Baadhi ya Njia za kutumia ukiwa hujisikii kufanya kazi kazini

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
288
Saa zingine unaenda kazini ila hujisikii kufanya kazi, hizi ni baadhi ya njia ambazo unaweza tumia ili kupata wasaha kidogo usukume siku iende ujafanya kitu.

Unawaza jitafakari, kutumia muda wako kujua kwanini hujisijii kufanya kazi siku hio, Umechoka? unamsongo wa mawazo? kuna mazingira ya kazi yamekuchosha? Kwa kufahamu Chanzo inaweza saidia kutafakari zaidi nini ufanye ili uboreshe hali yako.

Kama umechoka unaweza tafuta namna ya kuboresha ratiba yako, kwakulala mapema, punguza mambo ya ziada kama kwa kupunguza mazoezi, kuzurura bila mpango au kujihusisha na dhana yoyote inakutumia nguvu mara kwa mara.

Unaweza jipongeza na zawadi ambazo hazihitaji kuwa ghali, zinaweza kuwa ishara ndogo tu za kukubali kibinafsi. Kwa mfano, unaweza kutoa out kidogo kila unapowasilisha kazi mapema kuliko muda wa mwisho.

Ikiwa una shida kurudisha motisha yako na huwezi kupumzika, unaweza wasiliana na marafiki na familia kuhusu hisia zako. Mfumo wako binafsi wa msaada unaweza kukusaidia kupata fursa mpya na kushughulikia majukumu ya kibinafsi wakati unashughulikia pia hisia zako za kuchoka. Na saa nyingine wanaweza kupamawazo mema kutatua tatizo lako.

Huwa tunapuuzia sana ila unaweza ongea na daktari wa afya ya akili ili kuweza kukuhamasiha na kukupa motisha ya kurudi katika hali yako ya kazi.

Jikumbushe kwanini ulitaka hio kazi mwanzoni, Inaweza kusaidia kukumbushana kwa nini unafanya kazi na malengo yako ni nini. Kwa mfano, je, unafanya kazi ili kununua nyumba, kusaidia familia, au kuweza kumudu mtindo fulani wa maisha? Weka malengo yako akilini na uhakikishe unajikagua mara kwa mara ili kuthibitisha maendeleo yako.
 
asante sana mleta mada, nitaitumia hii kwenye kazi zangu, maana kuna siku mwili na akili zinakataa kazi kabisa.
 
Back
Top Bottom