Vijana mkipewa kazi fanyeni kazi. Inaumiza sana mnapewa kazi mnalipua kazi

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,610
Reaction score
59,577
Sina muda wa Salamu.
Nina hasira kichizi.

Wadau kuna hawa vijana wanaoingia na kutoka VETA huku mtaani wanafungua showroom zao za aluminium kufanya ufundi majumbani kufunga vioo kwenye madirisha.

Vijana mnapopewa kazi fanyeni kazi msilete utoto utoto na ujanja ujanja kwenye kazi ukipewa kazi hakikisha kazi imenyooka usiache kipengele chochote kwenye kazi, usipige konakona nyingi hio ni kazi kijana hio kazi inakujengea profile yako na usimfanye tajiri km fala mbumbumbu hajui kitu huyo tajiri ana wakaguzi wake wataikagua hio kazi.

Madogo wamepewa kazi wamelipwa full package yaani pesa yote mpaka na ya chakula njooni mfunge vioo kwenye madirisha. Vijana wakafika site wakaanza kufunga upande wa kwanza wa nyumba wamefanya vizuri marks 95% nikawapa.

Vijana walipohamia upande wa pili wakalipua kazi upande wote kioo ukisukuma mpaka utumie nguvu nusu kujichana mikono nusu kukipasua marks 0% kabisa.

Sasa Vijana km hawa wanapewa kazi wanalipua kazi wanataka kazi kweli? Unawapa kazi wafanye kazi vijana wanalipualipua tu kazi wanaondoka wakidhani kwamba tajiri hatokagua kazi.

Mbaya zaidi tajiri unawafuata kwa upole kabisa unawaambia vijana mmeharibu kazi kule emu njooni mrekebishe wanajibu sawa tajiri tunakuja kurekebisha sababu ya upole wa tajiri na mizunguko mingi aliyonayo vijana hawaji kurekebisha, anarudi kuuliza vijana walikuja anaambiwa vijana hawakuja kurekebisha zinapita siku 2 vijana hawataki kurekebisha kazi na pesa wamekula, vijana mnachezea kazi?

Hivi vijana hamjui kwamba unapofanya kazi nzuri kwa viwango kitaalamu yaan professional inakutengenezea uaminifu wa kazi zingine, wigo mpana wa kazi na inakujengea mtandao mzuri wa kupata kazi nyingine zaidi?

Kwanini mnachezea kazi vijana? Mnapewa kazi mnachezea kazi vijana kwanini? Kwanini mkipewa kazi mnacheza na kazi mnalipua kazi hamfanyi kazi kwa viwango vinavyotakiwa kwanini vijana mnachezea kazi?

Jirekebisheni vijana usicheze na kazi, ukipewa kazi fanya kazi tena nyoosha kazi iwe na viwango sio unalipualipua tu kisha unaondoka.
 
Madogo wamepewa kazi wamelipwa full package yaani pesa yote mpaka na ya chakula njooni mfunge vioo kwenye madirisha. Vijana wakafika site wakaanza kufunga upande wa kwanza wa nyumba wamefanya vizuri marks 95% nikawapa.

Nimeelewa wamelipwa ZOTE kabla ya kazi KUANZA/KUMALIZIKA.

📌📌📌KOSA KUBWA SANAAAAAA ULIFANYA. liwe funzo hata kama mtu unapesa ya kumwaga.
 
Pole sana mkuu na hilo ndio tatizo letu vijana wengi, sijui huwa umakini unapotelea wapi.

Ukikubali kufanya kazi ya mtu hata kama haina maslahi mazuri ifanye vyema na sio kulipua, kama ulijua haina maslahi bora usingekubali kufanya hiyo kazi. Na hii ni namna nyingine bora kabisa ya kulinda brand na ubora wako.

Kazi nzuri inakutangaza na vice versa is true.
 
Ndio kabisa sasa nimeshangaa vijana wamelipwa vizuri kisha wanalipua kazi hawa vijana wanataka nini sasa?
 
Kosa kubwa! Always aliyeshika pesa ndio mwenye pawa
Kosa sio kuwalipa mapema kosa ni kuwajali maana na chakula wamelipwa vijana bado wanalipua kazi? Unalipwa pesa yako ya kazi, unalipwa nauli, unalipwa na chakula bado unalipua kazi una akili wewe kijana kosa ni kukujali?
 
Kulipa vizuri ndio kulipa shilingi ngap bwashee?
Pesa uliyosema ulipwe ndio kiwango cha kulipwa vizuri plus bonus zangu za chakula na nauli umechoma mafuta kuja kufanya kazi hapo hujalipwa vizuri? Bado hujanywa bia za bure nimelipa mimi bado sijakulipa vizuri? Fanyeni kazi vijana acheni konakona kwenye kazi mnalipualipua tu kazi mnatia hasira sana
 
Acha kutumia mafundi maiko tafuta mainjinia wa hiyo kazi mpatane tajiri
 
Hao wanataka ubaya, next time ukimpa kazi mtu mwingine waanze maneno ya hovyo.
Mkuu inauma sana, mbaya zaidi ni vijana hicho ndicho kinachouma zaidi kinauma sana mkuu usichukulie poa kabisa unawajali vizuri still bado wanalipua kazi kweli? Mara 100 wangekua wazee ningesema labda hawana nguvu sababu ni wazee lakini hawa ni vijana wana nguvu bado wanalipua kazi kweli?
 
Acha kutumia mafundi maiko tafuta mainjinia wa hiyo kazi mpatane tajiri
Sio mafundi maiko mkuu hivi hawa vijana wanaoenda na kurudi VETA si wanafungua ofisi huku mtaani au wanafungua ofisi Mbinguni?
 
Sio mafundi maiko mkuu hivi hawa vijana wanaoenda na kurudi VETA si wanafungua ofisi huku mtaani au wanafungua ofisi Mbinguni?
Pole mkuu , wapeleke mahakamani kama mliingia nao mkataba wa kazi kisheria.
 
Pole mkuu , wapeleke mahakamani kama mliingia nao mkataba wa kazi kisheria.
Issue sio mkataba wa kisheria hapa ninachozungumzia mimi ni vijana kufanya kazi kwa weredi na kujituma sio kulipualipua tu kazi, najua humu wapo vijana wengine wa namna hio hata huko maofisini ndio nimekuja kuwakumbusha wasicheze na kazi wafanye kazi, kijana fanya kazi hio kazi inakujengea profile usicheze nayo nyoosha kazi sio unalipualipua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…