ngome1838
JF-Expert Member
- Feb 20, 2019
- 2,027
- 2,496
Hakuna pasipo na connection katika jamii ya wanadamu ila kama ni story za kwenye kahawa kwa mzee kibusha endelea na story.Hi hope mko poa Sana.
Nimeshangaa kuona kijana mmoja eti anataka kutoa 500K kwa kiongozi Fulani ngazi ya wilaya eti atamsaidia kupata kazi Tamisemi.
Yaani huu ujinga wa vijana wa siku hizi ni hatari, wengine wanatoa 50K kwa mkuu wa Shule ili awaandikie Barua za kujitolea eti ndo watapata ajira.
Vijana acheni Ujinga, Tamisemi hakuna Rushwa, watu wanatenda haki hakuna vya Connection Wala Nini, hata mtoto wa waziri hawezi penyezwa kijinga.
Badirika