Watu wanaolalamikia internet kufosi Starlink mbona Voda, airtel wana unlimited nzuri kwa 120,000 tu kwa mwezi

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,877
6,291
Habari wadau.

Binafsi nawashangaa sana watu wanaolalamikia kwa nini star link haipo?

Chief-Mkwawa amelinganisha vizuri kuhusu bei za internet ya starlink vs bei za ISP wa bongo.

Bei za unlimited bongo now Airtel 70,000, TTCL 55,000, Vodacom 120,000, Zuku 69,000, Raha 50,000, Netsolution, 60,000, Tigo 70,000 etc. Je hizi bei sio rafiki ila Starlink ambayo Gharama za Manunuzi ni zaidi ya Milioni na bei ya mwezi ni 100,000-240,000 basic na zaidi ya laki 3 kwa Unlimited speed Business. Je ni rafiki bei zao?
 
Asee sababu kubwa starlink inashika kila mahali ila hio mitandao ya simu nikanjanja sana asee mfano mimi natumia ya voda nikienda bagamoyo no network inakua aifanyi kazi kabisa.. tuachane na hilo dar hapa hapa kuna mahali nilipanga hakuna mtandao kabisa yanj mpka utoke nje au utegeshetegeshe router ndo upate mtandao hivo naweza sema internet bora kabisa ni fibre tu ila si haya makampuni ya simu.
 
Mzee ile Starlink ni konyo..Wewe uko town ila kuna maeneo hapa TZ ni Town au nje ya mji kidogo tu ila Network ni taabu sana kuipata kwa Mitandao yetu hii...Ila Starlink ni Mwisho wa Matatizo inanasa mpaka Vijijini na Vitongoji vyooote Dunia hii...

Unlimited za mitandao yetu unapata sijui 20mbps ikizidi sana 90mbps labda Usiku ndo inafika 100+ ila Starlink mchana tu inagonga 200mbps hapo ndo iko vibaya sana

UNLIMITED zetu mkiunganishwa watu 10+ tu inapata wenge na kuslowdown ILA Starlink inauwezo wa Kuimili watu 200+ na wote mkapata network ya kasi

Itoshe kusema Huwezi kufananisha Starlink na Network ya Voda,Airtel n.k Elon Mushi kafanya mapinduzi makubwa sanaa
 
yani kilichopo nyumbani bei si rafiki na mzawa si bora kuchukua starlink .kwa unafahamu speed ya starlink ni kubwa 10gb unadownload dakika 2 tu
 
Mzee ile Starlink ni konyo..Wewe uko town ila kuna maeneo hapa TZ ni Town au nje ya mji kidogo tu ila Network ni taabu sana kuipata kwa Mitandao yetu hii...Ila Starlink ni Mwisho wa Matatizo inanasa mpaka Vijijini na Vitongoji vyooote Dunia hii...

Unlimited za mitandao yetu unapata sijui 20mbps ikizidi sana 90mbps labda Usiku ndo inafika 100+ ila Starlink mchana tu inagonga 200mbps hapo ndo iko vibaya sana

UNLIMITED zetu mkiunganishwa watu 10+ tu inapata wenge na kuslowdown ILA Starlink inauwezo wa Kuimili watu 200+ na wote mkapata network ya kasi

Itoshe kusema Huwezi kufananisha Starlink na Network ya Voda,Airtel n.k Elon Mushi kafanya mapinduzi makubwa sanaa
Mkuu naipataje hapa TZ?

Sababu naona hazijawa official bado.
 
Asee sababu kubwa starlink inashika kila mahali ila hio mitandao ya simu nikanjanja sana asee mfano mimi natumia ya voda nikienda bagamoyo no network inakua aifanyi kazi kabisa.. tuachane na hilo dar hapa hapa kuna mahali nilipanga hakuna mtandao kabisa yanj mpka utoke nje au utegeshetegeshe router ndo upate mtandao hivo naweza sema internet bora kabisa ni fibre tu ila si haya makampuni ya simu.
Sahihi issue Sio kutangaza tu biashara shika simu safiri ndio utajua hayo makampuni utapeli mtupu Kuna maeneo unafika njiani hakuna Cha mtandao wowote unasoma na kifururushi ukichoweka mfano Cha masaa hawahali kuwa hayo maeneo mtandao wao hausomi na network hawana wanahesabu masaa tu yakifika kakifurushi kameisha wakati hayo maeneo Hata mtandao haupo wanahesabu masaa tu ya kifurushi

Wezi sana

Inakuwaje uko eneo hawana mtandao na wao Wana uhakika hawana halafu wanakata pesa za vufurushi ulivyonunua eneo Wana mtandao ambavyo havijaisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom