Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Hii ni thread ya vifurushi ambavyo sio rasmi kama vya chuo au vifurushi maalum ambavyo vinatoa kiasi kikubwa cha internet, nitalist vifurushi ninavyovifahamu kama kuna wanaojua vyengine watasaidia

Tigo
-1gb kwa shilingi 600

Nunua vocha ya 1000 halafu ingiza mfumo huu *104*namba ya vocha*03# watakukata shilingi 600 na utapewa 1gb ya internet

-Vifurushi vya chuo

Hivi utapata mb na dakika kwa pamoja ila nitaandika tu mb, shilingi 1500 mb500 kwa wiki na sh500 ni mb300 kwa wiki. kujiunga bonyeza *148*01*20# au bonyeza *148*00# kisha chagua vifurushi maalum, itabidi uwe na line ya chuo

Vodacom

-3gb kwa sh 2000 au 800mb kwa sh 1000
Bonyeza *149*03# kupata hivi vifurushi, kutegemeana na line utapata kifurushi kimoja kati ya hivyo
-Vifurushi vya chuo
Kwa sh 500 utapata mb500, 1500 utapata 1gb na 2500 utapata 2gb zinazodumu wiki nzima, kujiunga piga *149*42#

Airtel
-Vifurushi vya chuo
Hawa jamaa wana vifurushi vizuri zaidi vya chuo hasa cha usiku ambacho unapata 10gb kwa sh 600, pia kipo cha kawaida unapata 2gb kwa 1000 na 1.2gb kwa sh600. Kuvipata unahitaji kununua vocha za chuo zinazopatikana vyuoni au kutumia airtel money *150*60# kisha uchague ofa kabambe nafkiri option ya 6.

Halotel
-Vifurushi vya chuo

Hawa wana kifurushi kizuri cha chuo cha mwezi sh 10,000 unapata 10gb ni kizuri kwa wasiopenda usumbufu wa kuunga unga vifurushi, pia kipo cha wiki sh 500 mb600, kujiunga *148*55#
-Usiku 10g kwa sh 1500
Pia kipo kifurushi cha usiku kwa wale ambao airtel haina speed kwao, kujiunga *148*66# kisha utaenda upande wa internet.

TTCL
-Boom pack (vya chuo)

Kwa shilingi 500 utapata 500MB, shilingi 1500 1gb na shilingi 2500 3gb
pia wana vifurushi vya mwezi kwa sh 1500 utapata 2gb, 3000 utapata 4gb na shilingi 5000 utapata 7GB

kujiunga *148*30#
vifurushi vya usiku
kwa shilingi 1000 utapata gb 10 za 4g kuanIa saa 4 usiku hadi 12 asubuhi, kujiunga ni menu ile ile ya *148*30#.

Smart
-Unlimited bundle
Kwa siku unlimited 1,000 kwa wiki 7,000 na kwa mwezi 20,000 tuma neno DATASIKU au DATAWIKI au DATAMWEZI kwenda 100, vifurushi hivi ni kwa watu walio nje ya dar tu


Vifurushi vya youtube
Zipo website nyingi sana wanahost movie youtube, unaweza jiunga kifurushi cha youtube kisha ukatembelea hizo site na kudownload, sema utahitaji bundle nyengine ya kubrowse na bundle ya youtube ya kudownloadia. vipo kila mtandao.

Kuna kifurushi unaona kinastahili kuwa hapo? usisite kukitaja chini.

Remote
Hebu nipe maelezo kidogo chief mkwawa kwe hicho cha voda chenye 3gb kwa buku 2
 
ni kwa baadhi ya watu, bonyeza *149*03# kama hukioni ujue kwako hakipo.

Nijuavyo mimi hicho cha voda inategemea na umenunua kwa muda gani bundle zao ..kwa kuanzia wanakuu tsh500 kwa 300mb ukiwa unanunua sana ndio wanaku-upgrade na kua kwenye hizo categories nyingine.
 
Nijuavyo mimi hicho cha voda inategemea na umenunua kwa muda gani bundle zao ..kwa kuanzia wanakuu tsh500 kwa 300mb ukiwa unanunua sana ndio wanaku-upgrade na kua kwenye hizo categories nyingine.
kuna mtu hapa anaunga cha buku mb 800 kila siku, hakijawahi kubadilika hata siku 1
 
Back
Top Bottom