Battle: Graduate vijana wa zamani na sasa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Niende moja kwa moja kwa kwa battle hii ya vijana waliomaliza vyuo vikuu miaka ya zamani na vijana wa Sasa.

Vijana wa zamani walikuwa wanasoma vyuo vikuu na ilikuwa sifa sana kwa jamii.

Kijana kufika chuo kwanza ilikuwa unaonekana unaakili sana.

Ilikuwa kama ajabu Fulani kwa jamii kuona kijana amefika chuo kikuu.

Ikumbukwe kipindi hicho vijana wa zamani walikuwa wachache sana wanaweza kwenda chuo kikuu.

Pia walikuwa wanasoma na uhakika wa ajira maana walikuwa wanasubiriwa na kazi kama vile watu wanavyosubiri kuingia kwa mwaka mpya.

Hivyo vijana walikuwa wanauhakika na kazi maana walikuwa wakimaliza tu na barua mkononi ya kuripoti kazini.

Vijana wa zamani wengine walikuwa na kiburi maana walikuwa wanachagua kazi, yaani walikuwa wanaweza kukataa kazi ya ofisi Fulani na kwenda pengine.

Ikumbukwe walikuwa wanafanya hivyo kwakuwa kazi zilikuwepo na kazi hizo ziliwahitaji wao zaidi kulingana na uhaba wa kipindi hicho ya wasomi.

Miaka ikaenda Sasa na vijana wa zamani wakapita, yaani wale vijana wa analogia na sasa wakaja vijana wa digitali.

Vijana wa sasa wao wengi wasomi yaani namanisha wengi ni graduate, saivi ulisema we ni graduate Wala haishangazi sababu ni wengi sana.

Ajabu na kwa bahati mbaya ni kuwa graduate hao wamekuwa wengi hadi wamekosa mahali pa kula ugali.

Hapa ninavyoandika graduate wanatafuta ajira sehemu mbalimbali ila wanakosa kulingana na kuwa wengi na uhitaji ni mchache kwa wanaoajiri.

Ukija kwenye ajira graduate wa Sasa wanatafuta kazi kwa 'connection' yaani kama huna mtu wa kukuunganisha basi huwezi kupata kazi.

Battle inaanzia hapa kwa vijana wa zamani na vijana wa Sasa wanawasema vijana wa Sasa kuwa wajiongeze.

Vijana wa zamani wanasema vijana wa Sasa hawajitumi wamekuwa wavivu.

Vijana wa zamani wamekuwa wagumu kuwaunganisha vijana wa Sasa kwenye nafasi za kazi huko ofisini.

Ninavyoongea hapa kuna kipindi waliwaita mabroo kuwa wanawatenga, hawataki kuwasaidia kupata kazi.

Ninavyoandika hapa ni kama kuna bifu fulani la vijana graduate wa zamani na graduate wa sasa.

Ninavyoandika hapa ni kama Kuna bifu fulani la vijana graduate wa zamani na graduate wa Sasa..

Donatila
Zamani sio tu kufika ⁶chuo kikuu iliouwa ajabu bali hata kwenda sekondari tarafa nzima lazima ipate habari kwamba kijana wa fulani kutoka ukoo fulanikaenda sekondari. Hata kipindi shule zikifungwa ukarudi kijijini kila mtu anakuwa anakutazama na kukutamani.

Siku hz vijana wanaenda sekondari hata wakiwa hawajui kusoma wala kuandika. Elimu imeshuka thamani sana na imekosa soko hadi vijana wanatia huruma.

Zamani kufaulu kwenda sekondar lazima uwe unajua masomo kwelikweli, sio siku hz serikali inawatungia mitihani ya kubet ili wafaulu wote....hata wasiojua kusoma na kuandika.

Serikali ya CCM imetuharibia sana mifumo ya elimu oamoja na kuishusha thamani ya elimu yetu.
 
I think hii ypte imesababishwa na elimu yetu kuwa stagnant while dunia inaendelea kwa kasi kubwa.
Elimu imekomaa kuhakikisha mtu anakariri na kufaulu mitihani instead ya kuhakikisha inamjenga mtu kupambana na changamoto.
Kuna lecturer wangu mmoja alikua mbunge mstaafu, yule mzee mitihani yake yote alikua hasimamii, anafika anagawa makaratasi, akimaliza anamwambia CR watu wakimaliza akusanye makaratasi ampelekee ofisini.
His motto was always, usiandike ulichokariri, broaden your way of thinking, hakuna wrong answers, just go deep in your mind and wrote what you understand.
Lakini pamoja na hyo, bado watu walikua wanakomaa kupiga chabo hata kama hakuna usimamizi. It ahows uozo wa elimu yetu.
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Niende moja kwa moja kwa kwa battle hii ya vijana waliomaliza vyuo vikuu miaka ya zamani na vijana wa Sasa.

Vijana wa zamani walikuwa wanasoma vyuo vikuu na ilikuwa sifa sana kwa jamii.

Kijana kufika chuo kwanza ilikuwa unaonekana unaakili sana.

Ilikuwa kama ajabu Fulani kwa jamii kuona kijana amefika chuo kikuu.

Ikumbukwe kipindi hicho vijana wa zamani walikuwa wachache sana wanaweza kwenda chuo kikuu.

Pia walikuwa wanasoma na uhakika wa ajira maana walikuwa wanasubiriwa na kazi kama vile watu wanavyosubiri kuingia kwa mwaka mpya.

Hivyo vijana walikuwa wanauhakika na kazi maana walikuwa wakimaliza tu na barua mkononi ya kuripoti kazini.

Vijana wa zamani wengine walikuwa na kiburi maana walikuwa wanachagua kazi, yaani walikuwa wanaweza kukataa kazi ya ofisi Fulani na kwenda pengine.

Ikumbukwe walikuwa wanafanya hivyo kwakuwa kazi zilikuwepo na kazi hizo ziliwahitaji wao zaidi kulingana na uhaba wa kipindi hicho ya wasomi.

Miaka ikaenda Sasa na vijana wa zamani wakapita, yaani wale vijana wa analogia na sasa wakaja vijana wa digitali.

Vijana wa sasa wao wengi wasomi yaani namanisha wengi ni graduate, saivi ulisema we ni graduate Wala haishangazi sababu ni wengi sana.

Ajabu na kwa bahati mbaya ni kuwa graduate hao wamekuwa wengi hadi wamekosa mahali pa kula ugali.

Hapa ninavyoandika graduate wanatafuta ajira sehemu mbalimbali ila wanakosa kulingana na kuwa wengi na uhitaji ni mchache kwa wanaoajiri.

Ukija kwenye ajira graduate wa Sasa wanatafuta kazi kwa 'connection' yaani kama huna mtu wa kukuunganisha basi huwezi kupata kazi.

Battle inaanzia hapa kwa vijana wa zamani na vijana wa Sasa wanawasema vijana wa Sasa kuwa wajiongeze.

Vijana wa zamani wanasema vijana wa Sasa hawajitumi wamekuwa wavivu.

Vijana wa zamani wamekuwa wagumu kuwaunganisha vijana wa Sasa kwenye nafasi za kazi huko ofisini.

Ninavyoongea hapa kuna kipindi waliwaita mabroo kuwa wanawatenga, hawataki kuwasaidia kupata kazi.

Ninavyoandika hapa ni kama Kuna bifu fulani la vijana graduate wa zamani na graduate wa Sasa..

Donatila
Uandishi mbovu huu; kama na wewe umetoka chuo kikuu basi ndiyo hivyo tena.Wale wa zamani walikuwa hawaandiki hivi.
 
Mabraza na Masista wa zamani ambao kwa sasa mpo !! wale wa kuzaliwa 1980's mpaka 1989 tuwaambie ukweli mnakunja sana yan kila sehemu mna uchoyo (sio wote lakini majority) Nyie ndo mko kwenye rika ambalo kama ulikomaa umeshajipata hata sisi tumeshajipata kiasi chake lakini hiyo michoro mingi inabidi tuitoe kwenu ila mnakunja kichizi !! iwe kwenye biashara , mifumo hata deal nyingine nyingine huko .

Mna kiroho fulani hivi sijui kwanini , Yaan unamsaidia mtu ila unatamani apate tabu kufanikisha issue yake wakati wepesi upo !! sijui ni kwa sababu mlilelewa kwenye mifumo ya ujamaa (Natania) 🤣🤣 naamin mabraza waliowatangulia waliwakarimu !!

Punguzeni kukunja watu wa 1980's !!

Sasa kuna hii Generation Z ya 2000 kulanina zao ina dharau mbovu sijui ni mayai ya broiller 🤣🤣 ila haina roho mbaya sema ni don't care.
 
Hii battle ni kali sana. Nikitaka kuwatetea grafuates wa zamani kuna sauti inaniambia acha uduwanzi hao unaotaka kuwatetea ndo walisaini Meremeta, IPTL, Uuzwaji wa Loliondo, Ununuzi wa rada kwa bei iliyopitiliza na mikataba mingi inayoliumiza taifa hadi ninapoandika hii comment.

Nikirudi kwa kizazi cha sasa nako pia kuna sauti inayoniuliza umesahahu hawa ndo graduates wasiojua kutofautisha L na R? Umesahau hawa ndo wenye One kali huku akiwa na F ya Maths? Umesahau hawa bila mhadhiri kuelezea kwa kiswahili hata kidogo hiyo lecture inaweza isieleweke kabisa? Hujui hawa ndo ambao ukimpa karatasi na kalamu anaweza shindwa kuandika application letter kwa mpangilio mzuri?
 
Back
Top Bottom