Vifo vya Samaki Mto Mara: Mgodi wa Dhahabu wa North Mara wakanusha kuhusika na uchafuzi wa maji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Baada ya kuwepo kwa tetesi juu ya uwepo wa kemikali za sumu kwenye maji ya Mto Mara ambapo imesababisha samaki kufa na maji kuwa meusi, Mgodi wa Dhahabu wa North Mara umekanusha kuhusika katika uchafuzi wa maji ya mto huo.

Hili hapa tamko kamili...

****

Mgodi hauhusiki na uchafuzi wa maji ya Mto Mara

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, umepata taarifa za tuhuma zinayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utiririshaji wa zebaki kwenye Mto Mara. North Mara imebainisha mbali na eneo husika kuwa umbali wa kilomita 80-85 chini ya mgodi, zebaki si sehemu ya orodha ya vitendanishi vya mgodi huo wala haitokei kiasili katika eneo hilo na hivyo basi, kama kuna zebaki yoyote iliyopatikana katika mto haiwezi kuhusishwa na mgodi.

Meneja wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa amesema Mamlaka ya Bonde la Maji ya Ziwa Victoria mara kwa mara imekuwa kichukua sampuli za maji katika maeneo yaliyo jirani na migodi na mgodi wenyewe una mpango madhubuti wa ufuatiliaji wa maji ya ardhini na hakuna ushahidi wa kuwepo zebaki au uchafu mwingine wowote kwenye maji ndani au karibu na maeneo ya uzalishaji.

Aidha, Serikali ya Tanzania iliunda timu ya wataalamu inayoongozwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ili kuhakikisha hakuna uchafuzi wa mazingira au maji unaotokea katika mgodi huo na katika maeneo yanayouzunguka.

Mgodi pia umefikia lengo muhimu la uhifadhi wa taka zitokanazo a mchakato wa uchenjuaji wa madini kwa kupunguza kiasi cha maji yaliyohifadhiwa kwa kiasi kikubwa kutoka mita za ujazo milioni 7 hadi mita za ujazo 800,000 ndani ya kipindi cha miaka miwili, kama ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Maelewano na NEMC. Haya ni mafanikio makubwa, ambayo yanaonyesha zaidi dhamira na jitihada za Mgodi wa Dhahabu wa North Mara zinakwenda sambamba kwa kuhakikisha hakuna uchafuzi wa maji au mazingira kwenye Mgodi na maeneo yanayouzunguka.

*****

Pia soma
 
Sasa kama wameisha toa rushwa kosa lao liko wapi waacheni wapige kazi bhana
 
Kwanini hawahusiki?
Inawezekana huna uelewa hata kidogo kuhusu masuala ya uchenjuaji madini.

Hata bila ya kukanusha, kwa mtu tetote mwenye uelewa, hahitajiki hata kuambiwa, kuna uwezekano sifuri wa mgodi wa North Mara kusababisha vifo vya samaki myi Mara, mti ulio kilenra zaidi ya 80, na huku kukiwa hakuna vifo maeneo ya karibu. Hiyo sumu ilikuwa inatembea hewani?

Tatizo Watanzania walio wengi ni wajinga katika mambo mengi lakini wanajifanya wajuaji wa kila kitu. Mgodi ambao umezungukwa na piezometric environmental monitoring drill holes zaidi ya 50, underground water haina contamination, halafu contamination ikaonekane kwenye mto zaidi ya 80km!! Maajabu makubwa.

Halafu, watu wanadai kuna mercury, wakati inafahamika kuwa hakuna mgofi wowote mkubwa Duniani unaotumia mercury, sasa North Mara wakapeleke mercury North Mara river, wakiwa wameitoa wapi?

Kama kweli kuna mercury contamination, ina maana imetoka kwenye machimbo ya wachimbaji wadogo, ambao ni Watanzania wenzetu ambao hawazingatii kanuni za utunzaji wa mazingira.
 
Ngumu kuwaamini.

#MaendeleoHayanaChama
Kama huna uelewa wa mambo haya, wasikilize wenye uelewa. Hakuna binadamu anayeelewa kila kitu.

Mimi kama mtaalam wa sejta hii, tena katika kiwango cha juu kabisa, nikiwa nimefanya kazi mabara ypte except Asia, kama samaki walionekana wamekufa mto Mara, contamination ya maji ya mto ni dhahiri. Ni contamination gani, imetokana na nini, imetokea wapu, imeufikiaje mto Mara, ni masuala yanayoweza kujibiwa na uchunguzi.

Lakini kwa vyovyote, chamzo hakiwezi kuwa North Mara Mine. Mgodi upo mbali sana toka uliko mto. Hakuna uwezekano sumu zitoke North Mara mine, ziruke maeneo yote, zikaufikie mto North Mara ambao line distance ni 80km, umbali wa channels za kusafirisha pollutants kwa vyovyote ni zaidi ya 150km, halafu kote zilikopita kusiwe na madhara, madhara yakachomoze mto Mara.

Chemicals zote zinazotumika kwenye migodi mikubwa zinafahamika, na zinaidhinishwa na Serikali, uingizaji na matumizi yake, vinakuwa monitored na Serikali. Sasa, ni chamical gani iliyopatikana kwenye huo mto inayotumika na North Mara?
 
yule jamaa aliye anzisha uzi humu jamvin wa kuutuhumu mgodi wa north mara kwa kuchafua mto mara nilimuuliza ni aina gani ya sumu anayo 'tegemea' kuikuta kwenye mizoga ya samaki, akasema puff, cyanide, mercury, caustic soda, lime…….. yaani nikaishia kumdharau kabisa!
 
Kama huna uelewa wa mambo haya, wasikilize wenye uelewa. Hakuna binadamu anayeelewa kila kitu.

Mimi kama mtaalam wa sejta hii, tena katika kiwango cha juu kabisa, nikiwa nimefanya kazi mabara ypte except Asia, kama samaki walionekana wamekufa mto Mara, contamination ya maji ya mto ni dhahiri. Ni contamination gani, imetokana na nini, imetokea wapu, imeufikiaje mto Mara, ni masuala yanayoweza kujibiwa na uchunguzi.

Lakini kwa vyovyote, chamzo hakiwezi kuwa North Mara Mine. Mgodi upo mbali sana toka uliko mto. Hakuna uwezekano sumu zitoke North Mara mine, ziruke maeneo yote, zikaufikie mto North Mara ambao line distance ni 80km, umbali wa channels za kusafirisha pollutants kwa vyovyote ni zaidi ya 150km, halafu kote zilikopita kusiwe na madhara, madhara yakachomoze mto Mara.

Chemicals zote zinazotumika kwenye migodi mikubwa zinafahamika, na zinaidhinishwa na Serikali, uingizaji na matumizi yake, vinakuwa monitored na Serikali. Sasa, ni chamical gani iliyopatikana kwenye huo mto inayotumika na North Mara?
Unataka kuwadanganya wakina nani..kwamba mto mara upo umbali wa zaidi 80km kutoka mgodi wa NM.?

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom