Vijana tunapopewa nafasi tuzitumie kutengeneza fursa nyingi kwa wengi zaidi. Hili la Sabaya ni kosa, tusahihishe

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Wasalaam,

Viongozi wetu wakuu wanapoteua vijana ambao pengine hawana uzoefu wala ujuzi mkubwa sio kwamba tunastahili sana ila ni kwa sababu tunatengenezwa mazingira ya kuaminiwa kwa nafasi za juu na pengine siku moja vijana ndio washike hatamu ya uongozi wa Taifa hili. Kinachoendelea sasa, badala ya vijana kujenga imani kwa kuongeza maarifa, ujuzi na uwezo tumegeuka kuwa wajenga hofu kwa kufanya siasa za kibabe na zisizo na tija. Ningependa ubabe huo tungeutumia kutafuta fursa za uwekezaji na ujasiriamali kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wetu.

Siku chache zijazo Rais wetu atafanya mabadiliko kwenye nafasi za ukuu wa wilaya na ukurugenzi wa halmashauri na pengine katika nafasi hizi tutaona sura mpya nyingi za vijana. tutapewa nafasi nyingine muhimu ya kuaminiwa kwa nafasi za uongozi, tutumie nafasi hizi kujijenga na kuonesha imani kwa wananchi. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetengeneza mazingira mazuri kwa vijana wengine kuaminiwa.

Tabia aliyoionesha Sabaya na vijana wengine, inasikitisha na hazifai kuwa tabia ya kiongozi awe kijana ama mzee, hivyo tabia hizi tuepukane nazo na kuachana nazo kwa sababu ni doa kubwa. Tuchukue hii kama ni changamoto hivyo tusahihishe, kwa kufanya hivi hakika vijana ni mabadilio. Tumsaidie Rais wetu anatuhitaji sisi vijana.
 
Nakubaliana na wewe...

Lakini hili halipo kwa ajili ya vijana tu. Ni kwa mtu yeyote kwa sababu UOVU na UBAYA hauna cha kijana wala mzee.

Ole Lengai Sabaya alikuwa na matatizo makubwa na hatari na yaletayo mauti matatu.

1. Tamaa za kidunia na za kimwili i.e kupenda ufahari, Mali, kutukuzwa na kusifiwa. Haya ndiyo mambo ambayo dunia inayatoa na mwili kuyatamani. Ukiyapenda hayo bila akili na kipimo, mwisho wako ni MAUTI tu.

2. Kutotumia fursa ya matajiri wa mali na akili za watu wa ndani ya wilaya yake aliyokuwa anaiongoza kwa ajili ya kuwainua wasiokuwa nacho (masikini).

3. Ni mtu ambaye yuko so addicted na itikadi za siasa za ki - CCM kiasi cha kuwaona wote wasio wa CCM ni maadui wa maendeleo kitu ambavyo siyo kabisa.

Laiti angekaa na kuwatumia vizuri watu ambao tayari wana mitaji na kuomba serikali ishirikiane nao, pengine Hai ingeokoa vijana, wazee na maskini wengi kwa kuwafungulia fursa za kimaendeleo.

Alichofanya yeye ni kinyume chake kabisa. Akawa na juhudi za makusudi kuvuruga biashara na uwekezaji na mitaji ya watu hawa na badala ya kupigana vita ya umaskini na ujinga, akazidi kuuongeza.

Mfano unawezaje kuishawishi serikali iharibu biashara ya mtu aliyewekeza mtaji wa karibu Tshs. 1,000,000,000 eti tu kwa sababu huyo mtu si mwanachama wa chama chake CCM...??

Hivi ni lini itatokea kiongozi mfano Rais wa nchi au Diwani au Mbunge au DC akaongoza watu wenye itikadi ya chama kimoja tu...??

It's impossible. Watu wenye mtazamo huu wa ubinafsi, hawastahili kuwa viongozi katika jamii yenye watu wenye itikadi na imani tofauti tofauti...

Mwendazake Magufuli ndilo hasa lilikuwa tatizo lake pia...
 
Baada ya Sabaya sasa ni ya Simalenga. Huu uzi utadumu sana kama vijana wasipojisahihisha
 
Back
Top Bottom