labda itokee kitu fulani cha muhimu sana na kiwe kinahusu pesa tena pesa ya maana hasa na siyo ilimradi ela.
Mkoba kama huo wangu hapo juu unapendeza kuubeba ukiwa kwenye vazi la tshirt na jeans...na mimi hilo ndilo vazi langu.
Umri: Binafsi nimepanga siku nikifikisha umri wa miaka 40 sitaweza tena kubeba huo mkoba kwani kila kitu kina age limit.
lakini kwa vile niko chini ya umri wa miaka 40 na ninapenda tishirt na jeans basi nitaendelea kuubeba mkoba huu kila siku no matter niwe kwenye daladala,niwe kwenye Gari yangu au niwe na walk by foot baada ya kushuka kwenye gari nitaubeba tu.