Teh! Mkuu huyo huo uwezo wa kuunga atautoa wapi? Kaungishwa huyo! Labda kwa mfano huu nakubaliana na
Juliana Shonza kwamba CCM "inawajali" vijana kama ilivyomuungisha Nape toka Div. 0 hadi Masters isiyoeleweka.
Lakini pia ikumbukwe Nape hakuungishwa hivi hivi bali kupitia nyota ya baba na hapo ndipo penye tatizo. Ni wangapi nyota za baba zao zinang'aa humo chamani? Nape ni miongoni mwa elites wanaofaidi keki ya nchi sio kwa sababu wana uwezo sana kupita waTz wengine, la hasha; bali kupitia mfumo dhalimu, wa kitabaka na kujuana. Ni kwa sababu tu alizaliwa na Brig. Mosses Nnauye na sio vinginevyo.