Vijana ni kwanini hamtaki kuoa?

Vijana ni kwanini hamtaki kuoa?

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,750
Reaction score
7,850
Ijumaa Kareem!

Kwamba mmeamua kumwaga ugali au?

Naomba nisiongee mengi leo ila nashuhudia malalamiko mengi sana kutoka kwa wanawake. J Pili nikipiga jicho Kawe kwa Mwamposa naona mamia ya akina dada tena ni warembo wenye maumbo yao, wakitaka kuombewa wapate waume.

Vijana fungukeni, nini kipo nyuma ya pazia kwa nyie kukataa kabisa kuoa?

Hii kampeni ya 'kijana kataa ndoa' ilianza kama masihara humu JF, ila saa hizi mpaka mitaani vijana wenye mafanikio wengi wanaitumia.

Wanazalisha tu wanalea watoto.

Hii kampeni inazidi kusambaa kwa kasi ya ajabu with time.

Vilio kwa akina dada navyo ni vingi na si haba.

Hebu tusemezane sasa leo vijana.
 
Mimi nitaoa siku nikiwa na nyumba, gari na hela nyingi, nasema hela.

Sitaki mke wangu au mtoto wangu asimame kwenye daladala.

Mambo yasipokuwa hivyo, basi tu, sababu kwetu tupo wengi na ndugu zangu washasababisha watoto wa kutosha.
 
sio kwamba vijana hawataki kuoa ila mabinti wasiotaka kuolewa ni wengi kuliko wanaotaka, trust me mabinti wengi wanaoolewa ni kwa sababu maisha yamewaendea kombo au kutafuta unafuu wa maisha, ni wachache ambao wameolewa kwa utayari wao wa kuwa ndani ya ndoa
 
Ndoa haingalii urembo na makalio makubwa ndoa inajumuisha vitu vingi sana ambavyo ukianza kuchambua na kuringanisha baina ya wanawake wa zamani na sasa utaona kuna utofauti mkubwa sana.Wanawake wengi wa sikuizi hawana maadili yaani kuna vitu unakuta mke wa mtu anavifanya kwa mumewe hadi unabaki unatikisa kichwa tu ni aibu bora kila mtu ashinde mechi zake.
 
sio kwamba vijana hawataki kuoa ila mabinti wasiotaka kuolewa ni wengi kuliko wanaotaka, trust me mabinti wengi wanaoolewa ni kwa sababu maisha yamewaendea kombo au kutafuta unafuu wa maisha, ni wachache ambao wameolewa kwa utayari wao wa kuwa ndani ya ndoa
Unaowaongelea wewe kuwa hawataki ndoa ni mabinti wa 15 mpaka 24... kuanzia hapo wengi wana sonona za kukosa ndoa
 
IMG_4468.jpg
 
Back
Top Bottom