Nyimbo za kwenye vitabu vya siku hizi mbona hatujui zinaimbwaje

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,220
2,825
Nimejaribu kufuatilia nimegundua pamoja na maendeleo makubwa ya sasa na njia za mawasiliano kuboreshwa, bado kuna kitu watu wa elimu wameyumba sana.

Zamani vitabu viliandikwa vinyimbo nyimbo na takribani kila sehemu uliyokwenda ungekuta watu wanajua toni ya wimbo husika lakini siku hizi mavitabu yamejazwa nyimbo toni za kuimbia hatuzijui basi tunaskip tu katika ufundishaji.

Shughulikieni hilo jambo watu wa elimu, mwandishi/mtunzi wa wimbo atoe sauti za kuimbia wimbo wake kisha isambazwe mashuleni kazi iwe nyepesi maana siyo wote tuna ubunifu wa kisanii kusema kwamba nikiona tu wimbo niutungie sauti ya kuimbia


Acha nijikumbushe
🎵Tola njaa ipo muda mrefu, ... Tola mmh mmh🎶

🎵Upepo ukavuma twainama, twainama hatuvunjiki🎶

🎵Barua ikija, aitembeza kutwa🎶
 
Back
Top Bottom