Je, unafahamu kwamba Mr Bean alisoma shule moja na aliyekuwa waziri mkuu wa uingereza, bwana Tony Blair?

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,543
14,455
Maarufu kwa jina la Mr bean lakini jina lake halisi ni Rowan Atkinson. Aliyezaliwa siku ya tarehe 6 Jan 1955 huko nchini uingereza..

Je, unafahamu kwamba Mr Bean alisoma shule moja na aliyekuwa waziri mkuu wa uingereza, bwana Tony Blair?. Ndio, tena walisoma darasa moja katika shule ya Durham Choristers.

Kitaaluma, Mr Bean ni mhandisi, akichagua kusomea fani aliyosoma baba yake mzazi, ambaye pia ni Engineer. Alihitimu shahada ya uzamili katika chuo cha oxford, uingereza.

Lakini hakutaka kwenda kutumikia fani yake ya uhandisi wa umeme, bali aliamua kuingia kwenye sanaa ya vichekesho. Kabla ya kuitwa Mr Bean, alikuwa akitumia jina la Mr White, baadae alibadilisha na kuwa Mr Cauliflower.

Je, unajua kwamba Mr bean ametokea kwenye movie ya James Bond iliyochezwa na Sean Connery inayojulikana kwa jina la "Never Say Never Again" ya Mwaka 1983?!.. Humo, Mr Bean aliigiza kwa jina la 'Nigel Small-Fawcett'.

Mwaka 2001, Mr Bean pamoja na familia yake walikuja nchini Kenya. Wakiwa kwenye ndege aina ya 'Cessna 202 aircraft' iliyokuwa inatoka Ukunda kuelekea Nairobi, aliyekuwa rubani wa ndege hiyo 'alipoteza fahamu'. Ndipo Mr Bean aliamua 'kushika usukani' kuongoza ndege hiyo, hadi pale rubani alipoamka. Ruban alipoamka aliendelea kuongoza ndege hadi ilipofika pale Wilson Airport, Nairobi.

Hivyo, Mr Bean alifanikiwa kuokoa maisha yake na familia japokuwa hakuwahi kuendesha ndege hata siku moja.

Yeye na mkewe, Sunetra Sastry , walifunga ndoa mnamo Mwaka 1990 na kufanikiwa kupata watoto wawili, Benjamin na lily. Lakini ilipofika mwaka 2015, Mr Bean alitalikiana na mkewe.

Naam, hayo ndiyo machache kuhusu Rowan Aktinson, maarufu kama Mr Bean mwenye utajiri wa dola za kimarekani $130 milioni.
 

Attachments

  • IMG_20231222_120156_706.jpg
    IMG_20231222_120156_706.jpg
    14.5 KB · Views: 4
Moja ya interview zake ni ile waliyojibizana na yule jamaa aliyeimba sacrifice (Elton john) na wakawa wanabishana kuhusu kubadili jina......😄😄😄😄
 
Nilisikiasikia muda kidogo kafariki, nimegugoole kafariki, unajibu usichokijua kisa, misifa au kuonekana umechanjia upopoma, punguza mihemko na shobo mshindo isiyo na tija.
Mbona maneno makali bila sababu?
Jibu kistaarabu ili kama umekosea upewe somo.
 
Back
Top Bottom