Awamu hii ya serikali Ina support yangu kwa kuwajali na kuwaamini vijana katika uongozi

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Ingetokea nikaulizwa orally, maoni yangu jinsi serikali inavyowakumbuka vijana katika nafasi za kazi na hasa za uteuzi, ningesema bila wasiwasi Wana support yangu asilimia mia.

Binafsi ninapendezwa na kusuuzwa juu ya consideration waliyonayo viongozi wetu kwa kundi la vijana.

Vijana ndo uhai wa nchi kwa maana ya kuendeleza urithi (succession) hivyo kuwaweka mapema ktk nafasi za uongozi na kazi nyinginezo inajenga uimara (stability)wa nchi katika eneo la uongozi lakini pia inajenga kundi hili kuwafanya wakue wakiwa wamesheeni upana wa mambo kwani waliaminiwa na kujengwa mapema.

Hapa ndo napata moyo hasa wa kuipongeza serikali na hasa katika awamu hii na ninakiri hakika wanasitahili pongezi kwa hili.

Ukianza awamu ya kwanza ya serikali ya awamu hii Rais magufuli pamoja na complexity ya utawala wake (ambao nikiri sikuushabikia sana) uteuzi wa vijana na kuaniniwa kwao, kulivunja record ya tawala zilizomtangulia.

Kudos Magu walau kwa hilo. Hakujali background au status ya huyo anayemteua. Mara nyingi alisukumwa na ujana wa mtu na sifa nyinginezo kidogo. Ungempata wapi mtu kama Aweso, Nikki wa Pili, Jokate Mwegelo, Makonda, Chalamila na wengineo kuaniniwa katika nafasi muhimu kama zile kwa umri huo (ule) wa ujana wao?

Awamu hii ya pili ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Samia (naomba hapa nisamehewe, common sense inanifundisha kuuita utawala huu awamu ya tano na Rais wa sita, ingawa pale ninapotaka kuepuka shida zisizo za lazima, huuita awamu ya sita) nao ndo kabisa koleo limeshika moto.

Hussein Bashe, Aweso, Grace Kingarame, Abdallah Mwaipaya, Fatuma Almas Nyangasa, Katrida Mgeni, Chongoro, mlete nani?

Unaweza ona kabisa trend ya ujenzi wa kundi hili la vijana kuaniniwa na kupewa nafasi kubwa za kimajukumu ambazo kwa namna na mazoea wangepewa watu ambao achana tu kuchoka, wengine ni kama wanalazimishwa tu kufanya kazi hizo.

Awamu ya tano na Marais wawili wa awamu hizi oyeeeee!

Na watu waseme oyeeeee.

Keep this trend up!
 
Back
Top Bottom