Vijana mnaotafuta wake nendeni Jumapili kwa Mwamposa, wamejazana nyomi!

Wengi utamani kuolewa na wakishapata ndoa na watoto uanza bidii ya kuzibomoa ndoa zao, KWA kuleta ufeminist, wakishaachika uanza kushinda kwa waganga na Mitume na manabii kusaka mafuta ya urejesho wa ndoa.
Tunza ndoa YAKO huwezi jua umuhimu wake hadi ukiachika kisa mchepuko au ex ambao nao wakishapata habari umeachika nao lazima wakuache
 
Mabinti wengi pale wana matatizo aidha;
-mapepo sugu
-Kuachwa hovyo kwenye mahusiano
-UKIMWI
-Wapo kwenye mahusiano ila mwanaume hataki ndoa.
-Kutokuzaa n.k
Kama uko tayari kubeba hayo matatizo ruksa nenda
 
Ijuma Kareem ndugu zetu Waislamu na Heri ya siku hii pia kwa Wana-jamiiforums wote. Katika mihangaiko yangu ya kusaka 'ngawila' nimebahatika kufanya kazi na watu mashuhuri na wakubwa mbali mbali hapa nchini.

Miongoni mwa hao wakubwa basi Mwamposa na BM ni miongoni mwao. Ila naomba nijikite kwa huyu Mwamposa kwa muktadha wa huduma yake.

Kwa Jumapili siyo chini ya tatu nilizokwenda kanisani kwake pale Kawe, nimebahatika kukutana na MAMIA ya mabinti ambao wanakwenda kuomba wapate waume wa kuwaoa.

Mabinti wengi niliowakuta ni warembo, warefu wa vimo, wana maumbo ya kutamanisha, weupe na wana nyuso za furaha na ukarimu sana.

Sasa nikakumbuka humu kuna vijana wengi hawajaoa, sasa nikaona niwaambie vijana, jisogezeni pale Kawe mkajichagulie wanawake wa kuoa, hivi hamuwaoni wale pisi kali kwenye Arise And Shine TV kila Jumapili?

Yaani wanaume ni wachache sana mpaka watoto wazuri kama wale wanakosa wa kuwaoa. Aisee hali ni ngumu mno.

Achilia mbali hilo, hata mitaani huku wapo mabinti wengi tunaishi nao wanatafuta waume wa kuwaoa vijana mpo wapi? Mfano kuna binti ana gari, nyumba, elimu n.k, yeye anatafuta mume tu, mpaka kwa waganga ameshakwenda sana ili mambo yake yakae sawa.

Huyu binti hivi wakware hawamuoni? Vijana mnashindwa wapi nyie? Kawe kwa mwezi yaani Jumapili nne, zaidi ya pisi kali mia nne zinaripoti kutafuta waume. Zimekosa waume wa kuwaoa.

Zipambanieni zile pisi kali za Kawe vijana oeni wekeni ndani mpate familia. Mnaziangaliaje na kuziacha tu hivi hivi huku mkila kwa macho?
Acha maneno mengi leta namba ya huyo binti .
 
Pale ukienda kuna wanawake wa kila ina vimodo, wale wenye kazi zao, wenye shape na mizigo yao.

Ila kupata mke mwema pale ni sawa na kubet mkeka wa mechi 20 kwa jero, ila warembo wapo kibao.
 
Back
Top Bottom