Vigogo wa Kenya marufuku Uingereza

Mtu

JF-Expert Member
Feb 10, 2007
469
43
Waziri mmoja katika serikali ya Kenya na mshirika wa karibu wa rais Mwai Kibaki amepigwa marufuku kuingia Uingereza kwa madai ya rushwa, ikiwa ni siku chache kabla ya uchaguzi mkuu.

Ubalozi wa Uingereza mjini Nairobi umeyafahamisha mashirika yote makubwa ya ndege kutomchukua waziri wa mazingira David Mwiraria na wengine watatu wasiingie Uingereza.

Mbunge mwingine mwandamizi, Nicholas Biwott, mshirika mwingine wa Kibaki, pia yupo kwenye orodha.

Uingereza imekanusha madaia kwamba inaingia uchaguzi wa nchi hiyo, ambapo rais Mwai Kibaki anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Raila Odinga.

Wengine waliopigwa marufuku hata kufika katika viwanja vya ndege vya Uingereza ni wafanyabiashara, Sanjay Kumar Ramniklal na Manoj Ramniklal Panacha Shah.

Visa za watu hao wanne zimefutwa.Msemaji wa serikali Alfred Mutua amekataa kuzungumzia swala hilo.

Siasa

Bw Mwiraria anagombea kiti cha ubunge kupitia chama kinachoongozwa na Bw Kibaki cha Party of National Unity.

Aliwahi kujiuzulu wadhifa wa waziri wa fedha baada ya kuhusishwa na kashfa ya Anglo-Leasing mwaka 2006, lakini aliteuliwa tena mapema mwaka huu.Amekuwa akisema madai dhidi yake hayana ukweli wowote.

Mwaka 2005, aliyekuwa waziri wa usalama, Chris Murungaru, alikumbwa na adhabu kama hiyo ya kupigwa marufuku kuingia Uingereza.

==========
Source BbcSwahili

Jk angepewa ban hii ingependeza sana!
 
Back
Top Bottom