RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,580
- 122,468
Jana jioni nilikuwa nafanya mazoezi(jogging) nikapita barabara moja kuna ghorofa linajengwa.
Nikasikia kijana mmoja (27-30yr) anafoka na kutukana kwenye simu.
'WEWE MZEE SIKU YA PILI LEO NAFIKA HAPA UMEACHA LINDO. HUO UZEE WAKO MIAKA 70 ISIWE KIGEZO KUTUSUMBUA. KAMA ULITUMIA HELA ZAKO VIBAYA UJANANI USITULETEE... Duh nilishtuka sana nikaishia zangu.
Aisee inawezekana kweli mzee kakosea ila kuna njia nzuri ya kuongea na mtu mzima au mfanyakazi wako na sio lugha kama hizo. Kijana mdogo namna ile kumtukana mzee ambae anaweza kuwa baba au babu yake si sawa. Kuna laana nyingine za kujitakia. Vijana kuweni na busara.