Vijana mnaotafuta wake nendeni Jumapili kwa Mwamposa, wamejazana nyomi!

Ijuma Kareem ndugu zetu Waislamu na Heri ya siku hii pia kwa Wana-jamiiforums wote. Katika mihangaiko yangu ya kusaka 'ngawila' nimebahatika kufanya kazi na watu mashuhuri na wakubwa mbali mbali hapa nchini.

Miongoni mwa hao wakubwa basi Mwamposa na BM ni miongoni mwao. Ila naomba nijikite kwa huyu Mwamposa kwa muktadha wa huduma yake.

Kwa Jumapili siyo chini ya tatu nilizokwenda kanisani kwake pale Kawe, nimebahatika kukutana na MAMIA ya mabinti ambao wanakwenda kuomba wapate waume wa kuwaoa.

Mabinti wengi niliowakuta ni warembo, warefu wa vimo, wana maumbo ya kutamanisha, weupe na wana nyuso za furaha na ukarimu sana.

Sasa nikakumbuka humu kuna vijana wengi hawajaoa, sasa nikaona niwaambie vijana, jisogezeni pale Kawe mkajichagulie wanawake wa kuoa, hivi hamuwaoni wale pisi kali kwenye Arise And Shine TV kila Jumapili?

Yaani wanaume ni wachache sana mpaka watoto wazuri kama wale wanakosa wa kuwaoa. Aisee hali ni ngumu mno.

Achilia mbali hilo, hata mitaani huku wapo mabinti wengi tunaishi nao wanatafuta waume wa kuwaoa vijana mpo wapi? Mfano kuna binti ana gari, nyumba, elimu n.k, yeye anatafuta mume tu, mpaka kwa waganga ameshakwenda sana ili mambo yake yakae sawa.

Huyu binti hivi wakware hawamuoni? Vijana mnashindwa wapi nyie? Kawe kwa mwezi yaani Jumapili nne, zaidi ya pisi kali mia nne zinaripoti kutafuta waume. Zimekosa waume wa kuwaoa.

Zipambanieni zile pisi kali za Kawe vijana oeni wekeni ndani mpate familia. Mnaziangaliaje na kuziacha tu hivi hivi huku mkila kwa macho?
Wote hao ni misukule yenye kazi maalum.

Wajinga ndiyo waliwao.
 
Utakuja kubeba mke mwenye itikadi za hovyo na utayajutia Maisha yako, utakuja kubeba mke mgonjwa aliyeshindikana amekuja kutoa ushuhuda wa uongo kuwa amepona
Hili la ushuhuda wa uongo linakuwa kwa kasi sana siku hizi.
 
Shida sio kuoa au kutafuta ma binti, tatizo je mtaendana na tabia maana apo ndo kuna shida anaweza akawa na nyumba, magari na mengineyo ila tabia ikoje au usikute anamikosi alafu unaingia tu kichwa kichwa
 
Kwa wengi wa mabinti wanaokwenda huko ni reject personality au Misfits wa kwenye mahusiano. Wanajua mapungufu yao sasa hawapo tayari kuyabadili ila waporadhi kwenda kulia lia kanisani wakifanya maombi na kulilia muujiza wa kuonekena kwa wanaume na kuolewa ila in actually sense hapo ni time bomb inasubiria muda ufike kulipuka.

Hawa ndio mabinti ambao wanataka ndoa halafu wakishaipata wanaanza kuleta vimbwanga. Wao wanaamini kukosea ni sawa ila sio kujizingatia na kusimamia misingi ya maadili.

Unapokaa na mwanamke wa namna hii kila siku unakuwa na mtihani wa kumrekebisha, kumkemea kila siku.
 
Back
Top Bottom