Vifo vilivyoniumiza JF

Vifo vilivyoniumiza JF

Inasikitisha sana na kuumiza moyo unapofikiria pengo waliloliacha.

Kila jina na kila ID iliyozimika ghafla inabeba simulizi ya ndoto zilizokatika katikati ya safari, ikitukumbusha jinsi maisha ya mtandaoni yanavyoweza kugeuka kuwa kumbukumbu ya kudumu yenye majonzi mazito.

Mistari yao ya mwisho ya michango bado imesamaa jukwaani, ikisomeka kwa sauti ya upole lakini yenye mwangwi wa simanzi, kana kwamba walijua walikuwa wanaaga.
Kupita kwenye nyuzi zao za zamani ni kama kutembea kwenye makaburi ya kidijitali; kila neno waliloandika linachoma moyo, likiacha swali lisilo na majibu juu ya unyonge wa mwanadamu na ukweli kwamba hatutawahi kusikia tena maoni yao mapya.

Pengo lao halitafutika, na kila ukurasa wa JamiiForums utabaki na alama za vidole vyao vya kifikra ambavyo sasa vimetulia milele mavumbini. Tunatamani kuwatajia wale waliogusa zaidi hisia zako
 
Namkumbuka Ben Saanane. Siwezi kuzungumza sana kuhusu yeye. Lakini haipiti siku, sijafikiria juu yake. Popote ulipo Ben, nakukumbuka rafiki yangu.

Namkumbuka Le Mutuz (R.I.P). Watu wengi walimfahamu kupitia emage yake ya mitandao. Lakini kiuhalisia nje ya mitandao, William alikuwa ni mtu mpenda watu, mcheshi na sio mchoyo wa fursa.

Warumi (R.I.P), alikuwa mshikaji wangu pia hapa jamvini. Very sad!

Mshana Jr, umenikumbusha mbali jamaa yangu. JF inakuwa burudani zaidi kwa uwepo wako mkuu. Mada zako zinaleta "engagement" kwa members wengi. Hongera sana.
 
Chivundu maisha yetu duniani si milele😪 kuna siku sitakuwepo. Kitakachobaki ni haya maandishi😭
 
Back
Top Bottom