Kuna taarifa kuwa mwezi mmoja tu baada ya wanafunzi wa kidato cha sita kuanza mafunzo ya JKT tayari vifo vimeripotiwa.
Kifo cha wiki mbili zilizopita ni tukio lililotokea katika kambi ya JKT Oljoro iliyopo Arusha ambapo inasemekana binti kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro alifariki dunia kwa Pneumonia baada ya kukataliwa matibabu.
Hapo hapo Oljoro kijana mwingine amepigwa na afande na kuvunjwa mbavu na amelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Matukio haya yanatufadhaisha sana wazazi na kutujengea hofu kuhusu aina ya treatment wanazopewa watoto wetu kwani tulishuhudia awamu iliyopita ikighubikwa pia na wimbi la vifo vya watoto wetu waliojiunga JKT baada ya mafunzo haya kuanzishwa tena.
Sina uhakika kama askari wanaopokea watoto hawa wamepewa mafunzo maalum ya kuwa treat watoto ambao ndio kwanza wanatoka mazingira ya shule na kwenda jeshini.
Inawezekana kabisa maaskari walioko kambini na jeshini kwa zaidi ya miaka 5-20 kutaka kuwa transform wanafunzi hawa kuna wanajeshi kama wao katika kipindi kifupi hiki cha miezi 3.
Siamini hata iweje kuwa kipindi cha miezi mitatu mwanafunzi anayokaa JKT kitatosha kumfanya afikie calibre ya Uanajeshi mkakamavu.
Hii ni sawa na kulazimisha mimba ya mtu kutungwa na mtoto kuzaliwa katika kipindi cha miezi mitatu, jambo ambalo haliwezekani.
Ni lazima wajue wao walikuwa wanajeshi kamili baada ya mafunzo ya muda mrefu wakipitia hatua moja baada ya nyingine na huu ni utaratibu ambao naweza kusema ni natural phenomenal.
Kitendo cha kuwataka wanafunz hawa wawe wanajeshi kamili kwa muda mfupi kinawafanya askari hawa kuwa subject katika harsh environment kwa ghafla.
Ikumbukwe hata mche wa mmea unapohamishiwa kwenye shamba kubwa kutoka kwenye kitalu huhitaji uangalizi wa karibu kikiwemo kivuli, maji na bada ya muda unashika chini na kuanza kupambana kustahimili mazingira magumu wenyewe.
Wanafunzi hawa ni kama miche iliyotolewa katika kitalu na hivyo wanahitaji mafunzo yawachukue hatua kwa hatua hadi watakavvozoea na si ku wa induce kuwa full wanajeshi overnight.
Hapa mtawaua wengi!!!. na hiki ndicho chanzo cha vifo na vipigo. Tofauti na huko nyuma, wanafunzi wanaoingia JKT sasa wana umri mdogo ukilinganisha na sisi tulivyoingia kipindi cha miaka ya nyuma hadi JKT kwa mujibu wa sheria iliposimamishwa miaka ya 1996/97.
Mzazi anategemea mtoto akitoka JKT arudi kujiunga University lakini badala yake wanapokea maiti na walemavu na hivyo kukatiza juhudi zote za kumsomesha mtoto yule.
Hiki sicho mzazi alichotarajia hata kidogo. Wazazi wamekuwa na hofu kubwa hususani kutokana na aina ya mafunzo yanayotolewa na kugharimu maisha ya watoto wap. Inakuwa kama mtoto amekwenda vitani mstari wa mbele!!!.
Tunawasihi maafande wawaone watoto hawa kama watoto wao, watangulize utu mbele badala ya ukatili na kama kweli wana facilities za afya mtoto akiumwa basi wasiwa tease na kuona wana deka.
Kama hatua hazitachukuliwa tutakuwa tukishuhudia vifo vya watoto wetu miaka nenda rudi na JKT zitachukuliwa kama kambi za mateso na vifo kama zile za Adolph Hitler (concentration camps) na si kambi za mafunzo.
Mimi kama mzazi naiomba serikali ifanye uchunguzi wa sababu ya vifo na vipigo katika kambi za JKT ili wanaohusika au kuzembea wakibainika wachukuliwe hatua kali ikiwamo kufukuzwa kazi.
Lakini pia watoe mafunzo maalum kwa askari watakao kuwa wakiwafundisha wanafunzi kutoka mashuleni.