BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,117
Serikali kitanzini
na Mwandishi Wetu
Tanzania daima
VIGOGO kadhaa waliyatumia maadhimisho ya miaka minane tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere jana, kuinyooshea kidole serikali, wakiituhumu kwa kufanya mchezo na vita dhidi ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi.
Aliyeonekana kutoa maneno makali kuliko wote, ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, ambaye akizungumza wakati wa kufunga kongamano la kumkumbuka Nyerere huko Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alibainisha kuwa rushwa inazungumzwa sana hivi sasa lakini hakuna mtu anayethubutu kuchukua hatua.
Alisema yanayotokea sasa ni tofauti ya yaliyotokea miaka kadhaa iliyopita, akikumbusha kuwa katika miaka ya 1990, wakati serikali ilipokabiliwa na tuhuma nzito kuhusu rushwa, rais wa wakati huo, Ali Hassan mwinyi, aliamua kulivunja Baraza la Mawaziri.
Alisema kuwa alipoliunda upya, rais Mwinyi alibakisha mawaziri wa zamani saba tu, jambo ambalo lilimwezesha; kuanza upya' kuisuka serikali yake ifanye kile kilichokuwa kikipendekezwa na watu wengi.
Alisema hali hiyo ilibadilika baada ya Mwinyi kuondoka madarakani, kwani rais aliyemfuatia, Benjamin Mkapa, licha ya kuunda Tume ya Warioba, kuchunguza masuala ya rushwa, matokeo ya tume hiyo yamesababisha zaidi ugomvi badala ya kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa.
Ingawa hakufafanua kuhusu kauli yake hiyo, lakini uzoefu unaonyesha kuwa hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kutokana na mapendekezo yaliyokuwamo katika ripoti ya tume hiyo.
Akizidi kumchambua Mkapa, Butiku alisema kuwa hivi sasa rais huyo, ambaye katika harakati za kuwania nafasi hiyo alijulikana kama; Bwana Msafi' (Mr Clean), anakabiliwa na tuhuma nzito za kufanya biashara akiwa Ikulu, lakini inashangaza kuona kuwa ameamua kukaa kimya.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa aina ya Butiku, kujitokeza hadharani na kutaka rais huyo mstaafu ajitokeze kujibu tuhuma hizo. Butiku alitoa kauli hiyo, akiijenga chini ya msingi kuwa kimya kinachoonyeshwa na Mkapa, kinaweza kutumiwa na viongozi wengine kujenga utamaduni wa umangimeza.
Akionekana kuiweka serikali ya sasa kitanzini, Butiku alibainisha kuwa rushwa inazungumzwa sana hivi sasa lakini inashangaza kuona kuwa hakuna mtu au taasisi inayochukua hatua za dhati kukabiliana na hali hiyo.
Alisema kuwa kuna viongozi ambao wanatajwa kwa tuhuma za ufisadi na inashangaza kuwa badala ya tuhuma hizo kufanyiwa kazi, serikali inakuja na kauli zinazojikanganya kwa kugonganisha maneno.
"Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa nchi inanuka rushwa, alikuwa CHADEMA? Hivi sasa tunashuhudia tuhuma nzito dhidi ya viongozi; serikali ichukue hatua na kutoa majibu sahihi. Masuala ya rushwa si ya vyama," alisema Butiku.
Butiku alikwenda mbali zaidi na kuzidi kuibana Serikali ya Awamu ya Nne kwa kubainisha kuwa uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2005 ulitawaliwa na rushwa.
"(Makamu Mkuu wa UDSM) Profesa Mukandala ulikuwepo. Hukuona rushwa? Katika dakika za mwisho Mwalimu alisema rushwa ni donda ndugu, mimi nasema ni unfinished business (jambo ambalo halijamalizwa)," alisema.
Akikumbusha hatua zilizochukuliwa na rais Mwinyi, Butiku aliihimiza serikali kuchukua hatua akisisitiza kuwa katika masuala ya rushwa ambayo imefikia viwango vilivyopo nchini, mtu ahitaji ushahidi ili kuchukua hatua zinazopaswa.
Alisema kuwa amemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete kuhusiana na masuala hayo, ingawa hakueleza hadharani ni nini hasa kilichomo ndani ya barua hiyo.
Butiku ametoa kauli hiyo huku serikali ikionekana kana kwamba inafanya mchezo wa kuigiza kuhusiana na tuhuma zilizotolewa dhidi ya viongozi wake, wakituhumiwa kwa ufisadi.
Tuhuma hizo zilizotolewa na wapinzani, zimesababisha viongozi kadhaa wa serikali na CCM, kujitokeza hadharani kwa kile wanachodai kuwa ni kuzijibu, huku wakitoa kauli ambazo si tu zinatofautiana, bali zinakinzana katika masuala kadhaa.
Kiongozi mmoja aliwahi kunukuliwa akisema kuwa serikali haitajihangaisha kuzunguka mikoani kujibu tuhuma hizo kama walivyofanya wapinzani kuzunguka mikoani kuwaelezea wananchi kuhusiana na madai ya ubadhirifu.
Lakini siku moja baadaye, kiongozi mwingine aliibuka na kudai kuwa viongozi wa CCM watajipanga na kuanza ziara katika mikoa yote ili kujibu tuhuma hizo za wapinzani.
Mpango huo wa CCM ulidakwa na serikali, ambayo iliwatuma mawaziri wake katika makundi mikoani, wakiungana na makada kadhaa wa CCM wakijibu tuhuma dhidi ya viongozi wa serikali na chama.
Aliporejea kutoka ziara yake ya wiki tatu nchini Marekani, Rais Kikwete, akihutubia katika mkusanyiko wa kidini huko Arusha, alisema kuwa serikali inachunguza kila tuhuma inayotolewa, na kuleta mkanganyiko zaidi, hasa ukizingatia kauli za awali za viongozi wengine zilizolenga kuonyesha kuwa madai hayo ya wapinzani ni upuuzi.