SoC02 Vijana tufanye kazi, nyakati zinabadilika, uchumi wako unategemea utendaji kazi wako

Stories of Change - 2022 Competition

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,857
Salaam kwenu wapenda maendeleo. Najua Kuna wakati tunawachosha kwa makala nyingi za mfululizo , tusichoke kushiriki Hanna kwasababu kupitia platform hii, Kuna watu wanabadili mitazamo. Kuna wengine tunaandika siyo tu kwaajili ya shindano la story of change, No, wengine tunaitumia platform hii kufikisha ujumbe.

Leo nataka kuwakumbusha vijana wenzangu, kwamba, khari imebadilika Sana, haswa kuhusu maisha yetu sisi wenyewe. Kwa mfano, zamani ilikuwa kijana ukichangamkia fulsa fulani, kutoka ilikuwa kilahisi Sana, lakini kwa sasa khari ni tofauti Sana kwasababu kila unachokitafuta, unagawana na wengi haswa serikali. Kwa mfano,
  • Zamani ilikuwa ukiamua kujiingiza kwenye siasa, kutoka ilikuwa kilahisi kuliko siku hizi maana siasa za nchi hii zimekuwa ngumu lakini pia hazilipi na zinazowalipa ni kundi fulani tu.
  • Zamani ilikuwa unijichanganya kwenye elimu, kutoka ilikuwa kirahisi kwasababu ilikuwa ukijituma tu, unafikia malengo yako na hapakuwa na usumbufu Sana hata kufikia ajira uitakayo, lakini hivi sasa, kufika chuo tu ni mateso, kuomba nafasi tu ya Chuo ni sawa na kuomba ajira, ukifika chuo na ukahitimu, bado kupata kazi ni kazi pia.
  • Zamani ilikuwa ukiamua kujichanganya kwenye kilimo, kutoka ilikuwa kirahisi kwasababu hapakuwa na ushuru mwingi, lakini siku hizi serikali imekamata kotekote, kulipa tu shamba gharama zake ni changamoto, ukilipata, uendeshaji wake ni tabu kwasababu pembejeo zenyewe ni shida, wadudu ni wengi ,kwa ujumla mtaji wa kilimo ni sawa na mavuno ya kipindi Cha nyuma.
  • Zamani ilikuwa ukiamua kujichanganya kwenye biashara, kutoka ilikuwa kirahisi kwasababu serikali ilikuwa haifuatilii Sana. Siku hizi mpaka upate frame na kuiandaa, gharama zake ni kubwa Sana, bado ukifanikiwa, serikali inaanza kukusanya kile unachokipata kupitia ushuru, bima, usafi, too, Kodi, michango nk. Kwa ujumla manbo ni MBAMBAMBA
  • Zamani ilikuwa ukiamua kujichanganya kwenye ujasiliamali kutoka ilikuwa kirahisi Sana kwasababu wajasiliamali wenyewe walikuwa wachache na hapakuwa na kuingiliwa Sana na serikali. Baada ya serikali kuamka, ujasiliamali umekuwa mgumu Sana, hivyo vijana wamekuwa wakijaribu kila kitu alimladi kubahatisha wapi panaweza kuwatoa.

TUTAFANYA NINI SASA SISI KAMA VIJANA?

Kwanza, lazima tukubali Mambo yamebadilika, tulikubaliana na hilo tu, tutafanya vizuri katika utafutaji wetu.

Pili, lazima tuachane na lawama juu ya serikali, jamii au yeyote kwa namna yoyote lakini tujikite nakufanya kazi tu kwa bidii

Tatu, nyakati zimebadilika, hatuwezi tena kuishi kwa mazoea ya zamani. Mfano, zamani ilikuwa muda wa kufanya kazi ni mchana zaidi, lakini kwasasa tunapaswa kuongeza muda wa kufanya kazi ikiwezekana tufanye kazi kwa shift. Mfano, Kama wewe una mke, mchana mke wako asimamie biashara yenu Kisha usiku usimamie wewe.

Kama unaenda shamba mchana, hakikisha na jioni hadi usiku unarudi shamba. Kama wewe ni mwalimu unafundisha mchana hakikisha na usiku unapata wanafunzi wa kufundisha, tenga muda kidogo Sana wa kusinzia ikiwezekana sinzia ukiwa hapohapo eneo la kazi, achana na musemo wa kulala masaa 8.

Kama wewe ni mtu wa kuchomelea vyuma au seremala, au dereva au mchuuzi, ongeza muda wa kuwa kazini. Muda wa kulala uwe masaa 2 au 3 tu kwa siku kwasababu Kama nilizozitaja huko juu, kwamba, wewe unategemewa na wengi. Unategemewa na
  • Serikali kupitia Kodi, tozo michango, ushuru, kupitia shughuri yako hiyo ikiwemo na makato ambayo kwa namna yoyote hayawezi kufutwa Leo au kesho.
  • Unategemewa na familia yako, Wazazi/walezi jamaa na marafiki.
  • Unategemewa na jamii katika Mambo mengi ikiwemo maafa na starehe, Mambo yote ni mhimu na mengi yanahusisha Pesa.

Kama yote hayo yanakugusa moja kwa moja, hupaswi kuwadhia kupunguziwa juu ya muda wa kufanya kazi, yaani wewe umeajiriwa na unawadhia kupungudhiwa muda wa kufanya kazi?. Ukiona mwajiri wako anakutaka ufanye kazi siku 5, mwambie ufanye kazi siku 7 akulipe na hizo siku 2. Kama mwajiri wako anakutaka ufanye kazi kwa masaa 10, mwambie utafanya kazi kwa masaa 18, nane ailipie.

Kama mwajiri wako anakupa likizo, mwambie akulipe mara mbili ili ufanye kazi hata kwenye hiyo likizo yako kwa mujibu wa mkataba wako . Ukifanya kazi kwa mtindo huu, hakuna uganga au uchawi utakao kukwamisha kufikia malengo yako. Utaihudumia serikali kwa mujibu wa sheria zake na itakazoendelea kubuni, utaihudumia familia yako na jamii yako. Hutoona uzito wowote kwa mchango wowote unaohusisha pesa kwasababu utakuwa tajiri wa pesa na utaona kila kitu kutoa ni UZALENDO.

Lakini ukiishi kwenye umasikini, utaishia kulalamika kila siku na bado serikali inawadhia kubuni namna gani ichukue hata hicho kidogo unachokilalamikia. Vijana tuongeze mwendo kwenye kazi zetu. Kama tulifanya kazi tukiwa tumekaa, basi kuanzia sasa tusimame. Kama tulifanya kazi tukiwa tumesimama, basi tuanze kutembea, Kama tulikuwa tunafanya kazi kwa kutembea, basi tufanye kazi kwa kukimbia. Kama tulifanya kazi kwa kukimbia, basi tufanye kazi kwa kupaa zaidi.

Niwahakikishie, hakuna unafuu utakuja kutokana na serikali kwamba, TOZO, USHURU, KODI, MICHANGO au mahitaji ya kifamilia na kijamii YATAKUJA KUPUNGUA, NO!! kila kitu kitakuwepo na vingine bado vinazidi kuibuliwa ikiwemo kupitia midahalo Kama hii kupitia JamiiForums. Ujue jamiiforums vijana wanajiandikia tu Kama wanajaribishia, baadae viongozi wa serikali wakiyapenda hayo mawazo na kuyafanyia kazi, vijana haohao wanarudi kuandika kwa kulalamika.

Yapo mambo mengi sana yanatekelezwa na serikali na yametokana na michango ya mawazo ya vijana/ members wa hapa hapa jamiiforum. Hivyo basi, kumbe bado Kuna mawazo mengi bado hata hayajaganyiwa kazi na yakitekelezwa barabara, pesa yako itakutoka.

Popote ulipo sasa, badili mtazamo kwanza maana mabadiliko huanza na MTAZAMO. Mimi nipo tayari, anza na wewe, wajurishe na wengine, share ujumbe huu kwa nia njema Wala siyo kwa ajili ya shindano. Tuhamasishane kufanya kazi kila mmoja Kama tulivyohamasika kuhesabiwa SENSA. Ujue, Japani ilifanikiwa baada ya kila raia alipohamasikia KUFANIKIWA kufanya kazi na kuendelea kiuchumi. Sisi afirika bado tunaona misaada ndiyo suluhisho la matatizo yetu.

Tukitegemea kusaidiwa tutaishi kwa kulalamika Sana. Hatuhitaji semina za kutuhamasisha kufanya kazi, tufanye kazi kuanzia sasa kwasababu tunayonafasi ya kufanya kazi. Kazi hiyo hiyo uliyonayo ndiyo msingi wa matanikio yako. Achana na mazoea, badili mtazo, ongeza muda, punguza muda wa kulala, punguza weekend, likizo na matumizi yasio ya lazima.

Achana na kutunziwa pesa zako kwenye vikoba.
Zungusha pesa yako mwenyewe. Ongeza assets, Kama vile viwanja na mashamba popote nchi hii. Jilipue katika shughuri zako, mfano, ukiamua kulima, usilime chini ya hekali 10. Chochote utakachokifanya, kifanye seriously, hakika utatoboa.

Natamani mawazo yangu yawe matamanio ya wengi.

Mwenyezi Mungu awe nanyi na azidi kubariki kazi halali za mikono yenu.🙏🙏
 
Mungu akubariki kwa maono haya. Lakini wasomaji na wachangiaji watakuwa wachache. Posts za maana hazichangamkiwi- Binafsi naungana na wewe na najitahidi kwenye hili.
 
Ahsante Sana kwa kunielewa, natamani wasomaji wengi wangepitia huu uzi ili ujumbe uwafikie wengi. 🙏🙏🙏
 
Mwenyezi Mungu nisaidie, thread yangu ipate views nyingi. Natamani watu wengi wajifunze, hivi sasa Mambo yamebadilika Sana. Vifurushi vya data viko juu. Hatuna budi kufanya kazi kwa speed ya supersonic
 
Nakuunga mkono asilimianyingi Sana mkuu,umenena vyema Sana mkuu,nakuombe thread yako ipate viewers wengi maana inaujumbe mzuri Sana wakimapinduzi ,vijana WA nchi hii tumezidi kupenda vya bure ,napia hatujitumi zaidi,unakuta MTU analalamika Hana Ajira,siku akiipata hyo Ajira ndio huyo huyo analalamika KAZI nyingi,mara weekends,mara anahitaji kupumzika mara yaani,anageuka kubembelezwa kufanya KAZI aliyokua akiililia Kwa Mda mrefu.
 
Salaam kwenu wapenda maendeleo. Najua Kuna wakati tunawachosha kwa makala nyingi za mfululizo , tusichoke kushiriki Hanna kwasababu kupitia platform hii, Kuna watu wanabadili mitazamo. Kuna wengine tunaandika siyo tu kwaajili ya shindano la story of change, No, wengine tunaitumia platform hii kufikisha ujumbe.

Leo nataka kuwakumbusha vijana wenzangu, kwamba, khari imebadilika Sana, haswa kuhusu maisha yetu sisi wenyewe. Kwa mfano, zamani ilikuwa kijana ukichangamkia fulsa fulani, kutoka ilikuwa kilahisi Sana, lakini kwa sasa khari ni tofauti Sana kwasababu kila unachokitafuta, unagawana na wengi haswa serikali. Kwa mfano,
  • Zamani ilikuwa ukiamua kujiingiza kwenye siasa, kutoka ilikuwa kilahisi kuliko siku hizi maana siasa za nchi hii zimekuwa ngumu lakini pia hazilipi na zinazowalipa ni kundi fulani tu.
  • Zamani ilikuwa unijichanganya kwenye elimu, kutoka ilikuwa kirahisi kwasababu ilikuwa ukijituma tu, unafikia malengo yako na hapakuwa na usumbufu Sana hata kufikia ajira uitakayo, lakini hivi sasa, kufika chuo tu ni mateso, kuomba nafasi tu ya Chuo ni sawa na kuomba ajira, ukifika chuo na ukahitimu, bado kupata kazi ni kazi pia.
  • Zamani ilikuwa ukiamua kujichanganya kwenye kilimo, kutoka ilikuwa kirahisi kwasababu hapakuwa na ushuru mwingi, lakini siku hizi serikali imekamata kotekote, kulipa tu shamba gharama zake ni changamoto, ukilipata, uendeshaji wake ni tabu kwasababu pembejeo zenyewe ni shida, wadudu ni wengi ,kwa ujumla mtaji wa kilimo ni sawa na mavuno ya kipindi Cha nyuma.
  • Zamani ilikuwa ukiamua kujichanganya kwenye biashara, kutoka ilikuwa kirahisi kwasababu serikali ilikuwa haifuatilii Sana. Siku hizi mpaka upate frame na kuiandaa, gharama zake ni kubwa Sana, bado ukifanikiwa, serikali inaanza kukusanya kile unachokipata kupitia ushuru, bima, usafi, too, Kodi, michango nk. Kwa ujumla manbo ni MBAMBAMBA
  • Zamani ilikuwa ukiamua kujichanganya kwenye ujasiliamali kutoka ilikuwa kirahisi Sana kwasababu wajasiliamali wenyewe walikuwa wachache na hapakuwa na kuingiliwa Sana na serikali. Baada ya serikali kuamka, ujasiliamali umekuwa mgumu Sana, hivyo vijana wamekuwa wakijaribu kila kitu alimladi kubahatisha wapi panaweza kuwatoa.

TUTAFANYA NINI SASA SISI KAMA VIJANA?

Kwanza, lazima tukubali Mambo yamebadilika, tulikubaliana na hilo tu, tutafanya vizuri katika utafutaji wetu.

Pili, lazima tuachane na lawama juu ya serikali, jamii au yeyote kwa namna yoyote lakini tujikite nakufanya kazi tu kwa bidii

Tatu, nyakati zimebadilika, hatuwezi tena kuishi kwa mazoea ya zamani. Mfano, zamani ilikuwa muda wa kufanya kazi ni mchana zaidi, lakini kwasasa tunapaswa kuongeza muda wa kufanya kazi ikiwezekana tufanye kazi kwa shift. Mfano, Kama wewe una mke, mchana mke wako asimamie biashara yenu Kisha usiku usimamie wewe.

Kama unaenda shamba mchana, hakikisha na jioni hadi usiku unarudi shamba. Kama wewe ni mwalimu unafundisha mchana hakikisha na usiku unapata wanafunzi wa kufundisha, tenga muda kidogo Sana wa kusinzia ikiwezekana sinzia ukiwa hapohapo eneo la kazi, achana na musemo wa kulala masaa 8.

Kama wewe ni mtu wa kuchomelea vyuma au seremala, au dereva au mchuuzi, ongeza muda wa kuwa kazini. Muda wa kulala uwe masaa 2 au 3 tu kwa siku kwasababu Kama nilizozitaja huko juu, kwamba, wewe unategemewa na wengi. Unategemewa na
  • Serikali kupitia Kodi, tozo michango, ushuru, kupitia shughuri yako hiyo ikiwemo na makato ambayo kwa namna yoyote hayawezi kufutwa Leo au kesho.
  • Unategemewa na familia yako, Wazazi/walezi jamaa na marafiki.
  • Unategemewa na jamii katika Mambo mengi ikiwemo maafa na starehe, Mambo yote ni mhimu na mengi yanahusisha Pesa.

Kama yote hayo yanakugusa moja kwa moja, hupaswi kuwadhia kupunguziwa juu ya muda wa kufanya kazi, yaani wewe umeajiriwa na unawadhia kupungudhiwa muda wa kufanya kazi?. Ukiona mwajiri wako anakutaka ufanye kazi siku 5, mwambie ufanye kazi siku 7 akulipe na hizo siku 2. Kama mwajiri wako anakutaka ufanye kazi kwa masaa 10, mwambie utafanya kazi kwa masaa 18, nane ailipie.

Kama mwajiri wako anakupa likizo, mwambie akulipe mara mbili ili ufanye kazi hata kwenye hiyo likizo yako kwa mujibu wa mkataba wako . Ukifanya kazi kwa mtindo huu, hakuna uganga au uchawi utakao kukwamisha kufikia malengo yako. Utaihudumia serikali kwa mujibu wa sheria zake na itakazoendelea kubuni, utaihudumia familia yako na jamii yako. Hutoona uzito wowote kwa mchango wowote unaohusisha pesa kwasababu utakuwa tajiri wa pesa na utaona kila kitu kutoa ni UZALENDO.

Lakini ukiishi kwenye umasikini, utaishia kulalamika kila siku na bado serikali inawadhia kubuni namna gani ichukue hata hicho kidogo unachokilalamikia. Vijana tuongeze mwendo kwenye kazi zetu. Kama tulifanya kazi tukiwa tumekaa, basi kuanzia sasa tusimame. Kama tulifanya kazi tukiwa tumesimama, basi tuanze kutembea, Kama tulikuwa tunafanya kazi kwa kutembea, basi tufanye kazi kwa kukimbia. Kama tulifanya kazi kwa kukimbia, basi tufanye kazi kwa kupaa zaidi.

Niwahakikishie, hakuna unafuu utakuja kutokana na serikali kwamba, TOZO, USHURU, KODI, MICHANGO au mahitaji ya kifamilia na kijamii YATAKUJA KUPUNGUA, NO!! kila kitu kitakuwepo na vingine bado vinazidi kuibuliwa ikiwemo kupitia midahalo Kama hii kupitia JamiiForums. Ujue jamiiforums vijana wanajiandikia tu Kama wanajaribishia, baadae viongozi wa serikali wakiyapenda hayo mawazo na kuyafanyia kazi, vijana haohao wanarudi kuandika kwa kulalamika.

Yapo mambo mengi sana yanatekelezwa na serikali na yametokana na michango ya mawazo ya vijana/ members wa hapa hapa jamiiforum. Hivyo basi, kumbe bado Kuna mawazo mengi bado hata hayajaganyiwa kazi na yakitekelezwa barabara, pesa yako itakutoka.

Popote ulipo sasa, badili mtazamo kwanza maana mabadiliko huanza na MTAZAMO. Mimi nipo tayari, anza na wewe, wajurishe na wengine, share ujumbe huu kwa nia njema Wala siyo kwa ajili ya shindano. Tuhamasishane kufanya kazi kila mmoja Kama tulivyohamasika kuhesabiwa SENSA. Ujue, Japani ilifanikiwa baada ya kila raia alipohamasikia KUFANIKIWA kufanya kazi na kuendelea kiuchumi. Sisi afirika bado tunaona misaada ndiyo suluhisho la matatizo yetu.

Tukitegemea kusaidiwa tutaishi kwa kulalamika Sana. Hatuhitaji semina za kutuhamasisha kufanya kazi, tufanye kazi kuanzia sasa kwasababu tunayonafasi ya kufanya kazi. Kazi hiyo hiyo uliyonayo ndiyo msingi wa matanikio yako. Achana na mazoea, badili mtazo, ongeza muda, punguza muda wa kulala, punguza weekend, likizo na matumizi yasio ya lazima.

Achana na kutunziwa pesa zako kwenye vikoba. Zungusha pesa yako mwenyewe. Ongeza assets, Kama vile viwanja na mashamba popote nchi hii. Jilipue katika shughuri zako, mfano, ukiamua kulima, usilime chini ya hekali 10. Chochote utakachokifanya, kifanye seriously, hakika utatoboa.

Natamani mawazo yangu yawe matamanio ya wengi.

Mwenyezi Mungu awe nanyi na azidi kubariki kazi halali za mikono yenu.🙏🙏
Hongera mkuu
 
Back
Top Bottom